Wasifu (CV) ya Dr. John Pombe Magufuli

Magufuli hajaamua CCM! Alikuepo toka zamani, LOWASA alishawahi kua kiongozi wa CCM ngazi ya Taifa, vyote ni vyama vya siasa kazi ni moja.

Vyama tofauti,vyenye mifumo ya uongozi na sera tofauti,siasa tofauti,malengo tofauti
 
Magufuli atakuwa mwenyekiti wa ccm wa kwanza bila kuwa raisi.
POMBE MWISHO KAUNTA MTAANI NA IKULU LOWASA ANATOSHA.
 
He! Mimi nilikua silijui hili!,

Nimekutana na Mzee mmoja mkongwe wa CCM leo asubuhi mtaani kwetu akanambia; "Aisee CCM wanakiua chama hivi hivi,wanafikiri wamemaliza makundi lakini subiri utajionea mwenyewe!Eti huyu ndio aje kua M/kiti wa chama! yaani wao badala ya kuchagua kiongozi mwenye historia ya kukiongoza chama na kukijua vizuri, leo wamekosa kiongozi mwenye sifa mpaka wakachagua mtu ambaye hata hajui CCM imeanzia wapi?

Yeye anajua tu idadi ya barabara na samaki tu! Haujui hata muundo wa uongozi wa ndani ya Chama, Ni bora hata ya Mwigulu ambaye ndani ya muda mfupi nafasi ya N/katibu mkuu CCM bara kakifahamu chama vizuri, ni bora hata Lowassa pamoja na kuhama kwake lakini anajua namna vyama vinavyoendeshwa kwa uzoefu wake wa uongozi wa miaka mingi ndani ya CCM"

Aidha huyo mzee akaendelea kusema kwamba" Angalia hata kampeni za Magufuli! ni za hofu,jazba,kutetemeka, kukosa kujiamini mbele ya umma, Lakini Lowassa yeye hana hofu anafanya yake kimya kimya akijiamini kua Magufuli sio size yake! kwahiyo kijana ukweli tunaujua asikudanganye mtu"

Halafu anatamba ati hajawahi kushindwa uchaguzi. 1990 alishindwa kwenye kura ya maoni tena ya lichama lao hilo li CCM! Hilo anasemaje ?
 
Nachokiona atakuwa mwenyekiti wa ccm taifa alafu baadaye sana ndio aje agombee urais
 
Vyama tofauti,vyenye mifumo ya uongozi na sera tofauti,siasa tofauti,malengo tofauti
Hoja nyepesi! Dr Slaa ni katibu mkuu wa CHADEMA taifa, alihamia toka CCM alikuta CHADEMA wana mfumo waao wa kiuongozi zaidi aliongezea uzoefu wake.
 
Magufuli atakuwa mwenyekiti wa ccm wa kwanza bila kuwa raisi.
POMBE MWISHO KAUNTA MTAANI NA IKULU LOWASA ANATOSHA.
'Kama kuna mtu anampenda sana lowasa akanywe naye chai, ikulu so pango la wanyang'anyi' by Nyerere 1995.
 
ila amekuwa mbunge kwa miaka 20, waziri na sasa ni mgombea urais wa CCM na ndio rais wa awamu ya tano anayesubiri kuapishwa
 
Hoja nyepesi! Dr Slaa ni katibu mkuu wa CHADEMA taifa, alihamia toka CCM alikuta CHADEMA wana mfumo waao wa kiuongozi zaidi aliongezea uzoefu wake.

Sasa kwa nini mmembwaga Slaa mkaweka huyo fisadi wakati slaa ana uzoefu mkubwa kwenye chama hadi kuwa katibu mkuu wa chama?
 
Magufuli ni mtendaji, mtumishi/mtumwa. Hufanya jambo kwa ufasaha(ingawa kuna ujanja) ila hawezi kuongoza chama na hana uzoefu hata kidogo. Hivyo maamuzi hayatakuwa yake/hayawezi kuwa yake.

Pengine uwaziri mkuu unaweza kumfaa, kama akipunguza jazba na kuropoka ropoka ovyo
 
Habari ndugu,
watakaoelewa na waelewe..na
Ili kunielewa mada yangu naomba usilete ushabiki wa chadema uweke kando kuwa kama mtu mwenye fikra huru..mwanzo nilijua kifungo kibaya kwa mwanadamu ni dini pekee ipo kwa ajili ya wachache kunufaika uwongo mwing ndani yake,nisigusie sana kuhusu dini ili kuepusha kuchokoza watu kiimani
Kifungo cha pili alichoweza kufungwa binadamu ni siasa...tumefanywa mitaji na binadamu wenzetu hivi vyama vinaendeshwa na watu kama sisi na tunajua watu tuna sifa za unafki,tamaa,uwongo kama wewe usivo na huruma na wengne basi tambua hata huyo unayemwona mchapakazi au mkombozi vile vile ni binadamu na anajionea huruma yeye kuliko anavyokuonea wewe
unajua siasa ina mambo mengi wananchi sasa hivi hatufanyi reasoning tumeishia kutumika kama mitaji ya wanasiasa
Leo hii tunawashabikia viongozi wa ccm au wa ukawa tunajifanya hatuoni kama wenyewe wako pale/watakuwepo kwa ajili ya maisha yao,familia zao na koo zao..tupo kama misukule
Inauma sana great thinker amefanywa kama mtumwa chini ya tajiri lowasa au mbowe tunajifanya hatuoni kama wale wanapesa/wanataka pesa kama kweli wangekuwa na nia na huruma na wananch kwanini wasituambia sera zao wazi ni lini rasilimali zetu zitakuwa chini ya serikali watakayounda,tumeishia kuwashabikia.ndugu zangu wale hawana uzalendo
Ukirudi kwa upande wa ccm ndo matatizo matupu najuta kuzaliwa tanzania nchi hi wanafaidika wachache kama kweli kina kikwete na magufuli wangekuwa na huruma wangewezaje kuwatazama maskini wa kutupwa vijijini ilihali hata mlo hawapati..tunaona tumeletewa maendeleo kumbe ndo wananufaika wenyewe mfano eti mtu anaisifia serikali ya ccm imemsaidia yeye sasa iv ana smartphone hajiulizi kama amenunua hvo amenufaisha mtengenezaji na mtengenezaji naye kamuwezesha mwanasiasa kisha anaekewa mifumo inayomkinda..siasa bwana unafurahia serikali ya ccm eti imejenga barabara unasahau kama ni kwa pesa zako unasahau pia kama hzo barabara ni kwa ajili ya kuwarahisishia kupitisha mizigo yao ambayo wanakuuzia tena kwa pesa yako
Tusidanganyane siasa ni mchezo unaocheza na akili ya binadamu,sisi ni watumwa tunashangilia maigizo ya binadamu wenzetu ambao hawatupi elimu ili tuendelee kuwa wapumbavu
Hakuna atakaye kuja kutukomboa only strong ndo wata survive wengne tutaendelea kulalamikiwa na vizazi vinavokuja kwa maamuzi tunayofanya sasa kwa ushabiki..watoto wetu watakuja kushangaa kwa nini tulisikiaga kuwa kuna watu walichota mabilion lakini hawaulizwa?watoto wetu watakuja kushangaa mmoja wapo wa anayesemakana fisadi anashangiliwa kwanini tunajisahaulisha mapema hivi?binadamu tuna tatizo gani?
Ccm mmetupoteza mpaka wasomi na watu wanajiita watakatifu(viongozi wadini)mme wanununua hivo hivo pia kwa upinzani mnadanganya mpaka ma great thinker humu ndani wanawashabikia..jibu ni kuwa na nyie mnadanganya na wazungu (wawekezaji) kwa kupewa uwongo kisha mnatapeliwa ,siasa mfumo wa kijinga sana mtu kweli unajikuta unamshabikia mwizi au yule ambaye sio mwizi unamwona hafai
Taifa hili linachekesha,viongozi wote wanachekesha,wananchi mnachekesha hivi mnadhani wale waarab wanavofanya vita kulinda rasilimali mnadhani wanakosea..walioiba mabilioni wanaonekana wazuri
UKAWA MMEONEKANA MNAWEZA KULETA MABADILIKO WANAYOTAKA WATU LAKINI JE MBONA KUNA MAMBO HAMUWEKI SAWA?NI KIVIPI MTAZUIA MAKAMPUNI KUMILIKI RASILIMAL ILA TAIFA NDO LIMILIKI KILA KITU AU NDO YATAKUWA KAMA CCM KUACHIA WATU WAVUNE MADINI?WAZUNGU WATU WABAYA SANA
Ukawa ningewaona wa maana kama mnge utangazia umma kuwa mkishka nchi rasilimal zitalindwa nyie mnasubiri mpaka siku ya kufungua kampeni ili mkusanye watu wengi lengo ni kuwa lipiza ccm?ETI LEO SIASA ZA TANZANIA ZINABEBWA NA MISAMIATI YA KITOTO MFANO KILA CHAMA KINATAKA KIPATE MAFURIKO siasa za majitaka sana
Embu jiulize kwani kampeni zikifunguliwa kwenye ukumbi mfano mlimani city hazitafunguka?
MY TAKE:NAJUA WENGI MTANIDHARAU KWAMBA NIMEANDIKA ULOFA LAKINI LAZIMA TUJUE KUWA SISI TUNASHABIKIA UTUMWA CHINI YA BINADAMU WENZETU KIPINDI TUNARUSHIANA VIJEMBE JUU VISIVYO NA UMUHIMU KULE WENGNE WANAKULA VIZURI WENGNE VBY
Nimejitoa rasmi kwenye ushabiki nataka niwe mtu huru kichwan nibaki na vitu vya msing vinavyonihusu mimi moja kwa moja
USHABIKI UNAKWENDA KUHARIBU TAIFA MTANIAMBIA
Waasalam
 
Ni kweli hajawahi kushika nafasi hizo.
Lakini huo uwezo alikuwa nao na jinsi ya kuongoza anajua. Yeye kuwa M/Kiti wa CCM anafaa kabisa.

ANGALIZO; Kuwa M/Kiti wa CCM sio kwenda kulima au kubeba magunia bali ni kufuata kanuni na taratibu
za chama KUONGOZA.

Jambo la mwisho, MAGUFULI ndio Rais wako wa Tano. Ikulu ipo kwa ajili ya CCM tuu.

Mandla.

Sitawaangusha hehehehe
 
Wasiwasi wangu ni pale betri ya pace marker itakapo kuwa imeishiwa chaji na kuna maamuzi muhimu kama kiongozi anatakiwa ayatoe.
 
Habari ndugu,
watakaoelewa na waelewe..na
Ili kunielewa mada yangu naomba usilete ushabiki wa chadema uweke kando kuwa kama mtu mwenye fikra huru..mwanzo nilijua kifungo kibaya kwa mwanadamu ni dini pekee ipo kwa ajili ya wachache kunufaika uwongo mwing ndani yake,nisigusie sana kuhusu dini ili kuepusha kuchokoza watu kiimani
Kifungo cha pili alichoweza kufungwa binadamu ni siasa...tumefanywa mitaji na binadamu wenzetu hivi vyama vinaendeshwa na watu kama sisi na tunajua watu tuna sifa za unafki,tamaa,uwongo kama wewe usivo na huruma na wengne basi tambua hata huyo unayemwona mchapakazi au mkombozi vile vile ni binadamu na anajionea huruma yeye kuliko anavyokuonea wewe
unajua siasa ina mambo mengi wananchi sasa hivi hatufanyi reasoning tumeishia kutumika kama mitaji ya wanasiasa
Leo hii tunawashabikia viongozi wa ccm au wa ukawa tunajifanya hatuoni kama wenyewe wako pale/watakuwepo kwa ajili ya maisha yao,familia zao na koo zao..tupo kama misukule
Inauma sana great thinker amefanywa kama mtumwa chini ya tajiri lowasa au mbowe tunajifanya hatuoni kama wale wanapesa/wanataka pesa kama kweli wangekuwa na nia na huruma na wananch kwanini wasituambia sera zao wazi ni lini rasilimali zetu zitakuwa chini ya serikali watakayounda,tumeishia kuwashabikia.ndugu zangu wale hawana uzalendo
Ukirudi kwa upande wa ccm ndo matatizo matupu najuta kuzaliwa tanzania nchi hi wanafaidika wachache kama kweli kina kikwete na magufuli wangekuwa na huruma wangewezaje kuwatazama maskini wa kutupwa vijijini ilihali hata mlo hawapati..tunaona tumeletewa maendeleo kumbe ndo wananufaika wenyewe mfano eti mtu anaisifia serikali ya ccm imemsaidia yeye sasa iv ana smartphone hajiulizi kama amenunua hvo amenufaisha mtengenezaji na mtengenezaji naye kamuwezesha mwanasiasa kisha anaekewa mifumo inayomkinda..siasa bwana unafurahia serikali ya ccm eti imejenga barabara unasahau kama ni kwa pesa zako unasahau pia kama hzo barabara ni kwa ajili ya kuwarahisishia kupitisha mizigo yao ambayo wanakuuzia tena kwa pesa yako
Tusidanganyane siasa ni mchezo unaocheza na akili ya binadamu,sisi ni watumwa tunashangilia maigizo ya binadamu wenzetu ambao hawatupi elimu ili tuendelee kuwa wapumbavu
Hakuna atakaye kuja kutukomboa only strong ndo wata survive wengne tutaendelea kulalamikiwa na vizazi vinavokuja kwa maamuzi tunayofanya sasa kwa ushabiki..watoto wetu watakuja kushangaa kwa nini tulisikiaga kuwa kuna watu walichota mabilion lakini hawaulizwa?watoto wetu watakuja kushangaa mmoja wapo wa anayesemakana fisadi anashangiliwa kwanini tunajisahaulisha mapema hivi?binadamu tuna tatizo gani?
Ccm mmetupoteza mpaka wasomi na watu wanajiita watakatifu(viongozi wadini)mme wanununua hivo hivo pia kwa upinzani mnadanganya mpaka ma great thinker humu ndani wanawashabikia..jibu ni kuwa na nyie mnadanganya na wazungu (wawekezaji) kwa kupewa uwongo kisha mnatapeliwa ,siasa mfumo wa kijinga sana mtu kweli unajikuta unamshabikia mwizi au yule ambaye sio mwizi unamwona hafai
Taifa hili linachekesha,viongozi wote wanachekesha,wananchi mnachekesha hivi mnadhani wale waarab wanavofanya vita kulinda rasilimali mnadhani wanakosea..walioiba mabilioni wanaonekana wazuri
UKAWA MMEONEKANA MNAWEZA KULETA MABADILIKO WANAYOTAKA WATU LAKINI JE MBONA KUNA MAMBO HAMUWEKI SAWA?NI KIVIPI MTAZUIA MAKAMPUNI KUMILIKI RASILIMAL ILA TAIFA NDO LIMILIKI KILA KITU AU NDO YATAKUWA KAMA CCM KUACHIA WATU WAVUNE MADINI?WAZUNGU WATU WABAYA SANA
Ukawa ningewaona wa maana kama mnge utangazia umma kuwa mkishka nchi rasilimal zitalindwa nyie mnasubiri mpaka siku ya kufungua kampeni ili mkusanye watu wengi lengo ni kuwa lipiza ccm?ETI LEO SIASA ZA TANZANIA ZINABEBWA NA MISAMIATI YA KITOTO MFANO KILA CHAMA KINATAKA KIPATE MAFURIKO siasa za majitaka sana
Embu jiulize kwani kampeni zikifunguliwa kwenye ukumbi mfano mlimani city hazitafunguka?
MY TAKE:NAJUA WENGI MTANIDHARAU KWAMBA NIMEANDIKA ULOFA LAKINI LAZIMA TUJUE KUWA SISI TUNASHABIKIA UTUMWA CHINI YA BINADAMU WENZETU KIPINDI TUNARUSHIANA VIJEMBE JUU VISIVYO NA UMUHIMU KULE WENGNE WANAKULA VIZURI WENGNE VBY
Nimejitoa rasmi kwenye ushabiki nataka niwe mtu huru kichwan nibaki na vitu vya msing vinavyonihusu mimi moja kwa moja
USHABIKI UNAKWENDA KUHARIBU TAIFA MTANIAMBIA
Waasalam
 
Mmmmh!!! Mijini watu wanajitambua sijajua kwa ndugu zetu wa vijijini, maana hivi kupewa wali maharage kunaweza kupelekea kuuza kura zao kweli?? Mabadiliko yanahitajika
 
Attachments

  • 1440659771760.jpg
    1440659771760.jpg
    37.4 KB · Views: 169
CV YA Dr MAGUFULI
NGULI WA SAYANSI NA RAIS MTRAJIWA AWAMU YA 5:

Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.

Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.

Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.

Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.

Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)

Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.

Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
[12:08, 27/08/2015] Ayub Cmn:
Pamoja na kuwa busy na mambo ya kazi za siasa, Uwaziri na Ubunge, Mheshimiwa Magufuli aliweza kusoma na kumaliza PhD yake pale UDSM jambo ambalo ni la kupigiwa mfano tofauti na Mbunge mmoja wa Upinzani aliyeshindwa kumaliza Shahada yake laini (BBA) hapo hapo UDSM miaka nenda rudi.BAADHI YA MACHAPISHO/PUBLICATIONS YA MTEULEMulokozi A. M.; Akwilapo, L.D.: Buchweishaija, J.; Magufuli J. P., and Kyobe, J. ¿Securing the Mechanism of the Decomposition of CaCO3 by the Thermodynamics of the Reaction¿, East and Southern Africa Environmental Chemistry Workshop, pp 71-83, 1st ¿ 5th December 2003, Dar es Salaam 5 Dec 2003
Magufuli, J. P., ¿Funding requirements for the EAC Road network project the East African Community Roads Development partners Consultative meeting 29th ¿ 30th April, 2003 Arusha Tanzania. 30 Apr 2003
Magufuli, J. P., (MP) PIARC First Delegate and Minister for Works of the United Republic of Tanzania.¿ Access to Mobility a basic Social Service, Special Trunk Roads project, Design and Build Tanzania model, XXIInd World Road Congress, 19 ¿ 25 October, 2003 Durban, South Africa. 25 Oct 2003
Mulokozi, A. M., Kyobe, Magufuli, J. P. and R. Whitehead. ¿A New Rate Equation for Solid State Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3. TCS Inaug. Conf. Proc., 11 ¿ 16 July, 1999, p162 ¿ 183. 16 July 1999
Magufuli, J. P., ¿Background of the Mtwara Development Corridor¿ Meeting of the head of States from Malawi, Tanzania, Zambia and Mozambique during the Rounding of the Mtwara Development Corridor, 15 December, 2004, Lilongwe ¿ Malawi.
 
CV YA Dr MAGUFULI
NGULI WA SAYANSI NA RAIS MTRAJIWA AWAMU YA 5:

Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.

Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.

Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.

Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.

Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)

Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.

Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.[12:08, 27/08/2015] Ayub Cmn:
Pamoja na kuwa busy na mambo ya kazi za siasa, Uwaziri na Ubunge, Mheshimiwa Magufuli aliweza kusoma na kumaliza PhD yake pale UDSM jambo ambalo ni la kupigiwa mfano tofauti na Mbunge mmoja wa Upinzani aliyeshindwa kumaliza Shahada yake laini (BBA) hapo hapo UDSM miaka nenda rudi.

BAADHI YA MACHAPISHO/PUBLICATIONS YA MTEULE
Mulokozi A. M.; Akwilapo, L.D.: Buchweishaija, J.; Magufuli J. P., and Kyobe, J. Securing the Mechanism of the Decomposition of CaCO3 by the Thermodynamics of the Reaction¿, East and Southern Africa Environmental Chemistry Workshop, pp 71-83, 1st ¿ 5th December 2003, Dar es Salaam 5 Dec 2003

Magufuli, J. P., Funding requirements for the EAC Road network project the East African Community Roads Development partners Consultative meeting 29th 30th April, 2003 Arusha Tanzania.30 Apr 2003
Magufuli, J. P., (MP) PIARC First Delegate and Minister for Works of the United Republic of Tanzania.

Access to Mobility a basic Social Service, Special Trunk Roads project, Design and Build Tanzania model, XXIInd World Road Congress, 19 25 October, 2003 Durban, South Africa. 25 Oct 2003
Mulokozi, A. M., Kyobe, Magufuli, J. P. and R. Whitehead.

A New Rate Equation for Solid State Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3. TCS Inaug. Conf. Proc., 11 16 July, 1999, p162 183. 16 July 1999 Magufuli, J. P., Background of the Mtwara Development Corridor Meeting of the head of States from Malawi, Tanzania, Zambia and Mozambique during the Rounding of the Mtwara Development Corridor, 15 December, 2004, Lilongwe Malawi.
 
Back
Top Bottom