Profesa Sospiter Muhongo

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Mmoja wa mawaziri wataalam waliobobea kwenye masuala ya nishati na gas. Wakati anateuliwa na Raisi nilifurahi sana kwani alianza kutoa ahadi za wananchi kufungiwa umeme kwa muda wa mwezi mmoja kama umelipa. Nilijitahidi sana kutafuta hela ili nikaunganishiwe kwenye kibanda changu kilichoko eneo la usariver maeneo ya ngaresero nilijitahidi kukamilisha taratibu zote.

Hatimae zilikamilika januari 2013 chakushangaza mpaka leo hakuna kitu! Wananchi wa eneo lile tulijitahidi ili tujiunge wa 3 ili tupatiwe nguzo 1 tu ili iweze kutufikia wote lakini wapi! Kila ukienda ofisi ya Tanesko iliyoko maeneo ya usariver majibu ni kwamba subirini mpaka tumalize vijijini! Hivi hii ni haki kweli? Tangu january mpaka leo! Huu si ungwana hata kidogo.

SAME TIMES TUNAWASHUTUMU MAWAZIRI KUMBE HUKU CHINI WATENDAJI NI BOOM..

Waziri ebu fanya kazi
 
Changanya na zako,kusema mbali na kutenda mbali,maneno au maandishi sio vitendo,mimi ni mfuasi wa matokeo sio matukio
 
Mmoja wa mawaziri wataalam waliobobea kwenye masuala ya nishati na gas,
Wakati anateuliwa na Raisi nilifurahi sana kwani alianza kutoa ahadi za wananchi kufungiwa umeme kwa muda wa mwezi mmoja kama umelipa.
Nilijitahidi sana kutafuta hela ili nikaunganishiwe kwenye kibanda changu kilichoko eneo la usariver maeneo ya ngaresero nilijitahidi kukamilisha taratibu zote.
Hatimae zilikamilika januari 2013 chakushangaza mpaka leo hakuna kitu!
Wananchi wa eneo lile tulijitahidi ili tujiunge wa 3 ili tupatiwe nguzo 1 tu ili iweze kutufikia wote lakini wapi!
Kila ukienda ofisi ya Tanesko iliyoko maeneo ya usariver majibu ni kwamba subirini mpaka tumalize vijijini! Hivi hii ni haki kweli? Tangu january mpaka leo! Huu si ungwana hata kidogo.
SAME TIMES TUNAWASHUTUMU MAWAZIRI KUMBE HUKU CHINI WATENDAJI NI BOOM..
Waziri ebu fanya kazi
usimlaumu sana ni mfumo mbovu wa utendaji amesema Dr.Slaa ataumweke malaika ndani ya mfumo wa ccm tulionao hivi hatowez kufanya kazi. huyu mzee aliingia kwa kasi akaunda tume ya kuchunguza mikataba mibovu ripoti ilivyorudi imejaa mafisadi chungu mzima akasema hatuwezi kufanya lolote itabidi tuitumie hii ripoti kwa mikataba ijayo nikajua basi amekwishamalizika. what is going to stop others from doing the same things if you don't start from them??
 
​Acha kudanganya Muhongo siyo mtaalamu wa nishati na gesi bali ni mtaalamu wa geology!
 
Mafisadi wamemzunguka kila kona, sababu zinazotolewa za ukosekanaji wa ngozo ni za ajabu sana. Na jinsi mafisadi walivyo watahakikisha Mhongo anang'oka kwenye wizara hiyo yenye mirija yao mingi. Hata mimi nilijibanabana nikalipia Januari lakini mpaka leo Kiseke Mwanza haja niletea nguzo na pesa yangu wana zungushia business, sijui nikadai interest?
 
Aiseeiii, hawa jamaa ni watu wafiksi vibaya sana, ni mekaa karibia miezi sita nasubiri kuunganishiwa umeme. wanaamini katia uongo kwasabau wanaamini watanzania wanauelewa mdogo sana
 
Sasa ukitaka kupata starehe msikilize badra Masoud anavyo jitutumua kuhusu urahisi wa kuunganishiwa umeme, kama tayari unao hauwezi kujua jinsi inavyo kuwa ni kasheshe kuupata huo "mgao wa umeme"
 
Sawa mkuu nilijua ni mtaalamu wa hayo mambo kumbe siyo..Nadhani mambo mengi yamehamia kwenye gesi ya mtwara na kusahau mangine..
​Acha kudanganya Muhongo siyo mtaalamu wa nishati na gesi bali ni mtaalamu wa geology!
 
Sawa mkuu nilijua ni mtaalamu wa hayo mambo kumbe siyo..Nadhani mambo mengi yamehamia kwenye gesi ya mtwara na kusahau mangine..

Ni kweli mambo yako hot kwenye nishati zaidi kuliko kwenye madini! Na huko ndiko kwenye fedha zaidi!
 
Na cha ajabu zaidi nguzo zenyewe zinapatikana Mufundi ila watakwambia wanaagiza kutoka Africa ya Kusini kule ndio bei rahisi ukilinganisha na za hapa kwetu Mufindi kweli nchi yetu inaliwa na wenye meno.Hizi ahadi za wanasiasa sio za kutilia maanani sana ni za majukwaani tu hazina mbele wala nyuma.
 
​Acha kudanganya Muhongo siyo mtaalamu wa nishati na gesi bali ni mtaalamu wa geology!
Sure. Yeye kuwa waziri anatakiwa asikilize, kuwatambua, wataalamu waliobobea kwenye uchumi wa nishati, gesi, na madini. Kama hawapo je nchi inafanyaje kwenye vyuo. Sua kuna kozi ya Uchumi wa kilimo. (Agricultural economics). Ni nchi mbili tu duniani zina fundisha Mineral, gas, energy economics. USA na Australia.
 
Sure. Yeye kuwa waziri anatakiwa asikilize, kuwatambua, wataalamu waliobobea kwenye uchumi wa nishati, gesi, na madini. Kama hawapo je nchi inafanyaje kwenye vyuo. Sua kuna kozi ya Uchumi wa kilimo. (Agricultural economics). Ni nchi mbili tu duniani zina fundisha Mineral, gas, energy economics. USA na Australia.
Kama nina kumbukumbu nzuri kuna vijana wapatao 200 ambao ama wamepelekwa au watapelekwa nje kusomea taaluma hizo!
 
Aisee mie nipo moshi vijijini nimelipa toka feb nihitaji nguzo moja lakini wapi mpaka uwalambe miguu na pesa zetu wanazo
 
Muhongo hajui chochote juu ya gesi. Kama Ileje alivyosema yy ni mtaalamu wa miamba(geologist), hata hivyo sidhani kama practical zaidi maana si unajua malecturer wetu hawaendi field work prior to teaching...mtu anaikwaa first class yake murua, anakuwa tuitor, anasoma masters nad PhD mfululizo anaendelea kukata chaki....wanakosa field exposure. Kwa wenzetu kukamata chaki vizuri inabidiwe na field experience sio chini ya 5 years.

Anyway, ndio wataalamu wetu tulionao
 
Muhongo nilimuona bonge la waziri lakini kwa haya nimemwona ni mwanasiasa tu
 
Mu-h-ongo ni mtaalamu wa Uongo. Usitudanganye hapa. Bunge lilidhibitisha hivyo na wananchi wa Mtwara wanathibitisha hivyo
 
Back
Top Bottom