Professor Kitila Mkumbo slams Ministers Ummy and Kigwangala

Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
 
Profesa Mkumbo atofautishe Ishu ya Utawala na Mambo ya Lab!

Kwa mfano ikigundulika kuwa Watanzania asilimia 95 wana HIV, hata kama ni kweli, Kiutawala hutakiwi Researcher kujitangazia tu, hiyo ni sensitive issue inayohitaji Serikali kujiandaa kubeba athari za tangazo kama hilo!
 
Ebu SOMENI hili andiko Mwana JF mmoja kaandika na Prof.asome pia.

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida nchi yetu hii kila kitu kinakuwa related na Siasa. Professionals can't do their work.
 
Profesa mkumbo aeleww
Hakuna aliyepingana na utafiti
Tatizo ni njia iliyotumika kufikisha taarifa kwa umma
Unasababisha public panic pasipo sababu za msingi
Pia Dr Mwele ilipaswa kupima madhara yanayoweza kusababishwa na habari za utafiti wake huo kwa nchi yetu
Kwa yeyote sio kila kitu hutangazwa hadharani
Ugonjwa wa Zika sio kitu cha kutangazwa na mkurugenzi wa NIMR
huo ni taaruki ya dunia
Am sure imesababisha damage kubwa sana katika sekta ya utalii
Na hii inaweza tumiwa na maadui wa nchi yetu
Uzalendo ni muhimu
 
Hivi Dr.Mwele alikuwa anatangaza kuwa ZIKA ipo au alikuwa anatoa taarifa ya matokeo ya utafiti kuhusu ugonjwa wa ZIKA!!? Hivi matokeo ya utafiti mnataka akayatangaze Ummy Mwalimu!!?

Hayo mambo mengine ya kutangaza rasmi hao wanasiasa yangefuata baadae lkn kwanza taarifa ya kutalaamu lazima iwekwe public na watalaamu wenyewe na ndicho kilichofanyika...!!

Hivi kwa kutangaza ummy mwalimu kuwa ugonjwa wa ZIKA haupo ndo hautakuwepo kweli!? Yaani watalii ni muhimu kuliko sisi??
 
Waswahili WAWILI wizarani
 
Prof.anaongea ukweli lakini kuna ukweli nadhani ambao ambao Prof.haujui vyema. Hasa katika Mamlaka ya Mkurugenzi wa Utafiti zilizopo chini ya serikali. Nadhani kuna utaratibu wake wa kutanganza ugonjwa wowote ukigundulika hasa kwa kuwasiliana na mamlaka husika ndipo waone namna gani ya kuuambia umma.
Nadhani upeo wako ni mdogo sana katika suala hili.
Ngoja nikupe ufafanuzi.

1/NIMR ndio chombo rasmi cha serikali katika kusimamia tafiti zote za Afya hapa Tanzania. Kipo chini ya wizara ya Afya Makao makuu, na kinajukumu la kuanzisha, kuendesha na kuhitimisha mwenendo wowote wa tafiti zote za Afya hapa Tanzania.

2/Ni kosa kubwa sana kwa taasisi yoyote kufanya tafiti za kisayansi na mwisho wa siku kutokutoa matokeo ya tafiti hizo au kuchelewesha kwa makusudi matokeo ya tafiti hizo au kupotosha kwa makusudi matokeo ya Tafiti hizo (Kitaalamu inaitwa Research Misconduct, na moja ya adhabu yake kimataifa ni kuzuia kabisa kwa taasisi husika kufanya utafiti tena).

3/Utafiti wa kisayansi ni mali ya jamii iliyohusika katika utafiti huo. Utafiti sio mali ya mtu au serikali. Sio jukumu la serikali au mtu binafsi kuamua kutoa au kutokutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi uliokwisha kufanyika. Kuzuia au kuchelewesha kutoa matokeo ya utafiti wa kisayansi ni sawa na kuiba haki ya jamii.

4/Kuna tofauti kubwa sana kati ya Kutangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika(Research Findings) na kutangaza mlipuko wa ugonjwa kwenye jamii(Epidemic).
Mkurugenzi wa NIMR alitangaza matokeo ya utafiti uliokwisha kufanyika na wala hakutangaza mlipuko wa Zika hapa Tanzania.
 
Profesa mkumbo aeleww
Hakuna aliyepingana na utafiti
Tatizo ni njia iliyotumika kufikisha taarifa kwa umma
Unasababisha public panic pasipo sababu za msingi
Pia Dr Mwele ilipaswa kupima madhara yanayoweza kusababishwa na habari za utafiti wake huo kwa nchi yetu
Kwa yeyote sio kila kitu hutangazwa hadharani
Ugonjwa wa Zika sio kitu cha kutangazwa na mkurugenzi wa NIMR
huo ni taaruki ya dunia
Am sure imesababisha damage kubwa sana katika sekta ya utalii
Na hii inaweza tumiwa na maadui wa nchi yetu
Uzalendo ni muhimu

Hiki walichokifanya serikali sasa ndio kinasababisha chaos. Serikali ilitakiwa ieleze kwa raia tofauti ya kugundulika kwa virusi na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Zika.
 
Dr Mwele is very clever na I do support kitendo alichokifanya ingawa madhara yake yamemuondoa kikatili kabisa kwenye ajira.

Kila mtu anafahamu mfumo mbovu wa nchi yetu wa kuto disclose crucial matters na muda mwingine huwa findings nyingine zinafichwa kabisa mwisho wa siku mambo yanabumbuluka inakuwa aibu kwa serikali.

Huwezi kuingiza politics kwenye issue sensitive kama za afya ya binadamu.

Mtafiti ndio anaetoa report ya utafiti wake.

Big up Dr Mwele.. U are and will always be the HERO na utabaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi ambao huwa hawapewi taarifa za tafiti kama hizi na serikali yao.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom