PROFESA WA UD: Safari hii TUNAGOMA kweli kweli

jamani hebu naomba tuongelee hili jambo kwa ujumla kwa taarifa nilizo nazo wafanyakazi wote si wa serikali kuu, halmashauri hawajapata mishahara ni kweli au uuongo? tunaomba mtujuze maana familia zetu zita angamia sasa tutafute maarifa mengine
 
'Kama mshahara wa mwezi huu utakuwa ule ule ambao hauna nyongeza ya mshahara,tunagoma. Hebu angalia,wenzetu wote wameshapata mishahara yao tena yenye nyongeza tangu Mwezi wa saba kwanini sisi bado? Hadi leo tarehe 3/10/2012 hatujapata mishahara. Tunafanyaje kazi? Nadhani tunataniana hapa.Safari hii tunagoma kweli kweli. Ngoja uone'

Ni maneno ya ukali na ya kutia huruma ya Profesa mmojawapo wa UDSM ambaye alinipigia simu leo 'kuniazima' hela ili auanze mwezi huu. Nimemuonea huruma yeye,Wahadhiri wengine na wafanyakazi wa UDSM kwa ujumla. Mkuu wa Kaya yuko nje anakula maisha. Kwanini lakini mambo haya?

Hapo kwenye red, nahisi mishahara ilienda kugharamia chaguzi za CCM. Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
 
jamani hebu naomba tuongelee hili jambo kwa ujumla kwa taarifa nilizo nazo wafanyakazi wote si wa serikali kuu, halmashauri hawajapata mishahara ni kweli au uuongo? tunaomba mtujuze maana familia zetu zita angamia sasa tutafute maarifa mengine

Hbr ni ya kweli, we tafuta tu maarifa mengine kabla familia haijaangamia.
 
Kuna watu kila kukicha wanaota migomo. Huyu aliyeandika kuwa maprofessa safari hii udsm watagome kwa sababu ya mshahara sidhani kama anakifahamu vizuri chuo kikuu cha dar-es-salaam. Kugomea nini na wanamgomea nani?? Hii migomo sasa hivi ni unpopular, imeshindikana kwani haijengi bali kuwaharibia watu maisha binafsi bila kubadilisha kitu. Chuo kikuu kina utaratibu mzuri wa kufuatilia matatizo yao na si migomo. Kwanza maprofessa wengi wapo kwenye mikataba na walikwisha ku staafu.
 
Kama mishahara iinachelewa kima mwezi inatoka tarehe 5 basi ukijumlisha hakuna ucheleweshaji ni kwamba kila baada ya siku 30 unapata mshahara. Algebric ratther than politics
 
Wasomi wetu wamekuwa wasaliti mfano Bana ndo maana mambo haya yanatokea
mkuu na ile kamati ya bunge iliyopita juzi na kuondoka na maafisa wa duce na mkwawa kwa malipo hewa ninasikia iliyaona hayo madudu lakini cha kushangaza ud hakuna aliyeguswa km vyuo vingine!..
 
Back
Top Bottom