Professor Lipumba amchimba mkwara Maalim Seif, atishia kumpiga marufuku kufanya siasa bara!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
1.jpg

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwenye mkutano wa ndani mkoani Geita.

Ziara ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza barua kwa viongozi wa CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa Lipumba huku akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.

“Kama Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku mimi nikimtambua kuwa Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara,” alisema Lipumba.

Profesa Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa Zanzibar wala kiongozi wa upinzani atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye amekuwa mstari wa mbele kutetea Wazanzibari.

“Mimi natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki na mwenye mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na lazima theluthi moja ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar, lakini mkutano huo haukufanyika wala muhtasari haupo,”alisema Profesa Lipumba.

Alieleza kwamba kwa sasa yeye na wana CUF wengine wamejipanga kukijenga chama hicho.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia suala la Muungano akisema ni muhimu kwa usalama wa nchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema ili kulinda Muungano kuna mahitaji muhimu ya kuwa na vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa pande hizo mbili.

Lipumba alisema amefika wilayani hapa akitoka Urambo kwenye msiba wa Spika wa Bunge la Tisa, marehemu Samuel Sitta ambapo pia aliongea na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

“Tumeifika Kahama kuzungumza na viongozi wa hapa na wa wilaya jirani, dunia ina changamoto kubwa katika masuala ya demokrasia na kujenga utawala bora kwa baadhi ya viongozi,”alisema Lipumba.
 
View attachment 435586

Lipumba siyo Mwenyekiti Alishajiudhulu.
 
Lipumba Safi sana Mtie Adabu huyo Mzee amezowea kujimilikisha Chama anashindwa kufata Sheria za nchi kwa matwaka yake binafsi ya kulilia madaraka

Kama vipi mzuwie tu asifanye mikutano bara na ingependeza ukampa siku kama hajakutambua basi huku bara asitie mguu kama noma na iwe noma tu
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom