BinMgen
JF-Expert Member
- Jun 18, 2008
- 1,854
- 262
MrFroasty, bila ya shaka alichosema Prof. Shivji kinaitwa hekima. Sidhani kama kinaweza kuzua mjadala mkubwa. Tatizo ni pale watu wanapoamua kutunga historia au kuficha historia kamili ya Zanzibar au kutoa historia kwa kudonyoa donyoa huku yale mazuri ya kufurahisha ndiyo yanawekwa mbele na mengine hata kutajwa hayatajwi. Zanzibar ina historia yake nzito sana na haikuanzia 1964.
Ni muhimu Wazanzibar wakumbatie na kukubali historia yao yote na hiyo iwe ni sehemu ya maridhiano hayo.
Hakuna haja ya kukumbatia jambo sililo na faida. Historia ya Zanzibar haina nafasi wala faida yoyote katika jamii inayotaka kusonga mbele, hasa kizazi cha sasa. Matatizo yanayo ikumba zenj ni zao la kukumbatiwa na kuhubiriwa histori. Historia ni kitu kilicho pita, historia isiyo na faida hupitiliwa mbali, na badala yake watu hutafuta lenye faida na wao wakalikumbatia. Leo watu wataka kusahau yaliyopita ili wajenge NCHI YAO unawakmbusha histori!!. Zile kauli za MAMBO YA ZANZIBAR YATAMALIZWA NA WAZANZIBAR WENYEWE mmezisahau?? au kuuwana kwao ndio furaha yenu?.