Mbunge wa Muleba Mjini Mama Anna Tibaijuka akizungumza na kituo kimoja cha habari leo kuhusu ahadi ya Rais Magufuli kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi amesema kuwa ni jambo zuri na litahakikisha kuwa haki inapatikana.
Mama Anna amesema kuwa ukishaanzisha mahakama utakuwa unatafuta haki na ukweli kwani yeye mwenyewe ni muhanga kwa kashafa za ufisadi kwani amekuwa akituhumiwa kwa kitu ambacho hata hajakifanya. Pia Mama Anna aliwalaumu Watanzania kuwa ni wepesi wa kuhukumu kiasi kwamba kwao mtuhumiwa wanamfanya anaonekana tayari ana hatia.
Aidha amesema kuwa anamshukuru Rais Magufuli kwa hilo kwani kumekuwa na magenge ya mafisadi nchini ambayo wao hawakamatwi ila wakiona hali ni mbaya basi wanatafuta mtu wa kumtoa kafara. Amesema anatamani kuona majipu yakiwa majipu kweli na sio tukamue nyama.
Akizungumzia sakata la Escrow amesema kuwa zile zilikuwa ni tuhuma, na kama kweli fedha ziliibiwa basi wahusika watamke hadharani kama kweli ziliibiwa na watazirejesha. Tibaijuka amesema kuwa katika nchi ya wadanganyifu, wale waaminifu ndio wanaoteseka.
Mtu anayesimama katika misngi ya ukweli ndiye anaweza kuzungumzia maadili na si vinginevyo. Mimi si wakwanza wala wamwisho kutuhumiwa ila naamini mahakama hii ikija watu wataanza kuzisoma namba baada ya ukweli kujulikana.
Mama Tibaijuka amesema kuwa yeye anamuombea Rais Magufuli kila kisu kwani anaamini kazi anayopambana nayo ni kubwa.