Profesa Muhongo Aichana Mikataba ya IPTL, Songas na Agreco, Asema Haina Tija Yoyote kwa Taifa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Sunday, May 22, 2016
Profesa Muhongo Aichana Mikataba ya IPTL, Songas na Agreco,Asema Haina Tija Yoyote kwa Taifa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mikataba yote ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni za kufua umeme siyo mizuri na haina manufaa yoyote kwa Taifa.
Profesa Muhongo alisema hayo juzi wakati akijibu hoja ya kuongezeka kwa deni la Tanesco iliyotolewa na Msemaji wa Kambi ya Upinzani katika wizara hiyo, John Mnyika.
Kambi ya upinzani imekuwa ikisema mikataba ya Tanesco haina tija kwa Taifa na imekuwa ikiliua shirika hilo. Katika hotuba yake, Mnyika alisema Tanesco imekuwa ikiilipa IPTL Sh300 milioni kwa siku kama gharama za uendeshaji.
Profesa Muhongo alikiri kwamba ni kweli deni la Tanesco ni kubwa na limesababishwa na uongozi dhaifu, rushwa, wizi na mikataba mibovu ambayo Tanesco imeingia.
Alisisitiza kwamba hakuna mkataba unaolinufaisha Taifa.
“Lazima niseme ukweli, mikataba yote ya Tanesco siyo mizuri. Tumekuwa tukiwalipa Songas gharama za uendeshaji Dola 4.6 milioni; IPTL tunawalipa Dola 2.6 milioni; Agreco tunawalipa Dola 2.0 milioni. Hakuna mkataba wenye manufaa kwa Taifa,” alisema Profesa Muhongo na kuahidi kwamba wizara yake itachukua hatua ili kulinusuru shirika hilo na mzigo huo wa madeni kila mwezi.
Alisema wizara yake imeanza utaratibu wa kufanya tathmini ya utendaji wa wafanyakazi wa Tanesco ili kuhakikisha wanatoa huduma bora.

Alisema tathmini hiyo inafanywa kwa mameneja wa Tanesco kwa kuangalia wameingiza kiasi gani na wameunganisha wateja wangapi.
“Kila baada ya miezi mitatu tunafanya tathmini ya mameneja wetu na mwezi wa sita tutafanya tathmini ya pili. Wapo ambao walishindwa kukidhi vigezo katika tathmini iliyopita, wameondolewa,” alisema waziri huyo.
Kuhusu suala la umeme vijijini, Profesa Muhongo alisema Hazina imetoa Sh70.2 bilioni kwa ajili ya kumalizia utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa umeme vijijini, unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (Rea).
Jambo hili lililalamikiwa na wabunge wengi wakisema wakala huyo anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu fedha zake hazitolewi na Serikali.

Walishauri fedha za Rea ziwekwe katika akaunti yake maalumu bila kupitia Hazina. Hata hivyo, Profesa Muhongo alilihakikishia Bunge kwamba miradi yote iliyobaki katika awamu ya pili ya Rea itakamilika kufikia mwisho wa mwezi ujao.
Alisema miradi ya Rea haitatetereka kwa sababu ya Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC) kusitisha kutoa misaada kwa Tanzania akisema Serikali imejipanga kusimamia miradi ya maendeleo bila kutegemea misaada ya wahisani.
“Tumeanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta (Pura). Wakala huyu atakuwa na jukumu la kusimamia mikataba yote ya mafuta na atasimamia pia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),” alisema Profesa Muhongo.
Kuhusu suala la migodi kutolipa kodi, waziri huyo alisema ni kweli mingi hailipi na kusema ameanza kusimamia suala hilo na kuwa wote lazima walipe kodi.
Alisema Serikali pia itawalipa fidia wakazi wa Lindi katika eneo ambalo kitajengwa kiwanda cha kupakia gesi (LNG). Alisema fedha zipo na vijana wakasome Veta ili wapate ajira katika kiwanda hicho.
 
Hapa kazi tu, sijawahi kuwa dissappointed na huyu Professor, ktk maprofessor waliopo madarakani nafikiri ndo anayeitendea haki kiufasaha zaidi fani yake!!
JEMBE!!
 
muhongo awache porojo. tunachotaka kusikia ni kusitishwa mikataba ya kinyonyaji/wizi yote. ufundi wa kisheria uliotumika kuwela mikataba hiyo ya kinyonyaji/wizi ndio utumike kuisitisha. sio uhuni halafu tunapelekwa mahakani kudaiwa mamilioni. hao wanasheria mafundi wa wizi uwezo wa kunasua wanao vinginevyo nguvu ya umma itumike kuwahukumu wahusika wote. tuko nyuma yako jpm.
 
Nafikiri wangesema "aichana mikataba" kuliko kusema aichana mikataba!
Tofauti ya maneno uliyoandika iko wapi?

Hiyo mikataba wangeweza kufuta kabisa tungepata nafuu sana.

Nadhani wanaonufaika na mikataba hiyo ni chanzo hata ya Magu kushindwa kugusa Tanesco kwenye utumbuaji maana jipu lake ni kubwa sana

Kama leo ndipo wanakuballi hiyo mikataba ni mibovu basi nimeamini pia CCM ni slow learner ndo maana maendeleo ya nchi yetu yana kasi ya kinyonga.
 
Huyu si ndiyo aliyekuwa anatetea Escrow ya IPTL bungeni.
Hawa watu bana unafiki umewazidi sasa, maazimio yake yalishafikiwa na bunge Rais Mwema akamrudisha unafiki.com
 
Mi-CCM eti leo ndio inakiri huu uozo!That is why i hate CCM.Wapinzani wamewabeza kwa kupinga hii mikataba alafu leo ndio yanajidai kushituka na kuna mijitu iliyokuwa inaunga mkono misimamo ya serikali kutetea hii mikataba hii ila kwasababu leo serikali imekiri kuwepo kwa uozo huu wa mikataba,basi na yenyewe leo yatajitokeza hapa mtandaoni na kwenye media kuipongeza serikali.Ovyo kabisa hawa watu.
 
Tofauti ya maneno uliyoandika iko wapi?

Hiyo mikataba wangeweza kufuta kabisa tungepata nafuu sana.

Nadhani wanaonufaika na mikataba hiyo ni chanzo hata ya Magu kushindwa kugusa Tanesco kwenye utumbuaji maana jipu lake ni kubwa sana
Kuna tofauti kubwa sana hapo!! Hata ktk magazeti, ukiona kitu/ kichwa cha habari kimeandikwa na kuwekewa " ", jiulize maswali ya ziada!
 
Mi-CCM eti leo ndio inakiri huu uozo!That is why i hate CCM.Wapinzani wamewabeza alafu leo yanajidai kugeuga na kuna mijitu iliyokuwa inawasifia na yenyewe leo itawapongeza.Ovyo kabisa hawa watu.
Hivi wewe si mama Regina kweli?? Hii uturn yako baada ya mzee kuhamia chadema ni hatari.
 
Kama waziri hapaswi kuilalamikia mikataba mibovu,huu ni udhaifu wa kiwango cha juu kiutendaji.Muhongo ajipime kama bado ana uhalali wa kuwa waziri mwenye dhamana ya nishati na madini.
 
Back
Top Bottom