Profesa Shivji:"Rais Jk ana mamlaka kisheria kuwabana mafisadi" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Shivji:"Rais Jk ana mamlaka kisheria kuwabana mafisadi"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Dec 16, 2009.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]*WENGINE WAMTAKA WAZIRI CHIKAWE AACHE KUKURUPUKA


  Na Sadick Mtulya

  SIKU moja baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe kusema Rais Jakaya Kikwete hawezi kutumia mamlaka yake kuwabana mafisadi, baadhi ya wanasheria nchini, akiwamo Profesa Issa Shivji, wamepinga kauli hiyo kwa kusema sio kweli.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana wanasheria hao walisema rais anaweza kuwabana mafisadi kwa kutumia mamlaka yake ndani ya chama na serikali.

  Profesa Issa Shivji alisema Rais Kikwete anaweza kupambana na watuhumiwa wa ufisadi kwa kuwavua madaraka walionayo katika chama au serikali.


  Gwiji hilo la Sheria na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, alisema kama watuhumiwa watakuwa watumishi wa serikali au watendaji katika mashirika ya umma, rais anaweza kuwawajibisha kwa kutumia sheria na kanuni za utumishi wa umma.


  “Kumwajibisha mtuhumiwa sio iwe kumpeleka mahakamani, unaweza kuchukua hatua za awali ikiwemo kumvua nyadhifa zote. Kama ni mwanasiasa au mtumishi katika serikali na mashirika ya umma, unaweza kumwajibisha kwa mujibu wa sheria za umma," alisema Profesa Shivji.


  Alisisitiza “Kusema Rais Kikwete hana uwezo wa kuwabana mafisadi sio kweli na Watanzania wanatakiwa kuelewa hivyo kwamba rais anaweza.”

  Kauli ya Profesa Shivji iliungwa mkono na Profesa Abdallah Safari, aliyetia ngumu akisema sheria za nchi ikiwemo ya utawala, inampa uwezo na mamlaka rais kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya serikali yake na hata katika chama chake.

  “Rais kukasimu mamlaka yake kwa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ) na kwa DPP haimaanishi kwamba sasa yeye hana uwezo wa kupambana na watu wanaojihusisha na ufisadi. Bado anao,” alisema Profesa Safari.

  Alifafanua kwamba, Rais Kikwete anayewajibika katika kupambana na ufisadi kwa kuwa yeye ndiye anayewajibika moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania.

  Profesa Safari ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa umma, alisema rais anatoa madaraka kwa vyombo vingine ili kusaidiwa, lakini bado ndiye anayewajibika kwa kuhakikisha vyombo hivyo vinawajibika ipasavyo.

  "Suala hili ni kama vile baba anamwambia mtoto wake nisaidie jambo hili na kama akishindwa au akifanikiwa na yeye anawajibika katika hayo, sasa kusema hana uwezo wa kupambana na mafisadi sio kweli na kauli hiyo inapotosha jamii," alisema Profesa Safari.

  Dk Sengondo Mvungi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema Rais Kikwete ana nafasi ya kiutendaji kuhakikisha anapambana na watu wanaotuhumiwa na wanaojihusisha na ufisadi katika serikali yake.

  "Kusema Takukuru na ofisi ya DPP ndiyo inapaswa kuwashughulikia watu hao kwa kuwapeleka mahakamani ni sawa, lakini, rais naye ana nafasi yake katika hilo. Anaweza kufanya hivyo kwa mamlaka aliyonayo kama mkuu wa nchi au mwenyekiti wa chama," alisema Dk Mvungi.

  Alisisitiza kwamba, Rais Kikwete anapaswa kuwajibika kwa kuwa ndiye mkuu wa serikali inayoingia mikataba hivyo kusema kwamba hana uwezo sio sahihi.

  “Waziri Chikawe asizungumze mambo ki-uanasesere. Kwa kuwa kila hatua inayochukuliwa ikiwemo kusaini mikataba ni lazima kwanza Cabinet (Baraza la Mawaziri) ipitishe na hiyo mikataba ndiyo iliyozaa vitendo vingi vya ufisadi sasa ukisema rais hana uwezo maana yake nini? Hizo ni porojo zisizokuwa na msingi wowote," alisema Dk Mvungi.


  Dk Mvungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR Mageuzi, alisema kutokana na mgawanyo wa madaraka katika dola Rais Kikwete anahusishwa na kila jambo linalotokea nchini kwa kuwa ndio kiongozi mkuu.


  Juzi waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema Rais Kikwete hana uwezo kutumia mamlaka yake kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kwani hilo ni jukumu la vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchambua nani afikishwe huko baada ya kujiridhisha kwa ushahidi.

  "Huu ni utawala wa sheria, Rais Kikwete hawezi kutoa amri za kukamata watu wakati kuna vyombo alivyoviteua kuchunguza na kuchukua hatua." Waziri Chikawe alisema hayo juzi alipokuwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema kitendo cha baadhi ya Watanzania kumshinikiza Rais Kikwete awafikishe mahakamani watuhumiwa wa ufisadi kinaashiria kuwa wanataka aamuru watuhumiwa hao wapelekwe mahakamani bila kutumia vyombo husika jambo ambalo haliwezekani katika mfumo wa kibepari.

  "Enzi zile za mfumo wa ujamaa na chama kimoja cha siasa, hilo lingewezekana, lakini wakati huu ambao nchi inatumia mfumo wa kibepari, haiwezekani," alisema Chikawe.
  Hivi karibuni, wanasiasa na hata baadhi ya viongozi waliowahi kuwa serikalini awamu zilizopita, wakichangia mada ya mustakabali wa taifa kwenye kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waliitaka CCM imtose Rais Kikwete asigombee tena ili kumalizia ngwe ya miaka mingine mitano, iwapo tashindwa kufanya maamuzi magumu ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  anamamlaka kweli ila nia wala jeuri ya kuwakamata hata kuwakemea hana, anacheka nao, anakula nao, anawabembeleza, anawaogopa.....hana kujiamini na mamlaka yaliyo mikononi mwake.
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sheria moja interpretation ya Shivji au A.G ipi tufate???
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  JK si tu ana mamlaka kisheria kuwafanyia kweli mafisadi, bali ana mamlaka kisheria kumfunga mtu yeyote indefinitely bila kutoa sababu under the controversial "indefinite detention" powers.

  The point I am trying to make here ni kwamba hatuna tatizo la rais kukosa nguvu, kama tuna tatizo Tanzania ni kwamba rais ana nguvu sana. Nyerere mwenyewe kashasema hili, Kikwete mwenyewe kasema hili bungeni Dodoma, sasa huyu Waziri anasema nini?

  Huwezi kusema hana uwezo, labda hana nia.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Waziri wa sheria hata kama ni msomi aliebobea ili hali anaambatana na CCM amepofushwa macho kutokana na kiburi,rushwa,choyo,umajinuni,ubaradhuli na mawazo ya ukoloni wao mweusi, kwake kujipendekeza kwa RAIS ni jambo la maana zaidi ya mantiki ya kile aongeacho, anajivua nguo hadharani ili tu apate ugali wake, mtu kama huyu asingepata kazi nzuri bila sha angekua .s.ridhiki, aibu sana.
  Shivji ni mwanataaluma aliebobea katika taaluma ya sheria, maisha yake yote alikataa kuchotwa na mawazo dhariri, na kamwe hakujitenga na watu wa kawaida , daima amekua mtu anaetoa tafsiri jadidi za Kisheria katika maswala mazito kitaifa....huyu ni MTANZANIA wakipekee, hajajificha kule upanga ama Maghorofani kama Wadosi wa rangi yake wafanyavyo, hana woga, ni mwanazuoni makinI.
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  I really admire my 'lecturer', na kubaliana nawewe zaidi kwenye hayo nlopigia msatari.

  Mtanzania wa Kilosa mwenye mapenzi ya dhati kwa nchi yake....waache hao vibaraka waendelee kujipendekeza ila siku yaja!!!
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi kusema Kweli nashangaa Rais J.K anatumia vigezo gani wa kuwachagua baadhi ya wasaidizi wake? Nimemsikia mara nyingi Waziri Chikawe akizungumza kuhusu mambo fulani muhimu ya kisheria na mara nyingi anakuwa ambigous! Hivi kweli katika watanzania 40 milioni tumekosa mtu makini wa kuongoza wizara kama ya Sheria kwa ufanisi? Au tumefulia katika nyanja ya sheria kama tulivyofulia katika kucheza kabumbu!
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  wmeteuliwa kiambiguiti ambiguiti na utendaji ni kihivo hivo!!! what else would one expect....
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  roho ya upendeleo huzaa laana na matatizo sana, serikali yake imekosa baraka na ufanisi, imeshindwa kutukwamua, nnchi imekwama, kila siku ni vilio na kusaga meno. uteuzi wawashikaji katika nafasi nyeti za utendaji zimemgharimu sana, hebu angalia uteuzi wake huu
  Sofia Simba
  Hawa Ghasia
  Chikawe
  KULIKUA na KINGUNGE
  Adamu Malima
  makongoro mahanga
  kulikua na Bangusilo
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  With no any prejudice...we are in sh...t
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  sasa njoo katika CCM wasaidizi wake ni hawa
  Mzee Yusufu Makamba .....katibu mkuu
  Tabwe Hiza......... mkuu wa propaganda
  John Chiligati........ katibu mwenezi
  Sofia Simba mwenyekiti UWT....JK Inadaiwa alimuunga mkono na haijakanushwa.
  Andrew Chenge .....Msimamizi mkuu wa maadili CCM
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Chikawe,
  Ahaa sasa ina maana kuwa ubepari ndio mfumo unaoruhusu uoza, and we've opted for that, sawa Chikawe tumekusikia. Kwa nini sasa usipendekeze mabadiliko ya katiba tufute kabisa ujamaa na kujitegemea kwenye katiba kisheria ? Ila be carefull mkuu, as time goes unazidi kuongea pumba. I believe ur next speech will be a further crap, better keep quiet. Watanzania sio mabwege tena. Dr. H. Mwakyembe MP.
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hawa akina Chikawe ni kizazi kilichoonja utamu wa ufisadi, daima wako tayari kupambana mpaka damu ya mwisho ktk kutetea mambo yakijinga kabisa....ni kama wamelaaniwa.
   
Loading...