Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Kufaa au kutofaa kwa mradi kunaongozwa na feasibility study ya mradi husika. Na utekelezaji wake wa mradi unaofaa hakutegemei Professor kasema/katoa ushauri gani.
 
Mradi wa kuhamia Dodoma unaweza kusitishwa kwa muda wa miaka 10 mingine ikamilike kwanza, majengo hayaharibiki.
 
Pia kuhamia Dodoma kusitishwe kwa muda
Nadhani wangeacha ununuzi wa ndege. Kwenye usafiri wa anga wavutie wawekezaji kama fastjet warudi.

Pesa hiyo inayopelekwa kununulia ndege zinazoliingizia Taifa hasara kila mwaka, zote zipelekwe kwenye reli.

Kiuhalisia na kwa faida za kiuchumi, ujenzi wa reli, barabara na madaraja ilikuwa sahihi. Vingine vingefuata taratibu.
 
LNG ni pesa za wawekezaji.
Anachokisema huyo Prof ni sawa, lakini sasa mbona aliyeingia nae ni kama amekuja na miradi yake itakyotumia pesa mingi LNG kwa mfano, licha ya kwamba tayari wanatuambia lile bwawa la Nyerere wameanza kulijaza maji?

Naona kinachotuponza sisi ni siasa, kila kiongozi anayekuja anataka akiondoka aache alama yake, matokeo yake hapo wajanja ndio wanafunguliwa milango ya upigaji, haya mambo yakwenda bila vipaumbele yatatuumiza kwa muda mrefu sana ujao.
 
Hata siku moja wazungu Hawata kubali kuona nchi za Africa zina piga hatua kujikwamua kutoka kwenye Utegemezi.

Wao wanataka muwe watumwa wao ili waje wawekeze wao na kuwanyonya.

Ni MTU mjingatu Atamshabikia huyu beberu bila kutafakari kwamba ndani ya miaka 50 ijayo kama hamja jipanga kwenye miundo mbinu basi idadi ya watu itapata taabu sana maana watu wanongezeka na wanataka huduma.
Idadi ya watu inatakiwa idhibitiwe pia, kasi ya ukuaji wetu wa uchumi sio nzuri kiasi cha kuendelea kuongeza watu wengine wengi kwa kasi zaidi.
 
Mwamba kama mwamba popote alipo apumzike kwa amani na furaha.
Mwamba kama mwamba leo watu wanamtusi na kumtukana ila ni wachache ila majority wanamkubali sana na mm binafsi namkubali na nitaendelea kumkubali ukiachilia mbali yale mapungufu ya kibinadamu ambayo hata mimi ninayo.

Watu wa siasa daima hawaaminiko na wanaweza kutengeneza habari ili ionekane flan ni mbaya kwa maslahi yao binafsi.

Huyo kiumbe wa oxfod nadhan yafaa amwache mama aendeleze miradi iliyokwisha anzishwa baada ya hapo ndipo aje miradi mingine mipya

Nchi inapaswa kuwa na sera za kitaifa ili raisi yoyote atakayeingia madarakani asiwe na yake ila aende na sera za taifa. Mfano kipaumbele cha nchi ni nini? Kama ni kilimo basi anaekuja anachezea humo humo si mara mapinduzi ya kijani. Mara mapinduzinya viwanda dah yan tabu tupu.
 
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

View attachment 2497178
Ni vizuri mtu akitoa maoni, kama una uwezo, chambua. Usilete profesa fulani kasema hivi, sasa unataka tukubali ya huyo profesa pumbav? Tumepata Uhuru miaka mingi, nchi gani Afrika imesaidiwa na wazurngu ikaendelea? Ipi hiyo?

Ukiendelea kutukuza watu wa aina hii hufiki kokote! Ni mtu mpuuzi tu! Yaani tusiwe na umeme? Walimshauri Mkapa akavuruga NBC eti ni kubwa sana, Nyerere alimuuliza Mkapa kwamba benki zao ni ndogo? Sasa wanaleta ujinga mwingine tena eti miradi ni mikubwa, Mikubwa pumbav!
 
Idadi ya watu inatakiwa idhibitiwe pia, kasi ya ukuaji wetu wa uchumi sio nzuri kiasi cha kuendelea kuongeza watu wengine wengi kwa kasi zaidi.
Unasimulia kama risala la CCM. unawezaje kudhibiti idadi ya watu ktk umaskini? Taja mbinu moja tu!
 
hawa mashoga wameona tunaelekea sehemu nzuri, wameanza kutukatisha tamaa. walikuwa wapi awali? kama reli ya sgr sehemu zote inaenda vizuri, bwawa la nyerere liko vizuri. ni hayo tu, mradi gani mwingine mkubwa ambao huyu mzungu anaongelea anaotaka tuusimamishe? shetani huyu. Tangu lini taifa la magharibi likaishauri nchi yeyote ya afrika kwenye njia iliyo sahihi ili taifa hilo la africa lifikie sehemu lijitegemee? wanatamani tuwe na shida siku zote.

SGR itaharakisha sana maendeleo kwasababu ya usafirishaji, bwawa la nyerere litaongeza kiwango cha umeme kwa ajili ya SGR na viwanda, na mengine mengi. sasa ana nini cha kutushauri huyu?
 
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

View attachment 2497178
CCM kukaa madarakani kwa muda mrefu sana wamefikia hatua ya kuteletea mwendawazimu awe rais, matokeo yake tunayaona
 
Hii miradi ilikuwa na ten pasenti za Jiwe, Bashiru, Polepole, Dotto James, Kijazi na Mfugale na Kalemani.

Tunamuomba mama aiondoe kampuni ya ndege ikulu, ikaguliwe. Uwanja wa ndege Mwanza ni godown, lakini inasemekana ni la bilioni 9.

Masoko yote yachunguzwe, stendi zote, unaambiwa stendi ya JPM mbezi bilioni karibu sabini, hiyo fedha inajenga stendi tatu kama hizo.

Ndio maana Hilo kundi lilikuwa linaipigia kelele miradi hiyo, sio kwamba waliipenda nchi, hapana, walikuwa na vikampuni vyao vina subcontract.

Naona aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa dodoma baadae akahamishiwa njombe ndugu Mtaka alikuwa anajilia tenda za kuuzia serikali matofali kwa kupitia kampuni ya mkwewe wa GRONECY HOTEL, Morogoro,
Safi sana!

Ukipata nafasi nchi hii alafu usile wewe ni mpumbavu!

Nawapongeza wote waliotumia fursa vizuri
 
Back
Top Bottom