Profesa Mussa Assad: Natamani mahojiano yangu na Kamati ya Bunge yangewekwa wazi ili watanzania waujue ukweli

Kitu kimoja alichopungukiwa CAG ni HEKIMA na KUNYAMAZA. Ni mropokaji mno.

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.

Unajua ww Misuli umeshazoea kuona viongozi wengine wa taasisi za kimamlaka kama CJ,CDF, IGP, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, kamishna wa TRA wakitii kila kitu cha watawala wa kisiasa mpaka kufumbia macho dhuluma za wazi, kama wanajeshi kutumika kufanya kazi za polisi, Polisi kusimamia wizi wa kura, mahakama zikitumika kubambiakia kesi, TRA ikibambikia kodi huku wakuu wa taasisi hizo wakikaa kimya ambayo ww huita hekima. Ukimya wa viongozi wa taasisi hizo ndio umechangia taasisi hizo za kimamlaka kuwa dhaifu na kutoa mwanya kwa wanasiasa kufanya watakalo.

Leo hii bunge linatumika kupitisha maamuzi kwa jeuri maana wanajua viongozi wa taasisi zote za kimamlaka wanajinyeyekeza kwa wanasiasa hivyo wanaweza kuingia madarakani bila kujali ridhaa ya wananchi. Kwa sasa sio ajabu kuona viongozi wote wa kimamlaka kukusanywa na wanasiasa na kushiriki hata mambo yasiyo na tija. Ilifika mpaka mahali CDF yuko kimya hafla ya kijeshi kupokea wanachama wa ccm huku CDF akiwa kimya ambayo ww ndio unaita hekima! Hiyo inayoitwa hekima kwa viongozi wa taasisi za kimamlaka ndio kumewafanya wanasiasa kugeuza taasisi nyingine kudhalilishwa na wanasiasa kwa Hadaa ya uzalendo. Huyo CAG amegoma kujipendekeza kwa wanasiasa wetu ndio umebaki kusema eti hana hekima. Hekima ya kumtaka apike data hiyo ni hekima au wendawazimu?
 
Proffessor vip tena...naamin una mpunga wa kutosha na uzee umeenda sana .kama vip jikate tuliunge mtaani, tuanze kukimbizan na TRA, tatizo lenu mmezoea kazi za ofisi na kukalisha vitambi kwenye viti vya kuzunguka, alaf hujajua kuwa aliyekuajir ni mwanasiasa na lazima atakupelekesha tuu utake ustake, na wewe ndo utakayeumia....Muulize shetani baada ya kukosana na mwajir wake nini kilimpata..mpaka leo tuko naye tandahimba huku
Big no Prof wala asibow ati asalimu kwa kuachia ngazi. Kinachomweka offisini sio njaa, bali uzalendo kwa nchi yake. Nyie mnaojifanya kumponda ndio wale wale wezi pamoja na mawakala wenu wazee wa kugonga meza. Mlitegemea mkimbagaza atajitoa, sasa imebackfire he is staying. Soon tutasikia maandamano kutoka Lumumba ya kupongeza bunge maana hamkawii nyie.
 
Ndomana wenzio wamekufa ktk mwenge kwa akili kama zako
Mwendawazimu ni wewe Bosi wa CAG ni bunge maana ndilo linalomtuma kazi,Rais anateua tu CAG,, Bunge linasimamia serikali ambayo inakuwa audited na CAG,ripoti anakabidhiwa rais(serikali) ili ikabidhi kwa mamlaka inayoisimamia( bunge)
Ila kwa hili assad kaingia kwenye 18 hachomoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuna CAG up to now...kiti kipo wazi...hatuwez kuwa na CAG mropokaji, anashambulia mhimili wa bunge kweny media alaf wajinga fulani wanapiga makofi....kwa nin ashambulie only bunge? ina mana sehemu zingine ni dhabiti ispokuwa bunge? vip kuhusu mahakama.. kiufupi tu huyo anatakiwa afukuzwe kazi

Embu kwendeni huko. Hatuogopi tena. Kadri siku ziendavyo ndio tunapata ujasiri.
 
Bunge halikosoi taarifa ya CAG; hukosoa hao waliotumia fedha za umma tofauti na ilivyokusudiwa na kupelekea taarifa ya CAG iwe hivyo ilivyo. Kwa taarifa yako hao siyo wengine bali ni serikali. Haijapata kutokea serikali kuwa na kinyongo na CAG kwa sababu kazi yake ni "noble". Kazi ya kulinda fedha na rasilmali za watu wanyonge ni takatifu. Mtu mwenye dhamira njema na unyenyekevu wa moyo hawezi kuwa na kinyongo na mtu mwenye dhamana hiyo hasa anapoonekana kufanya hiyo kazi kwa uzalendo na utaalam mkubwa. Tatizo lililopo mbele yetu sasa ni kwamba tunayo serikali ambayo inaamini haikosei na mamlaka yake hata kwenye matumizi ya fedha za umma haina mipaka! Incredible!

Yani hawa watu hawa. Kama mambumbumbu
 
Jinsi muhimili wa dola unavyocontrol mihimili mingine, ukweli ni huu. Maamuzi ya bunge ni maamuzi ya CCM, na ni maamuzi ya serikali.
Hivyo, huu uamuzi wa hovyo utakuwa na baraka zote za CCM na Serikali. Kwa uamuzi kama huu utaitofautishaje, serikali, CCM na ufisadi!
 
Wewe ndo hujui. CAG kaajiriwa na wanasiasa ndio maana ripoti yake anawapelekea wanasiasa ili waijadili na kuwaagiza mawaziri wafanyie kazi. Kwa taarifa yako tu hao wanasiasa hawamuamini hata huyo CAG mwenyewe ndio maana wao darasa la saba wanajadiri taarifa ya CAG msomi na kuikosoa kabla hawajamuagiza waziri afanyie kazi.
Mawazo yako sawa kabisa na wale KK! Tulidhani ni KKK, kumbe hata ile ya kuhesabu nasikia kwao si lazima!
 
CAG ameliita Bunge dhaifu bila kutaja wapi na lini ni dhaifu na wapi na lini sio dhaifu, hakusema udhaifu wa Bunge ulianzia lini na awamu ipi na spika yupi. Kwa ujumla alipaswa kutaja kile tu ambacho Bunge kilionyesha udhaifu na sio udhaifu wa ujumlajumla kama vile alivyoliita yeye.

Lakini Bunge nalo haliamini kuwa lina udhaifu wowote pahala popote ingawa tunaona yako mambo ambayo hayaendi vizuri nchini ingawa yaliamuliwa na kupitishwa na Bunge letu tukufu. Mfano ni baadhi ya sheria zinazopingwa mahakamani na kushindwa, mikaba mibovu ya madini isiyojadiliwa bungeni, sheria mbovu za madini, nk. Bunge limekasirika sana kuitwa hivyo hadi kukataa kufanya kazi na CAG ikimaanisha kuwa kazi ya ukaguzi wa matumizi ya fedha za nchi yasifanyike au yasubiri CAG mgeni kabisa ateuliwe ambaye bila shaka ni atakayekuwa na hofu ya kulinyooshea kidole Bunge kwa kuogopa kilichompata mtangulizi wake. Bunge linajenga hofu kwa ma CAG wasifanye kazi zao. Bunge kushindwa ku address mapendekezo ya CAG bila kutoa sababu yoyote ya kushindwa kuchukua hatua sio udhaifu?

Nani Yuko sahihi kwenye sakata lao?
 
Hata woga kupitiliza na kuona kila wazo mbadala linastahili kupingwa na kufikiria adhabu kwa aliyelitoa ni Udhaifu mkubwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani kiongozi anahitaji kutafakali sana kabla ya kuhumu. Hasira na hamaki sio dalili ya kiongozi bora. Ukikasirika na kuhamaki unawesa kushitukia umempiga mtu fimbo ya kichwa na kusababisha kifo Kwa vitu hata vya kawaida tu
 
Wahuni wanalipwa tens of millions halafu wanasusa kufanya their primary job eti kisa wamesemwa vibaya?

Hawa jamaa wamechoka kuchezea mshahara sasa wanachezea kazi
 
Ukiona spika anatangaza madeni ya wabunge wenzake basi ujue spika huyo ana matatizo ya kiakili hivyo ni dhaifu kabisaaa!
 
Back
Top Bottom