Profesa wa Chuo Kikuu Oxford amshauri Rais Samia kuhusu miradi aliyoianzisha Hayati Magufuli kwa pupa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,814
18,808
Profesa wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford amemshauri serikali ya Samia kuwa na uangalifu kuhusiana na kutekeleza miradi mikubwa aliyoianzisha Magufuli kwa pupa kwa kuwa inaweza kuliingiza taifa kwenye madeni makubwa yatakayoathiri uchumi wake

Magufuli alipoingia madarakani alianzisha miradi mingi kwa fujo kama vile kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege kwa fujo, ujenzi wa SGR, ujenzi wa bwawa la Nyerere huku akihadaa wananchi wasio na uelewa kuwa miradi hiyo yote inatekelezwa kwa fedha za ndani

Hadi sasa deni la taifa linakribia kufikia trilioni 100 kutokana na miradi hiyo kutumia fedha nyingi, na hakuna uhakika itakamilika lini

FB_IMG_1674813365797.jpg
 
Wasimchanganye. Wanataka kumtoa kwenye reli maana wanajua ni wale wa kujipendekeza kwa wazungu.
Miradi wala sio ya magafuli ila ni ilani za chama cha mapinduzi. Mama ashikilie tu usukani hakuna mradi wowote utakua wa hasara. Wao wanapofikiria hasara wanafikiria muwekezaji binafsi lakini miradi yetu ni ya umma. Haijaanzishwa kiwazimu. Faida zake mingi ni ya kuonekana muda mfupi na mingi muda mrefu.
 
Hii miradi ilikuwa na ten pasenti za Jiwe, Bashiru, Polepole, Dotto James, Kijazi na Mfugale na Kalemani.

Tunamuomba mama aiondoe kampuni ya ndege ikulu, ikaguliwe. Uwanja wa ndege Mwanza ni godown, lakini inasemekana ni la bilioni 9.

Masoko yote yachunguzwe, stendi zote, unaambiwa stendi ya JPM mbezi bilioni karibu sabini, hiyo fedha inajenga stendi tatu kama hizo.

Ndio maana Hilo kundi lilikuwa linaipigia kelele miradi hiyo, sio kwamba waliipenda nchi, hapana, walikuwa na vikampuni vyao vina subcontract.

Naona aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa dodoma baadae akahamishiwa njombe ndugu Mtaka alikuwa anajilia tenda za kuuzia serikali matofali kwa kupitia kampuni ya mkwewe wa GRONECY HOTEL, Morogoro,
 
Hii miradi ilikuwa na ten pasenti za Jiwe, Bashiru, Polepole, Dotto James, Kijazi na Mfugale na Kalemani.

Ndio maana Hilo kundi lilikuwa linaipigia kelele miradi hiyo, sio kwamba waliipenda nchi, hapana, walikuwa na vikampuni vyao vina subcontract.

Naona aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa dodoma baadae akahamishiwa njombe ndugu Mtaka alikuwa anajilia tenda za kuuzia serikali matofali kwa kupitia kampuni ya mkwewe wa GRONECY HOTEL, Morogoro,
Hivi vyeti feki si mmelipwa au wewe hujalipwa mkuu?
 
Ili umuelewe raisi aliepita inabidi ipite miaka kadhaa ndio utamuelewa.Nakumbuka alipotoka hayati mwl.Nyerere watu tuliona kama katuingiza chaka, lakini baadaye tukamuona kumbe alikuwa sahihi sana.Sasa hii ndivyo itakavyotokea kwa Magufuli na hata Samia,baada ya miaka kadhaa kuondoka ndio utajua kuwa walikuwa na akili za ziada...
Mambo ya JPM yalikuwa ya hovyohovyo, kwa mara ya kwanza mkuu wa Mkoa anagombania ghorofa la mabilioni Masaki. Mshahara wa mkuu wa Mkoa hauzidi milioni tano.
 
Huyo Proffesor wa Oxford kwa nini asimshauri waziri mkuu wa Uingereza Rish Sunak jinsi ya kurekebisha uchumi unaoyumba kwa sasa!

Kutokana na mradi mkubwa wa upanuzi wa mfumo wa treni za mwedokasi nchini kwake Uingereza!

Sio kila msomi ni muelewa wa mambo anayoshairi.kina Dk Musukuma wapo hata Ulaya!

Huyu amewekwa hapo,kuna Kitu tunaenda kupigwa na Msoga Team verry Soon!

Mark my words!
 
Hivi vyeti feki si mmelipwa au wewe hujalipwa mkuu?
Tumelipwa mkuu, hapa tuko tunatest mitambo ya weekend, one two za baridi, Jiwe aliyetufanyia mtima nyongo, anasikilizia joto la ardhi linavyomnyoosha saa saba hii ya mchana akiwa amekenua huko alikolala
 
kwenye bwawa la Nyerere tayari inajulikana litaanza kazi lini,na lishaanza kujazwa maji.ila sgr ndo mziki upo hapo sasa.
Nadhani wangeacha ununuzi wa ndege. Kwenye usafiri wa anga wavutie wawekezaji kama fastjet warudi.

Pesa hiyo inayopelekwa kununulia ndege zinazoliingizia Taifa hasara kila mwaka, zote zipelekwe kwenye reli.

Kiuhalisia na kwa faida za kiuchumi, ujenzi wa reli, barabara na madaraja ilikuwa sahihi. Vingine vingefuata taratibu.
 
Nadhani wangeacha ununuzi wa ndege. Kwenye usafiri wa anga wavutie wawekezaji kama fastjet warudi.

Pesa hiyo inayopelekwa kununulia ndege zinazoliingizia Taifa hasara kila mwaka, zote zipelekwe kwenye reli.

Kiuhalisia na kwa faida za kiuchumi, ujenzi wa reli, barabara na madaraja ilikuwa sahihi. Vingine vingefuata taratibu.
ushauri makini kabisa huu.👆
 
Kama hakuacha amani ambayo ingemsindikiza huko aliko kwa amani, atapumzikaje kwa amani? Yaani kama kaburi lake lina masikio, kwa aliyoyafanya, kelele hizi zitamnyima amani

Na bahati baya hawezi kuamka kuomba radhi na kutubu.
Labda akatubu Kwa sabaya na makonda.sio Mungu wa Isaka na Yakobo
 
Nyerere aliwahi kutuambia ukiona beberu anakusifia sana jiulize umekosea wapi. Pia magufuli aliwahi kunukuliwa kwamba ukiona beberu anakukosoa basi jua umemtandika penye mshono. Sasa huto samaiah achague mwenyewe, kusifiwa au kukosolewa na beberu.
 
Anachokisema huyo Prof ni sawa, lakini sasa mbona aliyeingia nae ni kama amekuja na miradi yake itakyotumia pesa mingi LNG kwa mfano, licha ya kwamba tayari wanatuambia lile bwawa la Nyerere wameanza kulijaza maji?

Naona kinachotuponza sisi ni siasa, kila kiongozi anayekuja anataka akiondoka aache alama yake, matokeo yake hapo wajanja ndio wanafunguliwa milango ya upigaji, haya mambo yakwenda bila vipaumbele yatatuumiza kwa muda mrefu sana ujao.
 
Back
Top Bottom