Profesa safari amuua kwa risasi mhudumu wa bar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa safari amuua kwa risasi mhudumu wa bar.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NOT FOUND, Apr 8, 2011.

 1. NOT FOUND

  NOT FOUND Senior Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MGANGA wa Kienyeji anayefahamika kwa jina la Bakari Nyalobi ‘Profesa Safari’ [30] anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala, kwa tuhuma za kuua kwa kumpiga risasi kaunta wa Bar ya Luck ya Tabata Mawenzi aliyetambulika kwa jina la Sebastian.

  Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoani Ilala, Bw. Faustine Shilogile alisema kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa jana majira ya saa 7 huko Tabata Kimanga Darajani.

  Alisema mganga huyo alifika katika baa hiyo na kuanza majibishano ya hapa na pale na kaunta huyo na baadae mganga huyo alichomoa bastola yake na kummiminia risasi marehemu maeneo yake ya kifuani.

  Hivyo kufuatia hali hiyo kaunta huyo alianguka chini na wasamaria walitoa taarifa hiyo polisi na kukimbizwa Muhimbili kwa matibabu na alikufa muda mfupi baadae mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo katiia wodi ya Kibasila.

  Hata hivyo uchunguzi juu ya tukio hili bado unaendelea na mtuhumiwa anendela kushikiliwa kusubiriwa hatua za upelelelezi kukamilika ili mtuhumiwa huyo aweze kufikshwa mahakamani.

  Hata hivyo baadhi ya wakazi waishio maeneno hayo walidai kuwa mganga huyo mwenye jina kubwa hapa mjini na hasa hususani maeneo hayo alikuwa akitumia vibaya matumizi ya bastola yake kwa kuwatisha watu pindi tu alipokuwa akimiliki bastola hiyo kihalali

  “tunaomba sheria ifuate mkondo wake” walilalama wakazi wa maeneo hayo

  Wakazi wa maeneo hayo na kwingineko wanaiomba serikali itende haki katika tukio hili ili iwe mfano kwa wengine wanaotumia silaha hizo kinyume na sheria.

  SOURCE CLICK HERE
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hapana ndg zangu issue ni kwamba mganga huyu alikuwa rafiki yake mkubwa na kaunta kilichotokea ni kwamba huyu mganga aliona kimada pale bar akakiendea kumbe kile kimada kina wenyewe. Alipokuwa akiendelea kukisomesha ghafla mwenye kimada akatokea muda huo ni saa nane usiku na ile bar haina kubali kujiendesha kama night club ila tu ni kwasababu mume wa huyo Rukia ni mwenyekiti wa serikali za mitaa. Basi alipotokea yule mwenye mali na kumkuta yule mganga akiimba nyimbo kwa demu wake ukaanza ugomvi. Kaunta alitoka kule kaunta ili amsihi rafiki yake aache kutishia kwa bastola alitokea kwa nyuma akamshika bega mganga akadhani ni miongoni mwa wale wanaotaka kumdhuru kwa sababu ya kimada, akafyatua risasi ya ubavuni akadondoka chini. Mganga mwenyewe akambeba hadi Muhimbili kwa lengo la kuokoa maisha lakini Mungu akampenda zaidi. Mungu ailaze roho ya kaunta mahala pema peponi amina.
   
 3. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kwa hiyo ulikuwepo mkuu?
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Another confussion nikizani yule prof wa Cuf now CDM
  Any way huyo mganga wa kienyeji ana own bunduki?
  Kumekucha TZ
   
 5. majany

  majany JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hebu acha UDAKU...JF SIYO SEHEMU YAKE KABISA....
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  mauaji,ajali,mabomu everywhere..harufu ya damudamu sijui twaenda wapi
   
 7. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mganga wa kienyeji amesomea wap Phd? au ndo kuharibu elimu huku kama Dr. Kikwete, Karume, Prof. Maji marefu nk....? Acha kudharau elimu bw. Watu tunasoma kwa shida na kukamatwa mara kadhaa au kulamba madesa hadi basi
   
 8. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu Isaac mimi niko jirani sana na eneo hili ni usiku huo huo tulizipata zikiwa bado mbichi kabisa.

   
Loading...