Professor Lipumba unatuharibu vijana wako

Kambaya ndo nani ndugu?
Yaani humjui Kambaya halafu unakuja na hoja ya kuzungumzia CUF Bara Le Profesa Lipumba? Kweli wewe bado kijana inatakiwa u jitahidi kufuatilia masuala ya siasa utajifunza zaidi.
Kwa taarifa yako.....unaposema Vijana watajifunza nini toka kwa Lipumba lazima uzingatie yafuatayo
- Usaliti ulikuwepo toka kipindi cha kale cha Mitume wa Mungu
- vijana wanatoboa masikio na kuvaa hereni huku wakivaa milegezo kuonyesha chupi boxer ya ndani
- Unazungumzia vijana gani bado sijakupata vizuri? ??
 
Bila utafiti huna haki ya kunena juu ya kadhia yoyote. Inaonekana ww ni mtu wa mihemko tu kufuata kundi kama kondoo bila kujua wapi kundi hilo linakwenda na kwa madhumuni gani. Profesa Lipumba anachofanya ni kuinusuru CUF isitumbukia kwenye mtego wa kumezwa na Chadema, wakati ambapo Seif Sharifu anaifunga CUF pingu za mikono na miguu na kuipeleka mikononi mwa Chadema kwa tamaa ya fedha na ahadi ya Chadema ya kuwa watamsaidia kuitoa Zanzibar kwenye Muungano (yaani kuvunja Muungano wa Tz ambapo ni kutenda UHAINI).

Kwa taarifa yako, vifuatavyo ni baadhi tu ya vituko vya Chadema dhidi ya CUF chini ya usimamizi wa Seif Sharifu:-

1. Kwenye Bunge la 2010 Chadema walikuwa wanaitukana CUF na viongozi wake kuwa eti ni CCM B kwa vile tu walikuome kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar.

2. Kwenye Bunge hilo Chadema waliwanyima CUF nafasi za Uwaziri vivuli kwa vile eti ni CCM B.

3. Chadema wavunja makubaliano yote ya UKAWA dhidi ya CUF kwa kusimamisha wagombea wa Chadema kwenye majimbo yote waliopangiwa CUF na hivyo kuzigawa kura za CUF kulikopelekea CUF kokosa viti vingi mno. Mifano hai ni majimbo yafuatayo - Segerea (Mtatiro wa CUF akashindwa), Mtama (CUF) ikashindwa, Tabora (Katuga wa CUF akashindwa), n.k. Mbaya zaidi viongozi wa CUF walipolalamikia kwa Prof Baregu wa Chadema juu ya hujuma hizo, jibu lake ni kuwa walikubaliana na Seif Sharifu kuwa kwa upande wa T/Bara CUF wasigombee jimbo hata moja, badala yake yote waachiwe Chadema.
3. Seif Sharifu alipokutana na uongozi wa CUF (2015) kabla ya uchaguzi, aliulizwa swali vp uongozi huo umnadi Lowasa wa Chadema? Ni manufaa gani kwa CUF yatapatikana? Seif aliuambia ungozi huo kuwa tayari yeye alishapokea shilingi bilioni 3 toka Ukawa na kwamba angewapatia kiasi cha shilingi milioni thalathini na mbili kila jimbo lililosimamisha wagombea wa ubunge na udiwani. Lakini wapi, waliambuli milioni 2.5 au 3 tu, tena kwa baadhi tu ya majimbo.

Ni dhahiri kuwa Seif akishirikiana na Chadema lengo lao ni kuifuta CUF huku Bara. Naomba Seif Sharif achukue udhu kisha alishwe yamini hadharani kama hujuma hizi hakuzifanya.

Swali hapa nani msaliti na mnafiki anaepokea rushwa kwa kazi ya kukiuua cha cha CUF? Ivo ni Lipumba au Seif Sharifu? Haya ni baadhi tu ya madhambi ya Seif Sharifu na kundi lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno meeengi kumbe Nonsense tuu umeandika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Professor kwa masikitiko makubwa sana umeharibu sana na unaendelea kuharibu vijana na kizazi kinachokuja kwa kuonyesha kwamba wapiganaji wa kweli na haki wanaweza kununuliwa .... Hivi unafundisha nini vijana wapenda haki wenye hari na siasa kwa ajili ya kukomboa wa Tanzania ... kwa chochote unachopata na umri uliona sasa jua yafuatayo:

- Unakatisha tamaa vijana wengi kwenye masuala ya Siasi, mapinduzi na kusimamia haki.
- Unaweka doa kwenye historia ya siasa ya vyama vingi Tanzania, haya mambo huishi milele.
- Ni legacy gani unaiacha kwa Taifa lako Mzee?
- Elimu yako imekusaidia nini?
- Unawafundisha nini waumini wa dini? hata hija umeenda, unakatisha tamaa.
- Unatufundisha kwamba maslahi ni kabla ya Imani zetu.

MIMI KAMA KIJANA NA MTANZANIA KWA KWELI NINASIKITIKA SANA MZEE KAMA WEWE, MSOMI, UNA IMANI YAKO, UMEHESHIMIKA KUNIDHIHIRISHIA KWAMBA SIASA NI MASLAHI.... BORA HATA MZEE WETU ALIYEENDA CANADA, SIO WEWE!

NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE KUTAMBUA KWAMBA FEDHA, NA KILA KITU VINAPITA, ILA HESHIMA, HAKI NA USAWA VITADUMU NA KUTUSAIDIA KWENYE MAISHA YAJAYO.
Kipi alichokifanya ambacho kinaonesha amenunuliwa na amevunja katiba ya cuf ukifananisha na Mbowe na Chadema na rafiki yake Sultani Seif

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani humjui Kambaya halafu unakuja na hoja ya kuzungumzia CUF Bara Le Profesa Lipumba? Kweli wewe bado kijana inatakiwa u jitahidi kufuatilia masuala ya siasa utajifunza zaidi.
Kwa taarifa yako.....unaposema Vijana watajifunza nini toka kwa Lipumba lazima uzingatie yafuatayo
- Usaliti ulikuwepo toka kipindi cha kale cha Mitume wa Mungu
- vijana wanatoboa masikio na kuvaa hereni huku wakivaa milegezo kuonyesha chupi boxer ya ndani
- Unazungumzia vijana gani bado sijakupata vizuri? ??

Nimeongelea tabia za Lipumba tu, mimi si mwana CUF wala CHADEMA, wala CCM ... Mimi ni Mtanzania. Pelekea Ujinga wako huko kwa wanaokulipa na kukutuma. Hayo ya vijana unayoayaongea unaonyesha JINSI GANI WEWE NI MPUMBAVU.....
 
Kipi alichokifanya ambacho kinaonesha amenunuliwa na amevunja katiba ya cuf ukifananisha na Mbowe na Chadema na rafiki yake Sultani Seif

Sent using Jamii Forums mobile app

MI NIMEMWONGELEA LIPUMBA IN RELATION TO VIJANA NA WATU WENYE NDOTO YA KUWA WANASIASA, NA WEWE UNARUHUSIWA KUONGEA KUHUSU CHADEMA NA MBOWE, SASA USITAKE MIMI NIMUONGELEE MBOWE WAKATI NAMUONGELEA LIPUMBA ... NA HATA CUF SIJAIONGELEA MIMI!!!!
 
Katika imani na mafundisho ya kidini tunaambiwa dhambi ya unafiki na usaliti ni mbaya kuliko dhambi ya kuua nafsi
Ataiuwa cuf lakini hatoweza kufuta kile ambacho wana cuf wamekiamini na kukisimamia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Professor kwa masikitiko makubwa sana umeharibu sana na unaendelea kuharibu vijana na kizazi kinachokuja kwa kuonyesha kwamba wapiganaji wa kweli na haki wanaweza kununuliwa .... Hivi unafundisha nini vijana wapenda haki wenye hari na siasa kwa ajili ya kukomboa wa Tanzania ... kwa chochote unachopata na umri uliona sasa jua yafuatayo:

- Unakatisha tamaa vijana wengi kwenye masuala ya Siasi, mapinduzi na kusimamia haki.
- Unaweka doa kwenye historia ya siasa ya vyama vingi Tanzania, haya mambo huishi milele.
- Ni legacy gani unaiacha kwa Taifa lako Mzee?
- Elimu yako imekusaidia nini?
- Unawafundisha nini waumini wa dini? hata hija umeenda, unakatisha tamaa.
- Unatufundisha kwamba maslahi ni kabla ya Imani zetu.

MIMI KAMA KIJANA NA MTANZANIA KWA KWELI NINASIKITIKA SANA MZEE KAMA WEWE, MSOMI, UNA IMANI YAKO, UMEHESHIMIKA KUNIDHIHIRISHIA KWAMBA SIASA NI MASLAHI.... BORA HATA MZEE WETU ALIYEENDA CANADA, SIO WEWE!

NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE KUTAMBUA KWAMBA FEDHA, NA KILA KITU VINAPITA, ILA HESHIMA, HAKI NA USAWA VITADUMU NA KUTUSAIDIA KWENYE MAISHA YAJAYO.
Soma katiba ya cuf ndio uandike hii ngonjera
 
Nilikuwa najiulizaga sanaa kama huyu ni prof tena wa uchumi kwanin huwa hawampi wizara husika?
Sasa ndio nimeelewa bhana kumbe watu walishamchungulia daah acha tu hata kina makonda watese tufanyaje sasa kama wazee wenyewe ovyoo
Angefundisha uchumi kwa kutumia quran na ilani ya CCM
 
Mi nimesema mtazamo wangu .... kama kuna wengine na wewe unaweza tushawishi .... maana mtu alijiuzulu kwa hiyari, anarudi kutafuta nini?
Usilamlaumu prof Lipumba anza kwanza kuwalaumu CUF ambao badala ya kuandaa kikao cha kujadili kujiuzulu kwake ndani ya muda ule wao walitekwa na siasa za kuutafuta urais mwaka 2015.

Profesa katumia udhaifu wa CUF wa kutoshughulika na maamuzi yake ndani ya wakati. Walaumu wanachama wa CUF. Jitahidi usimezwe na hisia pasipo kutanguliza kwanza msingi wa hoja wenye kueleweka, katika andiko lako.
 
Hivi Mwizi akim time mtu akamwibia, kwenye swala la kimaadili, utamlaumu aliyeibiwa au alitumia fursa kufanya uhalifu? wewe walaumu CUF kwa siredi yako ....
 
Mfano mbovu usiokuwa na mashiko. Narudia kukwambia uwalaumu CUF kwa kumezwa na trend ya kumfuata Lowassa wakati ule, wakaachia ombwe la maamuzi.

Unaongea kwa hisia, unalialia na kulalama, kitu ambacho hakikusaidii zaidi ya kukupunguzia hasira kutoka kifuani mwako.
 
Professor kwa masikitiko makubwa sana umeharibu sana na unaendelea kuharibu vijana na kizazi kinachokuja kwa kuonyesha kwamba wapiganaji wa kweli na haki wanaweza kununuliwa .... Hivi unafundisha nini vijana wapenda haki wenye hari na siasa kwa ajili ya kukomboa wa Tanzania ... kwa chochote unachopata na umri uliona sasa jua yafuatayo:

- Unakatisha tamaa vijana wengi kwenye masuala ya Siasi, mapinduzi na kusimamia haki.
- Unaweka doa kwenye historia ya siasa ya vyama vingi Tanzania, haya mambo huishi milele.
- Ni legacy gani unaiacha kwa Taifa lako Mzee?
- Elimu yako imekusaidia nini?
- Unawafundisha nini waumini wa dini? hata hija umeenda, unakatisha tamaa.
- Unatufundisha kwamba maslahi ni kabla ya Imani zetu.

MIMI KAMA KIJANA NA MTANZANIA KWA KWELI NINASIKITIKA SANA MZEE KAMA WEWE, MSOMI, UNA IMANI YAKO, UMEHESHIMIKA KUNIDHIHIRISHIA KWAMBA SIASA NI MASLAHI.... BORA HATA MZEE WETU ALIYEENDA CANADA, SIO WEWE!

NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE KUTAMBUA KWAMBA FEDHA, NA KILA KITU VINAPITA, ILA HESHIMA, HAKI NA USAWA VITADUMU NA KUTUSAIDIA KWENYE MAISHA YAJAYO.
Hayo ni majungu kama majungu mengine yalivo, Prof. yupo sahihi kulingana na katiba ya chama chenu, mlaumu makosa yaliyofanywa na Seif na si Lipimba wala Msajili, kwann msimshauri Seif alejee Buguruni? kama yupo sahihi nn kinamfanya asilejee Buguruni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipumba ni mmoja wa watu wa hovyo sana kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu,

na maadamu anakula na kusaza bila kuvitolea jasho,anaona sawa tu,mtamsema mtanyamaza,hata akifariki hajali legacy anaacha ipi,
yeye concern yake kubwa ni tumbo lijae,basi
 
Tena kajitoa ufahamu kama si msomi, amekuwa mdanganyifu kule zanzibar kila kunapokucha anawambia wafuasi wake mara mwezi huu nakabidhiwa uraisi mwezi ukiisha tena anaongeza miezi mitatu, swali linakuja kwa hao wanaolalamika na kama ni vijana huo ujinga anaoufanya zanzibar hawauoni? kwann waendelee kimlaumu Lipumba? kwann wasimlaumu Seif kwa upotoshaji anaoufanya huko Zanji na wakati huo ni msomi mzuri2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maprofesa huwa wanafanya sana research pengine anayoyafanya ni sehemu ya research yake pengine akimaliza research atatupa mrejesho
 
Nimeongelea tabia za Lipumba tu, mimi si mwana CUF wala CHADEMA, wala CCM ... Mimi ni Mtanzania. Pelekea Ujinga wako huko kwa wanaokulipa na kukutuma. Hayo ya vijana unayoayaongea unaonyesha JINSI GANI WEWE NI MPUMBAVU.....
Wewe si ndio umesema ni Kijana unayeharibiwa na Prof Lipumba? Yaani tabia ya Prof Lipumba inawaharibu nyie vijana? Twende taratibu usitokwe povu mapema!!!!!!
 
Professor kwa masikitiko makubwa sana umeharibu sana na unaendelea kuharibu vijana na kizazi kinachokuja kwa kuonyesha kwamba wapiganaji wa kweli na haki wanaweza kununuliwa .... Hivi unafundisha nini vijana wapenda haki wenye hari na siasa kwa ajili ya kukomboa wa Tanzania ... kwa chochote unachopata na umri uliona sasa jua yafuatayo:

- Unakatisha tamaa vijana wengi kwenye masuala ya Siasi, mapinduzi na kusimamia haki.
- Unaweka doa kwenye historia ya siasa ya vyama vingi Tanzania, haya mambo huishi milele.
- Ni legacy gani unaiacha kwa Taifa lako Mzee?
- Elimu yako imekusaidia nini?
- Unawafundisha nini waumini wa dini? hata hija umeenda, unakatisha tamaa.
- Unatufundisha kwamba maslahi ni kabla ya Imani zetu.

MIMI KAMA KIJANA NA MTANZANIA KWA KWELI NINASIKITIKA SANA MZEE KAMA WEWE, MSOMI, UNA IMANI YAKO, UMEHESHIMIKA KUNIDHIHIRISHIA KWAMBA SIASA NI MASLAHI.... BORA HATA MZEE WETU ALIYEENDA CANADA, SIO WEWE!

NAKUOMBEA MUNGU AKUSAIDIE KUTAMBUA KWAMBA FEDHA, NA KILA KITU VINAPITA, ILA HESHIMA, HAKI NA USAWA VITADUMU NA KUTUSAIDIA KWENYE MAISHA YAJAYO.
Mkuu Huyu Mzee ni Janga..Mimi naona haina sababu ya Kumjadili tena kajiaibisha sana.
 
Back
Top Bottom