YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,909
- 51,904
Nyerere miaka ya 1970 aliwahi kumualika Profesa Mfaransa Rene Dumont mtu aliyebobea kwenye uchumi wa kilimo aliyesifiwa mno kwa uwezo kwenye eneo hilo la uchumi wa kilimo duniani.
Alipofika alitembezwa sehemu mbalimbali vijijini. Wakati huo operation ya vijiji vya ujamaa ndio ilikuwa imepamba moto watu waliondolewa maeneo yao ya asili wakaenda kurundikwa sehemu moja ambayo Nyerere alisema ni kwa ajili ya kuwasaidia watu wapate huduma kirahisi za maji, afya, elimu n.k sehemu moja.
Profesa akampinga kasema alichofanya sio operation vijiji ni operation anzisha miji. Sababu miji yote duniani ilianzishwa kama centre za huduma kama hizo. Akasema maana ya kijiji ni kila nyumba kuzungukwa na mashamba wakati mji ni kila nyumba kuzungukwa na nyumba zingine.
Na ni kweli alichosema vijiji vingi vya operation vijiji sasa hivi ni miji midogo na waliokuwa watoto wa wana vijiji wamegeuka watoto wa mjini kulima hawataki wanafanya kazi tu za mijini za umachinga n.k
Nguvu kazi imepotea ambayo ingeachwa kule kule kijijini tungeendelea kuwa na wana vijiji kibao.