Tumia akili
Member
- Apr 1, 2013
- 66
- 1,165
Hello JF.
Nimesoma makala hii na kushtushwa sana na kilichoandikwa kuwa viongozi wa CHADEMA walimuomba huyu Profesa Safari kujiunga nao. Najiuliza, huu ni utaratibu wa wapi? Katika hali ya kawaida ningetegemea msomi kama huyu awe amesoma vizuri katiba na sera za CHADEMA kabla hajaamua kujiunga nacho.
Je, ina maana vyama vingine navyo vinaweza kumuomba na akajiunga navyo?
Je, kila mtu anaweza kuja na maelekezo kwa CHADEMA juu ya nini wafanye ili ajiunge nao?
Habari kamili.
VIONGOZI na wananchi wanaoishi kwenye nyumba za Serikali zilizouzwa miaka kadhaa iliyopita wametahadharishwa kuwa, zitarejea mikononi mwa umma wakati wowote ule. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na RAI jijini Dar es Salaam wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema sula hilo kwa sasa linasubiri muda tu.
"Kwanza ieleweke kwamba viongozi hao hawakununua nyumba zile, bali waligawana tu. Hilo haliwezi kudumu miaka yote kwani halikufanyika kihalali," alisema Profesa huyo msomi wa Sheria na na Lugha ya Kiswahili.
Alisema ugawanaji wa nyumba hizo kisheria unajulikana kama "inconsolable transaction" (ununuzi wa kidhalimu), kwani haukuzingatia thamani ya ardhi wala ya majengo yenyewe kwa sasa.
Profesa Safari alisema nyumba hizo zingeweza kurejeshwa mikononi mwa umma hata leo hii kwa kufuata taratibu za kisheria, lakini bahati mbaya waliopewa dhamana ya kutafsiri na kusimamia utekelezwaji wa sheria (majaji) nao baadhi yao waligawiwa nyumba hizo.
"Ni wazi iwapo Chadema tutakamata madaraka ya uongozi nchini, basi nyumba hizo zitarejeshwa kwa umma. Hilo ni moja kati ya mambo matatu niliyowaambia CHADEMA waliponiomba nijiunge na chama chao kuwa ningependa yasimamiwe kikamilifu," alisema.
Sera ya uuzaji wa nyumba za Serikali ilifanyika wakati wa Awamu ya Tatu ya uongozi chini ya Rais Benjamin Mkapa na kusimamiwa kikamilifu na Waziri wa Miundombinu wa wakati huo, John Magufuli, ingawa ilipingwa na kulalamikiwa na watu wengi.
Nyumba hizo nyingi zilikuwa maeneo maarufu kama ‘uzunguni' na zilijengwa wakati wa ukoloni na Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere maalumu kwa viongozi wa kiserikali.
Lakini kwa mshangao wa wengi, kwa sasa idadi kubwa ya nyumba hizo zipo mikononi mwa viongozi wengi wastaafu wa Awamu ya Tatu na wengine wa Awamu ya Nne wanaoelekea kustaafu huku, Magufuli akidai kuwa zitajengwa nyumba nyingine maeneo muafaka kama yale ya zamani.
Katika mahojiano, Profesa Safari pia alizungumzia tatizo la udini lililopo nchini kwa sasa, akisema nalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
"Kwenye kikao changu na marehemu Bob Makani pomoja na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) tulilizungumzia hili na nikawaomba waliweke kwenye sera za utekelezaji wa chama chetu.
"Suala la udini ni ‘hyper sensitive' na lazima tukubali kuwa udini Tanzania upo! Upo na wala si kwetu tu, hili ni suala la kimataifa na tumelirithi kutoka kwa Wakoloni. Ni lazima tulitafutie ufumbuzi na nina amini CHADEMA italitatua hili," alisema.
Profesa Safari ambaye pia ni mwanazuoni wa Kiisalamu, alivitaja vitabu kadhaa vinavyothibitisha udini nchini na kushauri Tanzania ijifunze kutoka Senegal namna walivyolitatua tatizo hilo na kuiepusha nchi yao kwenda mwelekeo wa Nigeria na nchi nyingine kadhaa.
Source: Rai