Professional certification boards za Tanzania haziko kwa ajili wa kuwasaidia wahitimu bali kuwakomoa.

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,383
17,406
Elimu ya Tanzania ina matatizo mengi sana kuanzia msingi hadi kwenye taasisi za kudhibiti ubora wa taaluma au professional bodies kama ERB, NBAA, PSPTB, nk haziko kwa ajili ya kuwasaidia wahitimu wa fani hizo bali kuwakomoa.

Naanza na NBAA, hii ndio bure kabisa, imekaa katika mfumo wa kumtaka kila mhasibu aajiriwe ndio aweze ku- practice taaluma ya uhasibu. Yaani ukiwa na cpa na huna ajira huna tofauti na mtu aliemaliza darasa la saba maana huwezi kuitumia cpa yako popote pale nchi hii isipokua uwe umeajiriwa, huwezi kufanya chochote hadi uwe kwenye ajira. Kwa sababu ukipata tu cpa bado itakulazimu uhuzurie masomo yao ya semina ambazo kwa mwaka unatakiwa kuhuzuria si chini ya 2 na ada kwa kila semina si chini ya laki 4 kwa miaka kadhaa ndio uruhusiwe ku-practise uhasibu nje ya ajira, it is hilarious, huna kazi na hu-practise popote hiyo hela ya wewe kulipa semina zao kwa miaka kadhaa ili uruhusiwe ku-practice uhasibu unaitoa wapi?

Huwezi kua na cpa leo ukasema ngoja nianzishe auditing firm yangu au accountancy firm yangu, huruhusiwi. Unabaki unashangaa, kama mitihani ya board ni ku-harmonize profession, mtu kafaulu iweje tena awekewe vikwazo vya kujiajiri na taaluma yake. Mbona wanasheria wakimaliza tu law school wanaruhusiwa kujiajiri na taaluma yao, wahandisi hivyo hivyo, shida iko wapi kwa wahasibu? Yaani baada ya kuhakikiwa kama mhasibu uliekomaa na bodi bado tena huaminiki hadi uhuzurie/ufanye kazi miaka kadhaa ndio uruhusiwe kufanya kazi ya taaluma yako, hii ni akili kweli? Madaktari wakimaliza internship wanaruhusiwa kufanya public practise ila sio wahasibu.

Vijana wengi wako mtaani wana cpa wanauza mahindi ya kuchoma, yaani wamejiajiri kwenye fani isiyo ya taaluma yao huku wana vyeti vya ubora vya taaluma yao. Hii ni ajabu ya Dunia.

Bodi nyingine za taaluma haziko kwa ajili ya kuwasaidia wasomi bali kuwakomoa.
 
Back
Top Bottom