Profesa Ndalichako aongoza viongozi na wananchi wa Dodoma kutoa heshima za mwisho kwa marehemu John Kijazi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,662
Viongozi wa serikali na wananchi wa Dodoma wanatoa heshima za mwisho kumuaga marehemu John Kijazi chuo kikuu UDOM.

Prof Ndalichako ambaye ni waziri wa elimu ndio anaongoza watumishi na wananchi katika tukio hili.

Dr Kijazi (RIP) atazikwa siku ya Jumamosi huko Korogwe, Tanga.

Tukio hili liko mubashara TBC

Maendeleo hayana vyama!

=====

msiba (2).jpeg

WAZIRI Wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewaongoza wakazi wa Jiji la Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi, John Kijazi kwenye hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH).

Akimzungumzia Marehemu Kijazi, Profesa Ndalichako alisema alikuwa ni mtu mpole, mnyenyekevu, mtulivu mchapakazi na mzalendo aliyekuwaanafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria.

Kwa upandewake Katibu Mkuu Ikulu, Moses Kusiluka amesema ibada ya kiserikali ya kumuaga Marehemu Balozi Kijazi itafanyika kesho Jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Karimjee ambapo Rais John Magufuli atawaongoza wakazi wa Dar Es Salaam kuuaga mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho kutwa.

Naye Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM) Profesa Faustine Bee amesema alikuwa anatamani kuendelea kufanya kazi na Balozi Kijazi kwani hata katika changamoto nyingi za chuo hicho walikuwa pamoja katika mapambano ambapo haki ,wajibu na unatawala vilidumu katika kupelekea watanzania kukimbilia chuo kikuu cha Dodoma kusoma na kufanya kazi.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema Marehemu Balozi kijazi katika kipindi cha uhai wake alikuwa mstari wa mbele katika harakati ya serikali kuhamia Dodoma huku Mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika akizungumzia utii wake wakati akipata matibabu hospitalini hapo.

Balozi Kijazi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali hiyo Jijini Dodoma alipokuwa amelazwa kwa matibabu anatarajia kuzikwa Kesho kutwa (jumamosi)nyumbani kwao Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Na ikumbukwe kuwa Marehemu Balozi John Kijazi alikuwa katibu mkuu kiongozi ambapo pia Agost,2020 aliteuliwa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma kutokana na aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho Benjamin William Mkapa kufariki Dunia.
 
... unafiki wa daraja la juu kabisa. Ame-revoke ile barua waliyomtisha nayo VC wa OUT baada ya kuwatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi kuzingatia hatua muhimu za kujikinga na Corona?

Baraza la chuo (maprofesa) nalo likamtaka Profesa Bisanda kuomba radhi kwa kutoa tahadhari ya Corona! Kama tumelogwa vile!
 
Viongozi wa serikali na wananchi wa Dodoma wanatoa heshima za mwisho kumuaga marehemu John Kijazi chuo kikuu UDOM.

Prof Ndalichako ambaye ni waziri wa elimu ndio anaongoza watumishi na wananchi katika tukio hili.
Dr Kijazi rip atazikwa siku ya Jumamosi huko Korogwe Tanga.

Tukio hili liko mubashara TBC

Maendeleo hayana vyama!
Si hakuna corona, eh, ameogopa kuja. Si hakuna corona, mmeishinda kwa sala sasa kwanini asije kumzika rafiki yake wa damu?
 
Viongozi wa serikali na wananchi wa Dodoma wanatoa heshima za mwisho kumuaga marehemu John Kijazi chuo kikuu UDOM.

Prof Ndalichako ambaye ni waziri wa elimu ndio anaongoza watumishi na wananchi katika tukio hili.
Dr Kijazi rip atazikwa siku ya Jumamosi huko Korogwe Tanga.

Tukio hili liko mubashara TBC

Maendeleo hayana vyama!
Najiuliza yule bingwa wa maombi duani nzima yuko wapi?
 
Back
Top Bottom