Profesa Muhongo ni muongo, analea ufisadi!!!!!!!!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
22,378
19,213
Kitendo cha Profesa Muhongo kutetea wezi wa fedha za umma, waliotafuna zaidi ya Tsh bilioni 200 kupitia ufisadi wa IPTL na ESCROW, kimewashangaza watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kikabila au kikanda. Haiingii akilini kuona Profesa anayejidai kuwa msomi kuliko wasomi wote nchini Tanzania asimame kidete kuwatetea mafisadi huku nchi ikiendelea kuwa kizani kwa kukosa umeme wa uhakika na kushindwa kufikisha umeme maeneo ya vijijini licha ya kuwa watanzania hukamuliwa fedha nyingi kila kukicha na kuingizwa kwenye kichaka cha mafisadi (REA) ambao hufisadi fedha hizo bila kufikisha huduma za umeme kwa walengwa (wananchi wa vijijini).

Kibaya zaidi ni kwamba Muhongo na watu wake wamefikia hatua mbaya ya kumtisha balozi kutoka nchi ya wahisani anayehoji ufisadi wa fedha za umma ambao hutolewa kama sadaka na nchi yake anayoiwakilisha hapa Tanzania. Tutambue kwamba bajeti ya nchi yetu hutegemea zaidi ya 40% ya misaada kwa wahisani. Hii maana yake ni kwamba kitendo cha Muhongo & Co kupanua midomo yao mipana kumkemea balozi anayehoji utafunwaji wa fedha wananchi wa Tanzania ni sawa na mbwa kumkata mikono mmiliki wake anayemlisha kila siku! Ndiyo. Hata kama kuna watu hawatapendezwa na mfano huu lakini hii ndio hali halisi.

Kutamba kwamba Tanzania ni nchi huru kisa balozi kaingilia kati vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na makada wa chama na serikali yake hakiondoi ukweli kwamba bado nchi yetu haiko huru na haijawahi kuwa huru. Hivi ni kweli kwamba Tanzania ni nchi HURU? Uhuru huo tuliupata lini wakati kila siku mkuu wa kaya yu kiguu na njia kuombaomba misaada kwa hao wazungu wanaowachimba mkwara? Ushadi kwamba nchi yetu haiko huru uko wazi kabisa. Waziri Membe alitudhihirishia hilo wakati anatetea safari nyingi za mkuu wa kaya nje ya nchi—kwamba bila kufanya safari za kuombaomba fedha za misaada nchi itakosa fedha za kulipa mishahara, kujenga barabara, na kuendeshea serikali pamoja na miradi mbali mbali za maendeleo. Sasa huo uhuru wetu uko wapi?

Hivi hao wahisani ambao wanachokozwa wakigoma kutupa misaada si tutakula kinyesi? Jamani muambieni Muhongo & Co waache kudhalilisha wahisani wetu mintarafu ya kuficha vitendo vyao vya kifisadi. Elewa kwamba nchi hii ikinyimwa misaada hatuwezi kula usomi wa Muhongo. Sote tutakufa njaa bila kujali itikadi zetu za vyma, dini, kabila dini, nk. Tuache kumtukana mamba kabla hatujavuka mto.

Nawasilisha.
 
uliyoongea yote tunayajua,huna jipya unajaza server tu...mods unganisha huu uzi na nyingine nyingi!

Kuna hujui jambo bora ukae kimya! Acha kutetea ufisadi wakati watanzania wakizidi kutopea kwenye umasikini.
 
Anayepika majungu dhidi ya muhongo ni mwizi wa rasilimali za taifa letu
 
Wewe ni kibaraka wa mengi? Unachumia tumbo?

Mengi anaigiaje kwenye ufisadi wa IPTL, Richmond, EPA, Meremeta, Deep Green Finance, Kagoda na ESCROW? Usifikiri kwa kutumia tumbo lilojaa mataputapu uliyokunywa kwa kutumia mgao wa fedha za ufisadi--tumia kichwa, mkuu.
 
Ndani ya ccm kila mtu anautetea ufisadi kwa nafasi yake na sehemu yake!

Yaani haya ni majanga. Ukiona nchi ambayo mafisadi huabudiwa kama Mungu, ujue kwamba taifa hilo ni mfu! Serikali dhaifu na ya kifisadi ya CCM ndio iliyotufikisha hapa.
 
Yaani haya ni majanga. Ukiona nchi ambayo mafisadi huabudiwa kama Mungu, ujue kwamba taifa hilo ni mfu! Serikali dhaifu na ya kifisadi ya CCM ndio iliyotufikisha hapa.

tpaul kama hujui kitu ni kukaa kimya.. Amri ya mahakama kuu ni kuwa 200b za SCROW accnt apewe mwenye hela yake Mmiliki wa sasa wa IPTL, njooni na ushahidi, mmiliki alipewa au la? Mahakama ilikosea? ukisema watu wameiba wanaiba kupitia mahakama? kwa nini haikatwi rufaa?
 
Hivi kama ni Serikali Makini inafanyeje biashara na Singa Singa alieiba dola 600mln kwa kushrikiana na mtoto wa raisi??!! Au ndio amekuja kushirikiana na mtoto wa raisi na mawaziri kuiba Tanzania na 200bln ni mwazo tu??!!

Msilete upuuzi wa kutetea ushenzi unaoangamiza,mshaambiwa IPTL walidanganya hata mtaji,kampuni inawekeza dola 50 halafu serikali na makuwadi mnatetea??!!!

Wakina Rugemalira na wakuu wanagawana 200bln huku wakisema ni hela za ugoro(sijui za kuku choma ni trillion ngapi),serikali mnaangalia tu na kutetea na vimada wenu??!!

Uingereza kupitia balozi ambao ni wafadhili wa bajetti na mradi wa REA wanaohoji wizi huo,mnasema wanafanya ushushu na wamehonga watu,hui nchi una viongozi makini au wezi walilaaniwa,mavi wanasema ni pilau??!!
 
Serikali haifanyi biashara na Singasinga. Serikali inafanya biashara na Kampuni inayozalisha umeme, Inanunua umeme sababu tunauhitaji. Kama ni wizi kamuibia nani? kwanini aliyeibiwa hamfungulii mashtaka. Ridhiwani yupo bungeni kwanini hahojiwi? kupitia kinga ya mbunge walizoea kumsingizia, wamemubambikia utajiri wa ajabu nae kaingia mjengoni wameufyata.
 
Serikali haifanyi biashara na Singasinga. Serikali inafanya biashara na Kampuni inayozalisha umeme, Inanunua umeme sababu tunauhitaji. Kama ni wizi kamuibia nani? kwanini aliyeibiwa hamfungulii mashtaka. Ridhiwani yupo bungeni kwanini hahojiwi? kupitia kinga ya mbunge walizoea kumsingizia, wamemubambikia utajiri wa ajabu nae kaingia mjengoni wameufyata.

Wacha kutetea ushenzi,mkataba wa IPTL ulikua kuzalisha umeme wa dharula kwa mda wa miaka 20 (sijui dharula gani ya miaka 20)) ila kwenye mkataba waliandikishiana baada ya mkataba Tanesco atakuwa mmiliki wa mitambo pasipo kuinunua tena,mkataba unaisha mwakani (2015) kampuni na mitambo eti vimeuzwa??!!!

Sasa kama wewe sio mpumb@vu unaetetea washenzi sema hapo
 
Siku tukiondokana na serikali hii dhaifu ya CCM ndipo tutakapoanza kupata maendeleo. Ufisadi umetanda tangu magogoni hadi kwa balozi wa nyumba kumi kule kijijini Mchambawima. Rais aliwabembeleza wezi wa EPA wamrejeshee fedha za umma walizokwiba---wakaitika na kumpelekea hizo fedha na akaachiwa huru warudi mtaani waendelee kuiba tena! Rais akachukua zile fedha za umma alizopewa na mafisadi akazitia mfukoni mwake!

Lakini pia Rais kasema anawafahamu wauza unga kwa majina lakini mpaka leo hakuwahi kuwataja. Jamani, ni nchi gani hii ya kizezeta hivi?

This kind of stupidity can only happen in Tanzania.
 
Back
Top Bottom