Profesa Shivji: Sijawhi tamka Muungano uvunjwe- Tanzania Daima lamuomba radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Shivji: Sijawhi tamka Muungano uvunjwe- Tanzania Daima lamuomba radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Aug 10, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nimeshtushwa na gazeti moja la kila siku (Tanzania Daima la Agosti 7, 2012) lililonilisha maneno katika kichwa chake cha habari: "Shivji, Lwaitama Wataka Muungano uvunjwe." Siwezi nikamsemea Dk. Lwaitama lakini kwa upande wangu sijasema wala kumaanisha kwamba ‘Muungano uvunjwe'. Nikitoa mchango wangu baada ya mada mbili kuwasilishwa na Prof. Abdul Sheriff na Dk. Azaveli Lwaitama, nilisisitiza mambo haya matatu ya msingi. Mosi, kwamba wasomi, wakiwemo wanahabari, wana jukumu zito la kutokupinda ukweli wa kihistoria kwa lengo la kuhalalisha mtazamo na msimamo wao kuhusu Muungano.

  Nikatoa mfano wa jinsi Hayati Sheikh Abeid Aman Karume anavyodokezwa katika msimamo wake juu ya Muungano. Wasemaji hapa bara wanamsifu kwa kuwa muasisi mwaminifu na shabiki mkubwa wa Muungano tangu mwanzo.

  Huko Zanzibar, wasemaji hawachoki kumnukuu Mzee Karume kuwa tangu mwanzo yeye hakutaka Muungano isipokuwa alikuwa anafikiria Shirikisho. Wanaendelea kusema kwamba aliposaini Mkataba wa Muungano, Mzee Karume alifikiri kwamba anasaini shirikisho la serikali tatu, lakini kutokana na kiwango cha elimu yake hakuelewa vizuri mantiki na maana ya alichokuwa anasaini.

  Nikaendelea kueleza kwamba maelezo haya yote mawili hayaungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Ukweli ni kwamba Mzee Karume aliingia katika Muungano kutokana na hesabu zake mwenyewe za kisiasa.

  Muungano kwake ulikuwa njia ya kuondoa upinzani, au upinzani tarajiwa, wa utawala wake. Yaani ilikuwa ni tendo la mwanasiasa yeyote yule kudumisha utawala wake (political survival).

  Na kwa watawala wote wa Zanzibar waliomfuata, wakiwemo wa upinzani, ndivyo ilivyokuwa. Wamekuwa wakitumia mwavuli wa Muungano wakati utawala wao uko hatarini na kushawishi wananchi wao dhidi ya Muungano wakitafuta umaarufu wa kisiasa.

  Nikitoa mfano nikasema kwamba kuna taarifa kwamba chama kimoja huko Zanzibar kinapandikiza pendekezo la ‘muungano wa mkataba, sio wa katiba' bila ya kueleza waziwazi maana yake.
  Ukweli ni kwamba huwezi ukawa na Muungano wa mkataba bila kwanza kuuvunja Muungano. Kwa hivyo, wanachoshawishi moja kwa moja ni kuuvunja Muungano. Basi waseme hivyo badala ya kujificha nyuma ya pazia la ‘muungano wa mkataba'.

  Jambo la pili nililorudia ni kwamba tuliangalie suala zima la Muungano kwa mtazamo na maslahi na matakwa ya umma wa Zanzibar na umma wa Tanzania Bara, hususan matabaka ya hali ya chini. Katika hali yao kimaisha – kiuchumi na kisiasa – hakuna tofauti kati ya wananchi wa Zanzibar na wananchi wa Tanzania Bara.

  Uduni wa hali yao ni uleule; ukosefu wa ajira ni uleule; kutokuwa na mfumo wa dhati wa demokrasia unaojali walalahoi ni ulekule. Kwa hiyo, umuhimu kwao ni mshikamano wao kuboresha mifumo ya uchumi na siasa. Wasiburuzwe na wanasiasa na vyama vyao kwa maslahi yao binafsi ya muda mfupi ya kudumisha, au kuingia kwenye, utawala.

  Jambo la mwisho nililogusia ni kwamba kiini cha suala la Muungano si idadi ya serikali (mbili au tatu) bali ni mgawanyo wa madaraka (distribution of power) kati ya dola la Zanzibar na dola la Muungano.

  Na katika hili kila Muungano huu duniani ni wa kipekee kutokana na hali halisi yao ya kihistoria na uwiano wa kisiasa. Sisi pia tukiwashirikisha wananchi kikamilifu na tukaelewa vizuri matakwa yao tunaweza kubuni muundo wetu wa Muungano ambao ni wa kipekee bila kujali idadi ya serikali.

  Nimeona niweke wazi mtazamo wangu kwa sababu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa na hulka ya kupotosha mambo kutokana na ushabiki wao bila kujali madhara yanayoweza kutokea. Mwishoni ningependa kusema kwa dhati kwamba uvunjaji wa Muungano hauwezi kuwa kwa manufaa ya walio wengi. Ukweli ni kwamba unaweza ukasambaratisha nchi na jamii zetu pande zote mbili za Muungano.

  Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo. Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea kuila kila siku.

  Mytake: Nadhani hapa Tanzania Daima mlichemka sana...tunapaswa kuwa makini wakati mwingine tusiharibu mapambano yetu ya kuikomboa hii nchi.


   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa ndio uandishi makini !!nawapongeza Tanzania Daima
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Eti makosa ya kiuandishi. Tanzania daima walifikiri ni hoja ambayo ingeonesha kuwa wasomi wako kinyume na Katiba ya Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kwa ujumla.

  Tatizo hapa ni elimu ndogo ya waandishi wetu na papara za kuandika bila kutafakari kama amri aliopewa ina maslahi na inamshushia hadhi au la.

  Sasa wanajifanya kuomba msamaha.
   
 4. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mmeajiri 'makanjanja' wengi mno. Ati 'fomu foo felia' anaelekezwaelekezwa na kuwa mwandishi wa habari. Hii ndo inaitwa KUIBAKA TAALUMA hii.
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Gazeti la mbowe kazi kweli kweli!maana limezoea kuandika propaganda.
   
 6. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  sisi tumewazoea wahariri wetu wa kitz kwa uupotishaji wa makusudi tumeshuhudia mara nyingi mfano inapotokea ajali kila gazeti hua linaandika idadi yake.Jamani waharirir wetu vihio nendeni shule!
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Tanzania Daima msitake kuudanganya umma. Ukweli ni kwamba mlimnukuu Shivji vibaya kimakusudi kwa kuwa kuvunja muungano ni hoja inayoendana na Chadema. Mlitaka kufanya mass influence mkijua wengi wetu tunamheshimu sana Prof. Shivji.

  Ni very unethical kwa gazeti kuwa upande wa sera za mmiliki wake kwa njia za kificho (subtle) kama hii. Unprofessionalism of the highest order.

  Nikiwa mtu nisiye na upande wowote kisiasa, kuna mengi siyapendi katika CCM, na pia kuna mengi nayakubali katika Chadema, na mojawapo ya nisiyokubaliana katika Chadema ni msimamo wao juu ya muungano.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,134
  Trophy Points: 280
  ..Prof anacheza na maneno tu.

  ..nina hakika ziko makala alizoandika akidai kwamba muungano umekosa msingi wa kikatiba na kisheria.

  ..sasa ukishasema hivyo maana yake ni kwamba muungano ni batili.

  ..kama muungano ni batili basi unapaswa kuvunjwa.

  ..naona wapinga muungano wengi sana wanabadili kauli na misimamo yao baada ya kuona wa-Tanganyika tumeamka na kuanza kuhoji dhuluma tunayotendewa ktk muungano.

  ..MUUNGANO NI DHULUMA KWA WATANGANYIKA.
   
 9. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Mimi nataka mtu kama Prof. awaeleze kinabaubaga Wazanibari kuwa tunataka taifa moja , nchi moja serikali moja, asiyetaka afungashe virago arudi zanzibari Kwishney. Kelele za kero ya muungano zitaishia hapo , mbona mnabebeleza sana hawa waunguja wana kitu gani cha zaidi achana nao !
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,134
  Trophy Points: 280
  Wachovu,

  ..Prof amewaambia wa-ZNZ kwamba wataathirika zaidi ikiwa muungano utavunjwa.

  ..pendekezo la Prof.Shivji ni kuwa na mfumo ambapo tutakuwa na Raisi mmoja, akisaidiwa na Waziri Mkuu.

  ..katika pendekezo hilo, Raisi na Waziri Mkuu, watatoka pande tofauti za muungano.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ingekua uhur wameomba radhi, si ajabu ungesema wana matatizo kwanini hawakuchunguza kabla ya kuandika
   
 12. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuomba radhi ni jambo zuri katika uandishi, lakini angelieni sana taarifa zenu kabla ya kuandika!
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Hawa hata wakijikata bado watarudi katika EAC.
  Kelele zitaisha, usanii utaisha na ushirikiano mpya utazaliwa ambao nao utakuwa na changamoto zake.

  Wachovu hakuna nchi inayotaka/inayopenda kupoteza mamlaka yake.

  Kwa maelezo ya Prof, zipo dola mbili, dola ya Zanzibar na dola ya muungano ambayo ndani yake pia imo dola ya Tanganyika. Kumbuka, dola ya Tanganyika imekasimu madaraka yake kwa dola ya muungano. Unapokasimu maana yake bado unaishi/upo. Huu usanii wa muungano unaofanyika unaparaganya wengi, haueleweki.

  Nililoelewa mimi katika aliyosema Prof. Shivji ni kuwa kuwe na mgawanyo unaoeleweka wa madaraka. Kitu ambacho wanasiasa wetu wanakichezea sana/ uzembe/ au kuna kitu kinafichwa na ni kitu ambacho kinatuletea hizi zinazoitwa kero za muungano.

  Tanzania haijawahi kuwa nchi moja, Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Kwa nini nasema haijawahi kuwa nchi moja?

  Kwa sababu, mkataba wa Muungano unasema kutakuwa na mambo ya muungano na kutakuwa na mambo ambayo si ya muungano.
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  JokaKuu

  Prof. ni Mtanganyika hivyo haingii katika kundi hilo lenye rangi nyekundu.

  Prof. ni msomi aliyebobea na kama unafuatilia maandiko yake na mada zake utagundua mara nyingi husemea walalahoi wa pande mbili za muungano.

  Pia mara nyingi huwatupia lawama wanasiasa kwa usanii wanaoufanya.

  Kweli prof. ameandika kitabu na humo amesema kuwa muungano umekosa msingi wa kisheria.

  Hapa sifikiri kuwa Prof. anamaanisha Muungano uvunjwe. Nilivyoelewa mimi amewaonesha wanasiasa kasoro iliyopo ya muungano na ni jukumu la wanasiasa na wananchi kulirekebisha hilo. Viongozi waliopo madarakani kama ni wafanya maamuzi magumu na ya busara basi kura ya maoni kwa pande zote mbili kuamua hatma ya muungano au wajumbe/wawakilishi wa Tanganyika na wajumbe/wawakilishi wa Zanzibar wangepitia tena mkataba wa muungano ili huo uhalali wa kisheria upatikane.

  Prof. amesema hivi: "Muungano kwake ulikuwa njia ya kuondoa upinzani, au upinzani tarajiwa, wa utawala wake. Yaani ilikuwa ni tendo la mwanasiasa yeyote yule kudumisha utawala wake (political survival)."

  Utaona hapa kuwa huu ni ukweli mtupu.kwa viongozi waliopita na hata CCM ya leo. CCM wamesema muungano usiguswe katika maoni ya katiba mpya,kwa sababu bila ya muungano CCM inakwenda na maji.

  Prof. anasema Jambo la mwisho nililogusia ni kwamba kiini cha suala la Muungano si idadi ya serikali (mbili au tatu) bali ni mgawanyo wa madaraka (distribution of power) kati ya dola la Zanzibar na dola la Muungano.
  Hili ndio limekuwa tatizo sugu na ndio linaloibua kelele na sitofahamu zote za Muungano.

  Na kutokana na usanii wote unaofanyika, tukishindwa kuweka sawa muungano wetu hii hali itakuja kama anavyosema Prof."Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea kubaguana kwa msingi wa Uislamu na Ukristo, na Usukuma na Uchaga, Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo. Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea kuila kila siku."

  Naona sasa mjadala wa muungano unachukua hali ya ushabiki wa Simba na Yanga badala ya kutazama kipi kizuri kikaendelezwa na ipi kasoro ikashughuliwa/ikatatuliwa.

  Tuna mzozo wa mpaka na Malawi.Kuna wadau wametoa wazo kuwa tuunde muungano na Malawi. Ni wazo zuri kwa kweli. Lakini unafikiri Malawi watafikiri/ watakubali kuungana nasi baada ya kuona vipi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unavyoendeshwa?
  Unafikiri Malawi watapenda itokee siku waambiwe wao ni kamkoa/ wilaya tu?

  Litakalotokea baada ya kelele nyingi kama kasoro za muungano hazitorekebishwa basi Tanganyika itapasa ichukue hadhi ya mkoloni na kuichukua/kuimeza Zanzibar kwa nguvu au kwa hadaa au Muungano utavunjika.

  Katiba mpya itakapokamilika tutapata mwanga wa wapi Tanzania inaelekea.


   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,134
  Trophy Points: 280
  Nonda,

  ..Kwa mtizamo wangu makala nyingi za Prof zimekuwa zikitu-portray wa-Tanganyika kama tunawadhulumu wa-ZNZ ktk muungano.

  ..Zanzibar haichangii ktk gharama za kuendesha shughuli za muungano, sasa nilitegemea Prof.Shivji angekuwa mstari wa mbele kulizungumzia suala hilo.

  ..sijawahi kumsikia Prof.Shivji akilaani kitendo cha wa-Tanganyika kuwekewa vikwazo ktk kumiliki ardhi ZNZ, au wanaponyanyaswa kwa misingi ya kidini, au ZNZ kutumika kama kichaka cha kukwepa kodi na ushuru na kuinyima serikali ya muungano mapato?

  ..Katika wasomi namkubali zaidi Prof.Teddy Malyamkono kwasababu yeye ndiye amebainisha dhuluma ya jinsi Zanzibar ilivyokuwa mzigo wa kiuchumi kwa wa-Tanganyika.

  ..Pamoja na kusema hayo, nampongeza Prof.Shivji kwa kuwaambia ukweli wa ZNZ kwamba Sheikh Karume ndiye aliyeweka saini mswada wa sheria uliopelekea mafuta kuwa suala la muungano. Sheikh Karume alifanya hivyo wakati akikaimu nafasi ya Raisi wa muungano.

  ..Kwa maoni yangu huwezi kuzungumzia mgawanyo wa madaraka[distribution of power] bila kuuhusisha kwa namna moja au nyingine na idadi ya serikali[1,2,3, au hata 4]. Prof anapozungumzia mgawanyo wa madaraka kati ya dola ya Zanzibar na dola ya muungano, tayari anazungumzia idadi ya serikali ambazo ni 2.

  ..Zaidi, status ya Zanzibar kama dola ni suala la mjadala. Kuna wakati CUF wali-argue na kushinda mahakamani kwamba Zanzibar si dola, hivyo huwezi kutenda kosa la uhaini dhidi yake!!
   
 16. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Toa mifano, weka chanzo, vyenginevyo na wewe utakuwa unamtilia maneno kinywani ambayi hakuwahi kuyasema (kuyaandika).

  Toa mifano ya hoja yako, weka chanzo, na wala sio tafsiri yako kwa kile alichowahi kuandika au kukisema. Msimuingizie maneno kinywani ambayo hakuyasema (au kuyaandika).
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,134
  Trophy Points: 280
  MAMMAMIA,

  ..Prof amewahi kuandika makala ktk gazeti la raiamwema iliyokuwa na kichwa cha habari, "Katiba ya muungano haina uhalali wa kisiasa wala kimuafaka." Nakushauri uende kwenye website ya raiamwema ili uweze kuisoma.

  ..Zaidi, kuna mwandishi wa jukwaa la wa-ZNZ, www.mzalendo.net, anaitwa Foum, naye amemnukuu Prof.Shivji kama nilivyoeleza ktk post yangu. soma hapa chini:

   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Professor shivji naona baada ya kukosa kuwepo kwenye Tume ya katiba akalialia hapa sasa ccm imempa vihela anaaza kucheza na Maneno yeye ni mmoja wao anayetakiwa kufungasha virago
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Unakusudia kusema ma-ga-ba-cho-li wote wanatakiwa kufungasha virago?

  Na huyu mzee hapa naye pia afungashe virago?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jokakuu, katika bandiko lako #5 na 15 naafiki bila shaka. Wakati wa mchakato wa rasimu ya uandikaji katiba, Pro Shivji alifanya makongamano ZNZ (Rejea JF na mzalendo.net kwa kumbu kumbu).

  Mara zote ameeleza kukosekana uhalali wa muungano na jinsi Nyerere alivyofinyanga mambo. Amewahi kusema muungano ni batili na kama ni batili basi uwepo wake ni batili na hapo maana yake usiwepo achilia mbali kuuvunja.

  Mara zote Prof Shivji amezungumzia mgawanyo wa madaraka na jinsi gani ZNZ inakosa fursa kutokana na muungano uliopo.
  Hakuna mahali nilopowahi kumsikia prof akiongelea fursa wanazopata WZNZ hata kama ni chache zitokanazo na muungao.

  Leo katika sahihisho anasema watu wazingatie zaidi hali za watu wa chini wa pande zote.
  Ukweli ni kuwa anaficha kusema watu wazingatie hali za Wazanzibar wa kawaida.
  Ni hali za WZNZ kwasababu wao 350,000 wanaishi Tanganyika. Ukisoma makala nyingi za Shivji zimeegemea sana kutetea Uzanzibar. Hata kama ni Mtanganyika anaweza kuwa na motive nyingine ambayo si rahisi kuiweka wazi katika kiwango chake cha usomi.

  Mkuu Nonda, naomba nikunukuu

  ''Naona sasa mjadala wa muungano unachukua hali ya ushabiki wa Simba na Yanga badala ya kutazama kipi kizuri kikaendelezwa na ipi kasoro ikashughuliwa/ikatatuliwa.

  Tuna mzozo wa mpaka na Malawi.Kuna wadau wametoa wazo kuwa tuunde muungano na Malawi. Ni wazo zuri kwa kweli. Lakini unafikiri Malawi watafikiri/ watakubali kuungana nasi baada ya kuona vipi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unavyoendeshwa?
  Unafikiri Malawi watapenda itokee siku waambiwe wao ni kamkoa/ wilaya tu?

  Litakalotokea baada ya kelele nyingi kama kasoro za muungano hazitorekebishwa basi Tanganyika itapasa ichukue hadhi ya mkoloni na kuichukua/kuimeza Zanzibar kwa nguvu au kwa hadaa au Muungano utavunjika.
  Katiba mpya itakapokamilika tutapata mwanga wa wapi Tanzania inaelekea''

  Kwanza, hilo wazo la kuungana na malawi ni porojo na nashangaa umelichukulia serious. Ukiangalia kitaalamu muungano wetu na Malawi hauwezi kutokea bila kuwa na usaidizi wa jumuiya nyingine. Kikubwa ni kuwa kiutamaduni hatupo karibu kabisa na Malawi. Ungefikiria Burundi ningekuelewa.

  Pili, leo umegeuka na kuanza kufikiria kuwa tuchukue mazuri na tuache mabaya!
  Nashangaa sana. Nadhani WZN wanaanza kuona wapi wanakosea.
  Kukaa kimya kwa Watanganyika kuliwapumbaza WZNZ na kudhani ni wadau wakubwa sana wa muungano.
  Kila walichoomba au kutaka walipewa, zama hizo zimefika mwisho.
  Nonda, unapingana na WZNZ wanaotaka muungano ufe, unapingana na Watanganyika wengi wanaosema LET ZNZ GO!

  Jitihada za kufuata mazuri na kuacha mabaya zimefanywa na Tanganyika kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuvumilia matusi, kashfa na kejeli tukisemwa tunawanga'ng'ania.

  Wenzetu ZNZ hawakuwa tayari, na sasa sioni ni kwa vipi tutawashawashi Watanganyika waitwe wakoloni kwa gharama zao.

  Mimi binafsi nawa-challenge Watanganyika wajiulize, katika muungano huu wanadhani uwepo wa ZNZ unawasaidiaje na kutokuwepo kwa ZNZ kutawaathiri nini.

  Ni lazima Watanganyika waelewe kuwa gharama za muungano wa serikali 2, 3 au mkataba watazibeba wao.
  Sasa ni biashara gani tutaifanya na ZNZ kiasi chakudhani kuwa mtaji mkubwa wa muungano tulioweka au tutakaoweka utatunufaisha.

  LET ZNZ GO!
   
Loading...