Professor Rwekaza Mkandala na Uongozi mbovu University of Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Professor Rwekaza Mkandala na Uongozi mbovu University of Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CULCULUS, Mar 13, 2012.

 1. CULCULUS

  CULCULUS Senior Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu hapa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mlimani. Kwa muda wangu wote hapa chuoni nimekuwa nikisikitika sana jinsi mambo yanavyoendeshwa. Na kwa mgeni anaetoka nje hawezi amini kuwa haya yanatokea katika Taasisi inayojikita katika Elimu (Academic), Utafiti (Resarch) na Ushauri (Consultancy).

  Imefika wakati Tawala za Vyuo vikuu (UDSM hususani) viamke ni vitambue wajibu wao. Haya ni baadhi tu ya duku duku langu hapa Chuoni:-

  I) Vyoo vingi hapa Kampasi havina Taa (Bulb). Nyakati za usiku wanafunzi tunaingia vyooni kwa kutumia uzoefu kwamba choo hiki nikienda hatua tatu nitakuwa nimefika sehemu ya kukojolea. Then ukifika unakojoa. Matokeo yake vyoo vingi vimejaa maji maji (mikojo) kwenye kordo. Kwenye Jengo la UDBS ambalo halina hata miaka 3 sasa hivi Vyoo havina taa. Mikojo inachuruzika kama chemchem!

  II) Njia muhimu za chuo, mfano kutoka Cafeteria kupitia darajani hadi Seminar Rooms (SR) hakuna taa za barabarani. Taa zilizopo haziwaki, imebaki milingoti kama urembo.

  III) Electricity Socket za Seminar Rooms (SR) hazitoi umeme tangu nimeingia mwaka wa kwanza na sasa nakaribia kumaliza. Sasa sijui ziliwekwa za nini

  IV) Kumekuwepo na ongezeko wa wimbi la wizi wa laptop hususan kwenye Parking za Magari ya pale Hill Park. Magari yanavunjwa vioo na kupekuliwa wakati Auxilliary Police ipo. Wanafunzi wengi wa Masters wamekuwa wahanga wa janga hili

  V) Kordo za mabweni hazina taa na maji ya vyoo yamekuwa yakivujia kwenye makordo na pengine kuingia hadi kwenye vyumba vya wanafunzi kwa wale walio karibu na vyoo husika.

  VI) Maji yakikatika inakuwa ni kama janga chuoni. Wanafunzi wanajisadia kwenye vyoo vya maji (Vyoo vya kuflash) bila kuwa na maji matokeo yake kinyesi kinajazana kwenye sinki la shoo utadhani kimeziba. Hii kitu tunaiita ‘deposit' kwa kweli ni kero kwa sababu harufu hutanda mabwenini na pia si salama kiafya

  VII) Bweni la Hall 2 limechoka hata ukiliangalia kwa nje ingawa wenyewe wanasema life expectancy yake bado. Sasa sijui wanataka wanafunzi walitumie hadi end of life expectancy na hatimae wadondoke nalo. Kwanza sewerage system yake imechoka na kuna baadhi ya floor maji yanandokeo kwenye kordo hadi kwenye ngazi za kutembea waenda kwa miguu.

  VIII) Kubebana bebana kwenye vitanda imekuwa tabia ya kuzoeleka. Ingawa ni fault ya wanafunzi wenyewe lakini Utawala wa Chuo nao umezembea kwa sababu hawafanyi inspection kukagua wakazi wa mabwenini. Mfano vyumba vya Hall 6, awali vilijengwa kwa ajili ya kuishi mwanafunzi mmoja moja (kwa jinsi ninavyosikia). Baadae wanafunzi walipozidi kuongezeka Chuo utawala ukaongeza kitanda kimoja kimoja kwa kila chumba na hivyo vikawa viwili viwili viwili na kwa msingi huo wanaopaswa kuishi kwenye chumba hicho ni Wanafunzi wawili tu.

  Kwa sasa inashangaza sana kila kitanda wanafunzi wanabebana na bado unakuta kuna Wanafunzi wengine wanakaribishwa wanaingiza godoro wanakuwa wanalala chini. Na huyu anaelala chini nae anambeba mwenzie. Kwa hiyo chumba kilichokuwa designed kwa kuishi Mwanafunzi mmoja, wanaishi Wanafunzi sita! Uongozi unajua lakini hauwajibiki!


  IX) Licha ya kuwa na Library kubwa na ya kisasa, haina vitabu vya kisasa. Vitabu vingi ni vya miaka ya tisini kurudi nyuma. Vitabu vya miaka ya elfu mbili ni vichache sasa(Sisemi kwamba vitabu vya zamani si vizuri). Kwa mantiki hii Wanafunzi wanakosa maarifa ya mapya na ya kisasa. Tatizo hilo ndilo limechangia Wanafunzi wengi kuamini katika matumizi ya Mitandao hususani Google katika kutafuta material ya kujisomea.

  X) Wanazuoni wengi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (na vyuo vingine pia) wamegeuka kuwa brush ya utawala uliopo madarakani. Sasa hivi hakuna tena ile dhana kwamba Sauti ya Wanazuoni ni sehemu ya Sauti ya Wananchi. Pale Watawala wapovurunda, tawala nyingi za Vyuo vikuu licha ya kuwa na Wasomi waliobobea wamekuwa kimya bila kutoa matamko. Mengi ya Matamko yao ni ya kuisafisha na kuisifia serikali iliyopo Madarakani hata pale inapopaswa ionye. Dk Benson Bana, Rwekaza Mkandala, n.k ni mifano ya wanazuoni waliogeuza Taaluma zao kuwa Brush la Watawala.
   
 2. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu asante kwakusubutu kuiambia umma madudu yaliopo hapo UDSM. mimi pia nimesoma hapo nilipata hiyo kero sana.
  nilikaa hall 3, then hall 6 nikamalizia hall 5 ghorofa ya tano room number sizikumbuki ila miaka imepita sihaba.

  Ila kwa ushauri wangu uongozi ufanye maintenance kwani nihatari sana. kwahi hall two na five kuna vipisi vyo concrete au vipisi vya tofali vinadondoka kutoka juu , nakikimkuta mtu anayepita pale chini sihatari sana wajameni.

  Naamini wanao jua mazingira ya hall 2 na five atamuunga mkono mtoa hoja.
  Poleni sana wana UDSM.
   
 3. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Naomba umforwadie na Mkandala inawezekana asipitie hapa..plse..
   
 4. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya matatizo wanayapuuzi tu hawa watawala, ila wanayajua sana. Kwenye red naona kama sentensi yako inapingana vile. Library ya kisasa inajumuisha jengo, vifaa na wafanyakazi weneye uelewa wa kisasa.
   
 5. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkandara amekalia kufanya siasa na kuacha kushughulikia mambo ya msingi kama haya,tunashukuru kwa taarifa mkuu
   
 6. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nilikuwa mwanafunzi wa UDSM mwaka 1989-1993.
  mengi unayosema ni kweli, chuo ni kikubwa sana, na kama kawaida ya watanzania, concept ya maintenance ni zero.

  Lakini hili la kubebana, this is purely your responsibility. Administration can prevent, but students and their organization, has a crucial roles to play on this.

  We should not e externalize all your problems to Prof. Mkandala.
   
 7. N

  NGENDA NGOLOMA Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana kamanda kwa kuthubutu na kusema yaliyo moyoni na hakika woga si nidhamu. Ujasiri ni uajibikaji na kujali taifa lako. Mamlaka husika ziwajibike kwa maboresho zaidi vingine ni uzembe wa kupindukia
   
 8. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hapa wanasubiria hadi lidondoke na liue waja kutoa rambirambi , mtu lazima apigwe bisu siku hiyo
   
 9. S

  SIPIYU30 JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 686
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Mimi nilikuwa mwanafunzi hapo UDSM 2002-2006, then masters 2007-2010, jamani panatisha usione. Sina hamu na chuo hicho. Afadhali ya secondari ya A level niliyosomea.
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Itabidi upeleke barua ya siri kwa mkandala, copy kwa chama chenu cha wanafunzi sijui ndio Daruso.

  Maswala ya kubebana uongozi kuyastopisha ngumu sana, imagine mtu anakuja kulala saa tano usiku sasa wao watafanya nini? Wapite wanagonga chumba hadi chumba?

  Maswala ya usafi nk na nyie mnachangia kwa aisee hebu anzeni wenyewe kuelimishana kuhusu usafi. Huwezi mtu kusimama mlangoni unalenga shimo...
   
 11. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Usafi wa UDSM ameondoka nao Prof .Luhanga na Estate Manager Dr.Rubaratuka nini.Nakumbuka enzi za 1992 hao hao wakina Prof Mukandala na baadhi ya Mangwini alikuwa nalalamika kuwa Luhanga kaaribu chuo.Sasa wamepewa chuo mambo ndo yamekuwa hivi.Pole sana mdau...
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni hatari aisee, nadhani haya ndio mambo ya kuyabebea kidedea kupitia chama chenu cha wanafunzi, maana ukute hiyo Hall na Kikwete amekaa humo humo na nyie mnakaa tena na msipokomaa na watoto wenu watakaa humo humo.
   
 13. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hili ni swala la room mates wenyewe. Kwani wanaobebwa si wanaalikwa? Kama kama mko 4 room mates, mmoja wenu akabeba mtu, waliobaki kwa nini wasikatae? Kwa nini wa report kwa dean of students?

  Hili ni lenu wneyewe wanafunzi, msimwonee Mkandala.
   
 14. Reserved

  Reserved Content Manager Staff Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 750
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili la kudondoka vipande vya matofali Hall 2 imeanza siku nyingi sana
  Toka nikiwa hapo nilikaa Hall 2 mwaka 2001-2002 na 2004 wakati namaliza na Hall 5 mwaka 2002-2003
  Sehem niliyokaa kwa amani ni Hostel za Kijitonyama 2000-2001 wakati naanza chuo
  Pale ndio tulikaa kwa amani bila bughudha za kuwaza maji wala kubebana wala kulala wanne chumba cha watu wawili
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nguvu zote ziko UDOM sasa hivi kwenye chuo kikuu cha CCM, hiyo UDSM hata JK alishasahau kama ina-exist
   
 16. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Sasa mnataka wanafunzi waishi wapi , mtaa kila mtu anajua gharama zake za upangishaji, ukitegemea boom utaumbuka
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,696
  Trophy Points: 280
  Undergraduates mtatimuliwa wote siku si nyingi! Pale wanataka postgraduates tu. Nyie undergraduate utoto umezidi. Utaendaje kunya kwenye choo kisicho na taa eti unalenga shimo kwa hisia? Watu wa Masters na PhD hawawezi kufanya ushetani kama huo
   
 18. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bibikuku,
  Ukumbuke kwamba hata UDSM ilianza kama UDOM. So kuna siku UDOM nayo itatelekezwa kama UDSM na wataanzisha Chuo kingine kwa mbwembwe hizo hizo kama za UDOM. Mtoa hoja kaongea mambo ya msingi sana. Sijui kama Mkandala huwa anapita humu. Kimsingi hata Mimi nilishawai kukaa Hall 2. Ni bweni lililochoka na kuchakaa. Halifai hata kuwa Mbavu za Mbwa!
   
 19. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Samahani jamani Kwani mwenyekiti wa UDSM ni nani? na kilipewa usajiri lini na tendwa? pia nataka kujua kama kinashiriki Arumeru.
  Asanteni
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  MKUU uko sawa. Basi hili msimlaumu Mkandala.
  Ni uswahili wetu wa kubebana.
  Everything has a cost.
   
Loading...