Profile ya Dr Slaa

Status
Not open for further replies.
First Name: Dr. Wilbrod
Middle Name: Peter
Last Name: Slaa
Member Type: Constituency Member
Constituent: Karatu
Political Party: CHADEMA
Office Location: P.O. Box 119, Karatu – Arusha
Office Phone: +255 784 666995
Ext.:
Office Fax: +255 22 2668866
Office E-mail: wslaa@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 29 October 1948
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start
Date End Date Level
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health
1993 1993 CERTIFICATE
TransWorld Tutorial College, London Certificate in
Management 1985 1985 CERTIFICATE
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in
Rural
Development 1980 1981 ADV
DIPLOMA
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977
1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974
1977 CERTIFICATE
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy
1972 1973 CERTIFICATE
Itaga Seminary School A-Level Education 1970
1971 HIGH
SCHOOL
Dung’unyi Seminary School O-Level Education 1966
1969 SECONDARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965
PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961
PRIMARY
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary
Education 1958 1960 PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992
1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General
1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu – Roman Catholic
Church Padre 1977 1991
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu
Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive
Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi – CCM Secretary Foreign
Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
 
Msipende kurudia rudia mambo. Kama wewe umezaliwa jana uliza wakubwa zako hapa jukwaani. Unataka CV ya mtu iwekwe jukwaani kila mwaka?. Weka ya kwako kwanza ili hoja yako iwe na mashiko.
 
Wanajamvi; nimekuwa najaribu kutafakari hatua ya Dr. Wilbroad Peter Slaa kuchukua "sabbatical leave" wakati nyeti na tete kiasi hichi tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu na joto la kisiasa liko juu kuliko wakati mwingine wowote tangu nchi yetu ilipoingia katika mfumo wa ushindani wa kisiasa; sababu tunayoisikia kwa baadhi ya viongozi waandamizi katika muungano wa UKAWA eti ameamua kufanya hivyo kama hatua ya "kupinga Edward Lowassa kujiunga na CHADEMA/UKAWA" sina hakika maana mimi sio kati ya watu walioko ngazi za maamuzi katika CDM/UKAWA!

Namshangaa kiasi fulani Dr Slaa haswa pale ninapotafakari barabara yake ya maisha mpaka kufikia Dr. Slaa gwiji wa siasa hapa tanzania?!

Nionavyo mimi Dr. Slaa ni mtu ambaye wakati mwingine anasimamia kwa wivu sana jambo ANALOLIAMINI lakini wakati mwingine hugeuka na kusimamia pia kwa wivu mkubwa jambo ASILOLIAMINI!!

Hebu tutafaklari haya kwa kifupi sana?!

ISIDINGO THE NEED No 1 ya Dr Slaa: Alikuwa padiri wa kanisa katoliki; kanisa kubwa na lenye misimamo MIZITO na MIGUMU (DOGMATIC) isiyobailika badilika mpaka uitishwe mkutano wa kilele katika kanisa hilo unaoitwa MTAGUSO! Dr Slaa "alibwaga manyanga"! mimi sijui alitofautiana nini na misimamo ya kanisa lake lakini ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba Dr Slaa sio kasisi tena wa kanisa katoliki. that is in the public domain.

ISIDINGO THE NEED No 2 ya Dr Slaa: Alipanda madhabahuni akafunga ndoa na mke wake aitwaye Bi Rose Kamili; sio siri pia kwamba Dr Slaa alimbwaga Rose kamili na kwa sasa anaishi na Bi Josehine Mushumbusi kama mume na Mke! kama ilivyo katika tamthilia yake ya kwanza; sina hakika nini kilijiri Dr amambwaga Rose kamili; sijui na sitaki kujua!

ISIDINGO THE NEED No 3 ya Dr Slaa: 1995Dr akaingia kwenye ulimwengu wa siasa; akajaribu kugombea ubunge katika jimbo lake la nyumbani Karatu; AKAKATWA! akabwaga manyanga akaingia CHADEMA; akatumikia CHADEMA kama mbunge wa Karatu kwa muda wa miaka 15 mfululizo; akaachia kijiti na kuendelea kutumikia CDM kama Katibu mkuu kwa muda wa miaka 5 sasa.

ISIDINGO THE NEED No 4 ya Dr Slaa: Kwa taarifa za uhakika kwa sababu Mwenyekiti wa CDM Kamanda Freeman Mboiwe ametoa tamko kwa umma; kwamba Dr. Slaa ameamua kwenda mapumziko ya muda!! kwa kuzingatia timing ya hiyo "Sabbatical leave" yake; kuelekea uchaguzi mkuu 2015!! nachelea kutamka kwamba hiyo ndiyo Bye Bye ya Dr Slaa kwa CDM/UKAWA!; natamani prophesy yangu hii isiwe kweli!!!!!

Wanajamvi; je tumkumbuke vipi huyo Dokta wa kiwango?! 1. A principled man without principles! au 2. An Enigmatic world class technocrat with a BIG EGO!!!

Baada ya kuyasema hayo; mimi Kama mwana mageuzi na mwanachama wa CDM/UKAWA; nitakuwa mtovu wa fadhila kama nisipomalizia uzi huu kwa kumshukuru na kumpongeza kwa dhati kabisa Kaka yetu Dr Wilbroad Peter Slaa kwa utumishi wake uliotukuka kwa nchi hii; CDM/UKAWA na VUVGUVUGU la mabadiliko katika ujumla wake.
Asante sana Dr Slaa; Mwenyezi Mungu akupe nguvu; afya njema na faraja wakati huu ambao kwa namna moja au nyingine tunajua unapitia katika kipindi kigumu kijamii na kisaikolojia.

Nawasilisha
MTK
 
Umeeleza mabadiliko ambayo yamekuwa yakitokea katika maisha ya Dr kwa mtiririko wa matokeo ambayo ninaamini kila moja limetokea kwa sababu kwa kuwa ni jambo la kawaida katika maisha ya binadamu. Inaweza kusababishwa na internal ama external irresistible forces. Historia huwa ni somo la kutukumbusha tulikotoka na wapit tulifanya vyema na wapi tulikosea lakini knowledge sahihi hutufanya tusimame kwenye mwelekeo sahihi ukizingatia kila kitu kinaevolve.

Ninatamani Dr. Slaa ninayemfahamu kama muungwana, asiye na unafiki wala woga, angesimama upande wa taifa alilolipigania kwa muda mrefu. Ninatamani msimamo wake wa kuthamini na kuwajali wanyonge angeuendeleza katika kipindi hiki cha mabadiliko ili ayaongoze mabadiliko hayo yasiharibu misingi aliyoiamini akaiweka na kuipigania kiasi cha gharama kubwa. Ninatamani angelikuwa kama wale wazazi ambao huvumilia moto ndani ya mahusiano kwa ajili ya watoto wawapendao.

Lakini badala ya kuja na kutuambia ametutelekeza tujue wenyewe, ni afadhali anyamaze kimya.

Ingawa ukweli sikubaliani na maneno ninayoyasikia hapa na pale kwamba DR. Slaa anayeheshimika na kuthaminika ndani ya nje ya CHADEMA Tanzania na nje ya mipaka ya nchi, anaweza kuishia kimtindo namna hii!. Hili halipo. Ninacholazimika kukiamini ni kwamba anatuliza akili zake na kujipanga upya katika awamu nyingine ya mapambano ya ujenzi wa Tanzania mpya ambao ni muhimu kama ilivyo kuiondoa ccm madarakani.

Ninajua uraisi alikuwa hataki na ndiyo sababu alisema hatagombea kwa kuwa familia yake ilimkataza na lakini pia ninaona nia yake njeme ya kumtafuta lowasa kama mbadala. Sasa abaki aongoze hayo mabadiliko ili yaende katika misingi ya Tanzania tuitakayo yeye kama role model wetu.

Tukiiondoa ccm na kumweka Lowasa, haitoshi bila kuwa na nguvu kubwa pale juu ya kutoa miongozo na mwelekeo sahihi wa kuwafikisha Wtanzania katika nchi yao iliydhurumiwa na ccm. Haitakuwa na maana kuiondoa ccm na kuanza kufanya yale yale ya ki ccm.

KWA MANTIKI HIYO, NINAJUA DR. IS A BRAVE PERSON, ATAKUWA LIKIZO MCHAKATO WA LOWASA NA MISSION YAKE YA KUIONDOA CCM IKIKAMLIKA, LAKINI SOON TUTAMWONA DR. WETU AKIINGIA UWANJANI KWA AJLI YA UONGOZI WA UJENZI WA TANZANIA MPYA.
 
endeleeni kumdhihaki mzeee wetu ula kuna mda mtarudi kumuomba muungane nae lakini itakuwa too late
 
Slaa ameamua kupumzika ni uamuzi wake uheshimiwe na kila mtu.!
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom