Profesa Safari: CHADEMA waliniomba nijiunge nao

Tumia akili

Member
Apr 1, 2013
66
1,165
Hello JF.

Nimesoma makala hii na kushtushwa sana na kilichoandikwa kuwa viongozi wa CHADEMA walimuomba huyu Profesa Safari kujiunga nao. Najiuliza, huu ni utaratibu wa wapi? Katika hali ya kawaida ningetegemea msomi kama huyu awe amesoma vizuri katiba na sera za CHADEMA kabla hajaamua kujiunga nacho.

Je, ina maana vyama vingine navyo vinaweza kumuomba na akajiunga navyo?

Je, kila mtu anaweza kuja na maelekezo kwa CHADEMA juu ya nini wafanye ili ajiunge nao?




Habari kamili.


VIONGOZI na wananchi wanaoishi kwenye nyumba za Serikali zilizouzwa miaka kadhaa iliyopita wametahadharishwa kuwa, zitarejea mikononi mwa umma wakati wowote ule. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na RAI jijini Dar es Salaam wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Profesa Abdallah Safari, alisema sula hilo kwa sasa linasubiri muda tu.

"Kwanza ieleweke kwamba viongozi hao hawakununua nyumba zile, bali waligawana tu. Hilo haliwezi kudumu miaka yote kwani halikufanyika kihalali," alisema Profesa huyo msomi wa Sheria na na Lugha ya Kiswahili.

Alisema ugawanaji wa nyumba hizo kisheria unajulikana kama "inconsolable transaction" (ununuzi wa kidhalimu), kwani haukuzingatia thamani ya ardhi wala ya majengo yenyewe kwa sasa.

Profesa Safari alisema nyumba hizo zingeweza kurejeshwa mikononi mwa umma hata leo hii kwa kufuata taratibu za kisheria, lakini bahati mbaya waliopewa dhamana ya kutafsiri na kusimamia utekelezwaji wa sheria (majaji) nao baadhi yao waligawiwa nyumba hizo.

"Ni wazi iwapo Chadema tutakamata madaraka ya uongozi nchini, basi nyumba hizo zitarejeshwa kwa umma. Hilo ni moja kati ya mambo matatu niliyowaambia CHADEMA waliponiomba nijiunge na chama chao kuwa ningependa yasimamiwe kikamilifu," alisema.

Sera ya uuzaji wa nyumba za Serikali ilifanyika wakati wa Awamu ya Tatu ya uongozi chini ya Rais Benjamin Mkapa na kusimamiwa kikamilifu na Waziri wa Miundombinu wa wakati huo, John Magufuli, ingawa ilipingwa na kulalamikiwa na watu wengi.

Nyumba hizo nyingi zilikuwa maeneo maarufu kama ‘uzunguni' na zilijengwa wakati wa ukoloni na Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere maalumu kwa viongozi wa kiserikali.

Lakini kwa mshangao wa wengi, kwa sasa idadi kubwa ya nyumba hizo zipo mikononi mwa viongozi wengi wastaafu wa Awamu ya Tatu na wengine wa Awamu ya Nne wanaoelekea kustaafu huku, Magufuli akidai kuwa zitajengwa nyumba nyingine maeneo muafaka kama yale ya zamani.

Katika mahojiano, Profesa Safari pia alizungumzia tatizo la udini lililopo nchini kwa sasa, akisema nalo linapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

"Kwenye kikao changu na marehemu Bob Makani pomoja na Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa) tulilizungumzia hili na nikawaomba waliweke kwenye sera za utekelezaji wa chama chetu.

"Suala la udini ni ‘hyper sensitive' na lazima tukubali kuwa udini Tanzania upo! Upo na wala si kwetu tu, hili ni suala la kimataifa na tumelirithi kutoka kwa Wakoloni. Ni lazima tulitafutie ufumbuzi na nina amini CHADEMA italitatua hili," alisema.

Profesa Safari ambaye pia ni mwanazuoni wa Kiisalamu, alivitaja vitabu kadhaa vinavyothibitisha udini nchini na kushauri Tanzania ijifunze kutoka Senegal namna walivyolitatua tatizo hilo na kuiepusha nchi yao kwenda mwelekeo wa Nigeria na nchi nyingine kadhaa.

Source: Rai
 
Alishikishwa mtutu wa bunduki kukubali??!! kama ni hiari yake mwache maadamu anakidhi kama katiba ya nchi inavyomruhusu.
 
Tatizo lipo wapi kijana, umeruka-ruka tu, hata wewe tunakukaribisha ujiunge nasi CHADEMA na wapenda mabadiliko wote tunawakaribisha!
 
Unajua watu wengine wanaonyesha uwezo mdogo sana wa kufikiria. Wanachama wote wapya huwa wanaombwa kuingia kwenye chama fulani, wakati wa kampeni mgombea pia anaomba kupigiwa kura pia, sio kulazimisha ni KUOMBA, hata Obama alikuwa anaomba watu wampigie kura
 
Prof ni habari nyingine kijana, ni watu wenye uwezo wa hali ya juu na kumuomba ajiunge nao sioni kama ni jambo la ajabu.
 
Ndiyo tofauti ya usajili wa real madrid na qpr.unakumbuka jalala mlilowaokota shonza na mwampamba?
 
sioni tatizo chama kumshawishi mtu kujiunga nacho. hiyo ndiyo kazi kuu ya chama cha siasa. kwa mtu mwenye hadhi ya uprofesa kumuomba ndiyo muhimu zaidi. japo mimi sina chama lkn sioni kosa la chdm
 
Ndugu yangu, siasa ndivvyo ilivyo, hata wakati TANU inaanzishwa na wakati wa kupigania uhuru watu maarafu walifuatwa kuombwa kujiunga nacho. Hii siyo ajabu, ingawa ulivyoitoa hapa ni kama kitu cha ajabu kwelikweli. Au una wasiwasi na msimamo wa Prof Safari kwamba anaweza kubadilika ikiwa ataombwa na vyama vingine? Hii nayo ni haki yake.
 
Yawezekana hakukuwa na watu wenye muonekano wa kitaifa ikabidi waanze kuwaomba watu mbalimbali.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuingia kwenye ushabiki wa mkumbo kwa kitu usichokifahamu. Pengine tumia akili ulitakiwa uulize namna gani vyaama vinaweza kupata wanachama wapya.
 
Unajua watu wengine wanaonyesha uwezo mdogo sana wa kufikiria. Wanachama wote wapya huwa wanaombwa kuingia kwenye chama fulani, wakati wa kampeni mgombea pia anaomba kupigiwa kura pia, sio kulazimisha ni KUOMBA, hata Obama alikuwa anaomba watu wampigie kura

Jamaa mleta uzi hana elimu ya uraia hata SIFURI,,, hivi hajui maana ya kuwa na mikutano au operesheni za chama kazi yake ni hiyo ya kuwaomba watanzania kujiunga na chama. Labda kazoea kujiunga na CCM hauombwi bali unanunuliwa kwa hela sasa yeye anashangaa kwa nini Prof alijiunga CHADEMA bila kupewa hela au jamaa amegubikwa na UDINI
 
Hapo alitaka kuBLEND sera yake na sera za cdm sasa kama cdm wasingekuwa tayari kupigania nyumba za serikali zirudishwe ingemaanisha Prof Safari ndoto zake zisingetimia kama anejiunga na cdm. Ndivyo nilivyomuelewa
 
Mimi sijaona tatizo, mleta uzi hata wewe unakaribishwa chadema. Ni. Haki yako kikatiba kwenda cjama upendacho.hata mzee wa tembo kinana aliombwa kuwa katibu wa ccm maana ni haki ya ccm kikatiba kumuomba mtu awe kiongozi au kujiunga nao.so there is no point at all.
 
Alishikishwa mtutu wa bunduki kukubali??!! kama ni hiari yake mwache maadamu anakidhi kama katiba ya nchi inavyomruhusu.

Yaani Professor mzima mpaka aombwe? Inamaana alisoma sera za CHADEMA na hakuzielewa mpaka aombwe? Wasiwasi wangu ni kuwa huyu jamaa hajioni kama mwanaCHADEMA na ndio maana anadiriki kusema 'chama chao' na sio chama chetu.
 
Tatizo lipo wapi kijana, umeruka-ruka tu, hata wewe tunakukaribisha ujiunge nasi CHADEMA na wapenda mabadiliko wote tunawakaribisha!


Mkuu wewe una hatari kubwa sana maana huruhusu akili yako kufanya kazi. Jibu hoja iliyopo mezani. Mimi sipendi mabadiliko, napenda maendeleo maana sio kila mabadiliko ni maendeleo. Napenda sera za CCM japo viongozi wake wengi siwakubali. Napenda watu wachache, almost watatu CHADEMA ila sera zao sizikubali. Vyama vingine hata sioni mwelekeo wake, navipotezea tu. Kwa sababu hiyo naendelea kutokuwa na chama. Nikiwa huru ni rahisi kupima.
 
Back
Top Bottom