Professor Rwekaza Mkandala na Uongozi mbovu University of Dar es Salaam

Pamoja na Matatizo mengine lakini tatizo kubwa ni kukabidhi kila kitu kuanzia akili zetu kwa mtu mmoja anayeitwa RAIS. Huyo Mkandara na Bana lazima wawajibike kwa BWANA yao aliyewaweka hapo. Matatizo mengine na hasa ya uawajibikaji yangeweza kuepukika kama VC itakuwa ni POST watu wanaomba kulingana na qualification, wanafanyiwa interview then finally anachaguliwa na JOPO la WATAALAMU wenzake. Lakini hii ya kuwa picked up with a single handed man kamwe haiwezi kuleta uwajibikaji. Sijui kwanini Wasomi wa UDSM wameshindwa kupigania hili!

Ninasikitika sana kusikia UDSM sasa hivi iko hivyo. Sisi tuliosoma enzi zile 80s hayo mambo ya kubebana sijui kulenga choo etc hayakuwepo!!

Mungu wangu tuepusha na haya, tumeua viwanda sasa tunaua VYUO VIKUU, SIJUI tutakuwa TAIFA gani katika SAYARI hii?!.
 
UDSM wanaongoza kwa ruzuku na goverments funding lakini ufisadi wake wake sijui hata uanze wapi..

UDSM muhimili ya kifaisadi umesukwa na Prof. wa ufisadi Mahalu..
 
Mzazi umenena UDSM sasa ni aibu Mkandala alifanya ziara ya chuo hapo lini maana inakuwa kama yuko another country hivi ndo watu wa JK hao mzazi kula tu!
 
Ndugu asante kwakusubutu kuiambia umma madudu yaliopo hapo UDSM. mimi pia nimesoma hapo nilipata hiyo kero sana.
nilikaa hall 3, then hall 6 nikamalizia hall 5 ghorofa ya tano room number sizikumbuki ila miaka imepita sihaba.

Ila kwa ushauri wangu uongozi ufanye maintenance kwani nihatari sana. kwahi hall two na five kuna vipisi vyo concrete au vipisi vya tofali vinadondoka kutoka juu , nakikimkuta mtu anayepita pale chini sihatari sana wajameni.

Naamini wanao jua mazingira ya hall 2 na five atamuunga mkono mtoa hoja.
Poleni sana wana UDSM.




mkuuu mim nilikoswa koswa na concrete pale hall2 mwaka 2007 nikiwa 1rst year sikutgemea mpaka na graduate pawe vile vile lakin mpaka leo hamna walicho repair zaiidi ya lift
 
Tembelea mabibo hostel vyooni ni kama mabwaya ya samaki au mpunga ukienda kuoga utadhani unavuna mpunga
 
siombei mabaya yatokee lakini hayo majengo chakavu yataporomoka karibuni

da me naombea tu isianguke before cjamaliza mwishoni wa mwezi wa sita maana ndo naishi hall 5, na lianguke kipindi cha likizo kubwa ili liangukie kwenye majengo yao wenyewe wapate hasara,kiukweli majengo yanatisha ile mvua ya jana alfajiri ilikuwa na upepo mkali sana kwa jinsi jengo lilivyochoka nkahisi kama linataka kuanguka, nilishaanza kuwaamsha wenzangu tushuke chini tukalale hall 6, kiukweli hall5 hall2 yanahali mbaya, nmeingia hapa 2008 walau mabomba ya mvua yalikuwa yanatoa maji kwa uchache ila siku hizi hamna kitu kabisa, hata lifti ya hall 5 ina zaidi ya miaka miwili haifanyi kazi, vyoo vingi vimefunikwa na mifuniko ya ndoo kwa sababu vimeharibika kabisa. Kwa ukweli ckuhizi ud hakuna daruso .daruso iliisha 2008 ile ya machibya hawa wote wanaokuja ni waoga na wanaangalia vitambi vyao, wanaongeza na kuomba misaada na kukopa bank ya dunia ili kujenga madarasa na majengo yao ya anasa, ukifikiria sana unaweza kulia. Kuna haja ya kuitisha mgomo juu ya haya yote, mimi naishi hall5 na nategemea kumaliza mwaka huu.
 
mkuuu mim nilikoswa koswa na concrete pale hall2 mwaka 2007 nikiwa 1rst year sikutgemea mpaka na graduate pawe vile vile lakin mpaka leo hamna walicho repair zaiidi ya lift
hata lifti yenyewe sasa haifanyi kazi kabisa, na concrete zinaendelea kuanguka tu kila leo
 
Napata mashaka kujua jinsia yako,ulikaa hall 3(ladies) na hall 5&6(gents),
Ndugu asante kwakusubutu kuiambia umma madudu yaliopo hapo UDSM. mimi pia nimesoma hapo nilipata hiyo kero sana.
nilikaa hall 3, then hall 6 nikamalizia hall 5 ghorofa ya tano room number sizikumbuki ila miaka imepita sihaba.

Ila kwa ushauri wangu uongozi ufanye maintenance kwani nihatari sana. kwahi hall two na five kuna vipisi vyo concrete au vipisi vya tofali vinadondoka kutoka juu , nakikimkuta mtu anayepita pale chini sihatari sana wajameni.

Naamini wanao jua mazingira ya hall 2 na five atamuunga mkono mtoa hoja.
Poleni sana wana UDSM.
 
Mmh!nakumbuka pia tar 31.12.2007,tulipata dhahama kubwa,concrete za madirisha zilidondoka toka floor ya 10 hadi chn,hali ilikuwa mbaya sana,tulinusulika kufa,hall two itakuja ua watu.
mkuuu mim nilikoswa koswa na concrete pale hall2 mwaka 2007 nikiwa 1rst year sikutgemea mpaka na graduate pawe vile vile lakin mpaka leo hamna walicho repair zaiidi ya lift
 
Ninyi ndiyo wale ambao mchana ni wacha Mungu lkini usiku ni wanga sugu, mnawezaje mkathubutu katika maisha na mazingira hayo?
Ina maana hata mkihamishiwa pale Tanganyika Parkers kawe bila ukarabati mtahamia, koz elimu mnayoipata haiwapi fursa ya kutofautisha mazingira ya kuishi binaadam hivyo mnaishia kuswagwa kama wale wanyama mazizini.
Its a time to reason and take measures.
 
Bibikuku,Kikwete ndo akaweke balbu na kusafsha vyoo si HESLB wanapeleka hela ya ada?
 
Duh kweli umeyaanika.Mi niliishi hall 2 floor ya 10 na lifti ilikuwa mgogoro mwaka 2003.Siku moja ilinizimikia nikakaa 1 hr kabla ya kuokolewa na tangu siku hiyo nikawa nahesabu ngazi mpaka ghorofa ya 10.
 
kaka mimi nimeamua kukimbia kabisa maana ni hatari tena hatari sana haiwezekani room ya watu wawili mnalala watu 6 hii ni hatari ni ipo siku tutakutwa na madhara makubwa na hili pia linachangiwa na udhaifu wa uongozi wa daruso mi nashauri bora daruso tuizike kabisa hakuna maana ya kuwa na daruso ambayo viongozi wake hawawajibiki kwa wanauma wa chuo
 
Mtoa Mada!
Wewe si wa kwanza kusoma UDSM ati unajidai unashangaa hali ya hapo wapo waliopita kabla yako na sasa either kwa Certificate, Diploma, Degree(Bachelor, Masters,Post Graduate Diploma or PhD) toka mwaka 1961 chuo kikiwa Lumumba na sasa wanafaidi matunda ya kujitoa kwao kusoma kwenye mazingira magumu, USHAURI WANGU wewe SOMA usipoteze muda wako mwingi kumuangalia Mukandala na watawala hapo maana haitasaidia kitu UDSM sio kwenu dogo hapo unapita tu mi nakumbuka nilikuwa nasoma Civil Engineering hapo nakaa hall 2 naenda kujisaidia ama vyoo vya COET, Chemistry au Hill Park na sasa nimeanzisha kampuni yangu na nimajiri vijana kama wewe kutwa kulalamika badala ya kufanya kazi mpaka nafikiria kuajiri wakenya wachina wewe baki kulia lia muda haukusubiri na dunia ya ajira/kujiajiri itakupokea ukiwa bado unalia kuhusu Mukandala na Dr. Benson Bana
 
Kila nikitembelea UD huwa nawaambia watu pale campus kwamba ili pabadilike pale mahala inabidi mpate uongozi wa chuo kutoka katika watu ambao hawakusoma pale, hawakufundisha pale, au chuo chochote cha kibongo. Rwekaza Mukandara na wenzie wamekulia pale pale UD, kuna mambo wameshayazoea miaka nenda rudi, hayaoni.

Mgeni anaekuja kwako anaweza ku sense kwamba nyumba yako inatoa (inanuka) lakini wewe kwa vile senses zako zishazoea ile harufu unakuwa husiki kabisaaa... sasa ndio kama pale UD. Panahitaji outsiders wapabadilishe. Mtu yeyote aliyepata fursa ya kuona maisha ya campus nyingine duniani yani ukifika pale UD unasema msalie Mtume! Jamani! Yani tunatia huruma.
 
Undergraduates mtatimuliwa wote siku si nyingi! Pale wanataka postgraduates tu. Nyie undergraduate utoto umezidi. Utaendaje kunya kwenye choo kisicho na taa eti unalenga shimo kwa hisia? Watu wa Masters na PhD hawawezi kufanya ushetani kama huo

Mkuu sasa unauliza sisi tutaendaji kunya kwenye choo kisicho na taa wakati hivyo vyoo ndivyo vilivyopo. Ulitaka tufanyaje Kaka?
 
Ndg. The Priest , sisi tulio soma zamani pale UDSM, hall 3, block B ground floor yote walikuwa wanakaa ma Gents, wamebadilisha tu miaka ya karibuni. naamini sasa umeelewa
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom