Nyaru-sare
JF-Expert Member
- Aug 2, 2019
- 5,263
- 3,625
Msomi wa kiwango cha kimataifa wa Tanzania, Profesa Shivji ameshangazwa na kitendo cha wafanya biashara kuchaguliwa kuongoza taasisi za umma.
Shivji anasema sekta ya umma haiwezi kuchangamana na sekta binafsi.
Sisi wengine tumeshangazwa na uteuzi wa wafanya biashara na watu wenye maslahi binafsi kwenye bodi ya TANESCO. Yule mama Balozi ndie mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Rex Attorneys ambao wanaiwakilisha Dowans na Symbion kwenye kesi ambazo TANESCO inashitakiwa na hayo makampuni halafu anateuliwa kuwa board member.
"Pamoja na kushirikiana na sekta binafsi, huwezi kuwaingiza wafanyabiashara jikoni wakupikie chakula cha umma!
Sekta ya umma na sekta binafsi hazilinganiki. Ni kweli huwezi kuendesha biashara kama idara ya serikali; pia ni kweli huwezi kuendesha serikali kama kitengo cha biashara."
Unaweza kusoma mwenyewe hapa.
View attachment 1954110
Mleta Mada!..... UMMA ni nini?
Humo kwenye Umma kuna mchanganyiko wa wafanyakazi na wafanya biashara pia!! hata hao wafanya kazi wa umma siku hizi ni wafanya biashara pia!! wakulima ni wafanyabiashara pia kupitia mazao yao!!
mfano unapokula chips za mkulima palee! Masangati unalipia kila, mlo? ivoivo na kwa mazao mengine pia je huo siyo umma wa wafanya biashara?
unamnunukuu Huyo mzee kizembe na siasa zake ni za zamani sana! wkt wa enzi hizo babu zetu hawaku soma! ...... Kampuni ya Tanesco ni ya Umma pia inafanya biashara!! sasa kwa nini usiweke wananchi wenye maono ya kibiashara? kinyume na hapo ni ubaguzi?
Siyo kila alichoandika professor ni sahihi!!! hawezi pita humu bila changamoto! kamwambie huyo professor atoe maelezo kwa hayo maoni yangu!! kifupi hatuwezi chukua wapiga debe wa mbagala wakasimamie Tanesco! hata wao hawatakuelewa! watakupuuza!
kwa sababu hawajawahi kuota kufanya hiyo kazi!! lkn je wanaipenda? wana mikakati yenye tija? wana maoni mazuri kuhusu Tanesco? Huyo professor wako akumbuke kuwa sisi tuna chagua mtu kutokana na vipaji vyao, upenzi, uwezonk, wa kufanya ile kazi!
yaani huyo mzee ana taka tuweke nani sasa km siyo hao? wafugaji au?? hizi Siasa za nyerere hizi, hata mwenyewe alizistukia kitambo sana!