Professionalism ya Askari Polisi wa Tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,498
19,338
attachment.php

attachment.php

attachment.php

Ninapoangalia picha hizo, ninajiuliza kama kweli askari polisi wa Tanzania wanaijua profession ya upolisi sawasawa. Naona kama wengi wanajua kuwa jukumu la upolisi ni kutumia mabavu mahali popote.
 
Attachments

  • 1232369221_chuo_2.jpg
    1232369221_chuo_2.jpg
    8 KB · Views: 127
  • 1232369221_chuo.jpg
    1232369221_chuo.jpg
    10.3 KB · Views: 133
  • 1232369221_chuo_1.jpg
    1232369221_chuo_1.jpg
    10.2 KB · Views: 129
Ninapoangalia picha hizo, ninajiuliza kama kweli askari polisi wa Tanzania wanaijua profession ya upolisi sawasawa. Naona kama wengi wanajua kuwa jukumu la upolisi ni kutumia mabavu mahali popote.

Bila shaka wewe either umewahi kusoma CCP au umewahi kupata masimulizi juu ya professionalism ya upolisi inavyotakiwa kuwa. Ni vizuri ukatuwekea hapa ili tujue walichokosea na sisi tujue mipaka ya kazi zao, ikibidi kudai fidia kama wataivuka. Nasubiri maelezo yako ili tuendelee kujadili, wengine hapa kama mimi hatujui huwa wanafundishwa nini huko CCP !!
 
Huyu POLISI inabidi kutunza hii picha ili siku moja na wao waadhibiwe kwa kunyanyasa vijana wasio na hatia. Au alitakiwa kumtia pingu kama alikuwa anaona jamaa anasumbua na au kumtanguliza mbele na kumfuata. Sasa hii ya kumtia mtu JEKI, tena jamaa kakuzidi mwili na urefu, na kuacha mikono yake iwe huru, akikutia KIPEPSI? aka kubwa kubwa kuliki??
Hivi hii nayo inahitaji hadi uende chuo cha polisi Moshi?

Kumbe YO-YO ni mchina? Naona anapiga mziki kwenye kuapishwa kwa Obama!!!!!
 
Bila shaka wewe either umewahi kusoma CCP au umewahi kupata masimulizi juu ya professionalism ya upolisi inavyotakiwa kuwa. Ni vizuri ukatuwekea hapa ili tujue walichokosea na sisi tujue mipaka ya kazi zao, ikibidi kudai fidia kama wataivuka. Nasubiri maelezo yako ili tuendelee kujadili, wengine hapa kama mimi hatujui huwa wanafundishwa nini huko CCP !!
Sijakuelewa swali lako sawasawa, je ni kwa sababu unadhani poilisi huyo yuko sahihi au ni kwa sababu unajua kuwa mimi siyo polisi kwa hiyo sijui professional responsibilities za polisi.

Hata kama kijana yule kafanya fujo na kutishia amani, kilichotakiwa kufanywa na polisi professionally ni kumfunga pingu na kumpeleka mahabusi kwa masaa kadhaa kabla ya ama kumwachia huru au kumfungulia mashtaka. Kumbuka kuwa pamoja na yaliyotokea, bado yule kijana hana hatia hadi pale mahakama itakapoamua hivyo; kwa hiyo ana haki ya kuheshimiwa bila kunyanyaswa na mtu yeyote including polisi. Polisi amepewa zana za kumdhibiti mtu anayeleta fujo, kubwa ikiwa ni pingu. Deadly force inaweza kutumika endapo itaonekana kuwa mtuhumiwa pia anatumia deadly force.

Kwa jinsi alivyomkwida vile, kama kijana huyo ni mhalifu kweli anaweza kumgeuka na kunyang'anya silaha zake za kipolisi na kuzitumia dhidi yake. Na kama hana silaha, bado kijhana huyo anaweza kuwa na nguvu kumzidi yeye polisi na hivyo akaweza kumpiga na kumwumiza. Hapo ndipo swala la profesionalism linapokuja.
 
Nimekumbuka post hii niliyoweka hapa muda mrefu kidogo ulioputa. bado najiuliza, je polisi wetu kweli wanajua kazi yao ya upolisi? Wamekuwa wanatumika kama wapigana vita dhidi ya raia badala ya kuwalinda raia na mali zao. Raia wakiwa na mgomo au maandamano tu, basi polisi wanakwenda pale kama wanaingia vitani, na kuanza kuwanyanyasa ikiwa ni pamoja na kuwaumiza hata kuwaua raia wasiokuwa na hatia yoyote.

Miezi hii mitatu iliyopita tumejionea polisi wetu wakitumia nguvu nyingi sana dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, je hawajajifunza kutoka kwa wenzao wa Misri jinsi walivyokuwa wakilinda waandamanaji siku zote hizi?
 
hawa majamaa yani yana elimu ya std 4 then anampiga tanganyika jeki msomi hajui kuwa kesho na kesho kutwa atakuwa bosi wake au ?
 
kweli kabisa atuwekee hayo mambo muhimu katika kazi zao.
Pili hivi anapokuja kukukamata huo muda wa kumuuliza kosa lako nini utakuepo?
Je ukienda mahabusu na ukafunguliwa charge yyingine utajiteteaje?
Tuelimisheni wajuzi.
 
Tunachosahau hapa ni kuwa polisi 'ni mtu' or 'is person' like you. Nachelea kuongea mengi maana sijui ufahamu wa mwanzisha mada kuhusu taaluma ya upolisi. Kama person yeyote polisi anaweza kufanya makosa akiwa kazini kama vile ambavyo mwalimu anaweza kutembea na mwanafunzi wake, mhasibu anweza kukwapua fedha za mwajiri wake, daktari akasahau mkasi tumboni mwa mgonjwa n.k n.k. Tusilete ushabiki ktk vyombo vya dola ambavyo cdm ikishinda itahitaji kuvitumia. SIJAONA PROFESSIONAL MISCONDUCT YO YOTE KTK HIZO PICHA
 
Du!
 
Back
Top Bottom