Profesa Muhongo aiagiza TANESCO kutokata umeme bila sababu za msingi

unanitaka

JF-Expert Member
Oct 7, 2014
2,178
1,045
Aagiza umeme kutokatika tena!!!!

Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha mara moja tabia ya kukata umeme bila sababu ya msingi.

Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walipofanya ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara hiyo.

Mara tu baada ya kuapishwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake, Dkt Medard Kalemani walifanya ziara hiyo ya kushtukiza kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo.

Profesa Muhongo alisema wananchi wamechoshwa na tabia ya shirika hilo ya kukatakata umeme bila kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.

Haiwezekani kila mwaka matatizo ni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hili halikubaliki na halivumiliki. Ninataka tutengeneze historia ya kutatua matatizo ya umeme nchini. Umeme ukiendelea kukatikakatika lazima muondoke,? alisema Profesa Muhongo.

Alisema wananchi wanahitaji umeme wa bei nafuu ili waweze kujikwamua na umasikini huku akieleza kwamba ni wakati mwafaka suala hilo likatazamwa kwani bei ya huduma ya umeme ikishuka bidhaa nyingine pia zitashuka.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwataka watendaji hao kujieleza ni kwanini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwataka waeleze wao kama Menejimenti ya Shirika hilo ni hatua zipi ambazo tayari wamezichukua kuhakikisha hali hiyo haijirudii.

Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na hivyo inatakiwa kuwa na umeme wa uhakika.

Vilevile aliwataka waeleze ni kwa nini huwa wanachelewa kufika maeneo ambayo kumetokea hitilafu hali yakuwa wananchi wanatoa taarifa mara tu wanavyoona hitilafu husika.

Huduma zenu haziridhishi, unakuta transfoma imeharibika ama nguzo imeanguka na taarifa mnaletewa niambieni ni kwanini huwa hamfiki kwa wakati,? alihoji Profesa Muhongo huku akiwasisitiza wabadilike.

Profesa Muhongo alisema tangu ametangazwa amepokea simu nyingi kutoka kwa Watanzania wakisikitishwa na hali ya umeme nchini. ?Nimepokea simu kwa wananchi wa mikoa mbalimbali nchini hususan Arusha na Mwanza wakinilalamikia kuhusu kukosekana kwa huduma ya umeme kwenye mikoa hiyo. Nataka leo hii mnipe jibu tatizo ni nini,? alihoji Profesa Muhongo.

Alisema ni wakati sasa viongozi hao wawe wabunifu vinginevyo Serikali haiwezi kuwaelewa kwani kila kukicha tatizo la umeme linaonekana kuendelea kuwa palepale.

Kwa miaka yote mliyofanya kazi hapa Tanesco naona mmeshindwa kubuni mbinu zitakazolipeleka shirika kule ambapo wananchi wanataka. Ninawaagiza kujitathmini kama kweli mnafaa kuendelea na majukumu yenu,? alisema Muhongo.

Alisema wananchi wamechoka kusikiliza maneno bila kuona vitendo na hivyo kuwaagiza kuhakikisha wanabadilika haraka iwezekanavyo kabla Serikali haijachukua hatua zingine.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alisema kazi kubwa ya shirika hilo ni kuwapelekea wananchi huduma ya umeme na si vinginevyo.

Alisema ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imebainisha lengo la Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapelekewa huduma ya umeme na sio ahadi na maneno yasiyokuwa na tija.

Aliwaagiza kuhakikisha katika utendaji wao wanazingatia masuala makuu manne ambayo aliyaelezea kuwa ni maadili, uadilifu, uwajibikaji na kuzingatia taaluma badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

Akizungumzia suala la wizi wa umeme, Dkt Kalemani alisema watumishi wasio waadilifu wa shirika hilo nao wanahusika kwa namna moja ama nyingine na hivyo kuwaagiza watendaji hao kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa mapema iwezekanavyo.

Tubadilike, tutafsiri mipango yetu kwa vitendo, tupange na tutekeleze. Hakuna muda wa kuendelea kuzungumza mipango bila utekelezaji. Wananchi wanahitaji kuona utekelezaji unafanyika,? alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba aliwapongeza viongozi hao kwa kuteuliwa kwao na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kutatua changamoto mbalimbali.

Tumefurahi na ute
 
muhongo lazima amalizie alipoaacha,, lazima aivunje tanesco na kuigawa mashirika madogo madogo ianze upyaaaaa....


shirika kubwaaa wafanyakazi 6000 lakini bado linasua sua,,,
 
Hadi yeye kuwa Prof sidhani kama wanafunzi hawaku-disco, hivyo lazima pia kutokuwa perfectionists katika kila jambo. Nchi yetu bado ni changa na yenye miundo mbinu chakavu katika kila sekta. Hali sikubaliani na tatizo la kukatikakatika kwa umeme muda mwingi lakini sikubaliani na hali ya kufikiria kuwa Tz inayotegemea umeme wa maji na mabadiliko ya tabia ya nchi kuwa tutakuwa salama. Nilitarajia kusikia akisema mikakati ya kisera mipya ya kuongeza umeme toka vyanzo vingine mbadala maana ni taaluma yake pia. We should not exaggerate 'hapa kazi' na kuwa hapa 'udikteta' hata pale suala si professional.
 
Mhongo ni "tingatinga2". Tunakuaminia. Vunja Tanesco kwa kuunda makampuni mawili tofauti. Uzalishaji na usambazaji. Imarisha mifumo ya usambazaji umeme vijijini.Shusha bei ya umeme.Hakikisha umeme haukatiki hovyo.
 
Alikuwa pale na alibadilisha mambo lakini fitina za mengi nz zito zikamuondoa wakati alieagiza mzigo utoke alikuwa mzee wa msoga.ilikuwa dhambi kumdhalilisha prof wakati muhusika ni ikulu,bot na mwanashera mkuu wa serikali
 
Wawape hela za gesi na mafuta!

Mpwa haya maigizo tumeyachoka sasa. Hivi wanatuonaje hawa jamaa? Mie nimerudi home naambiwa kitoweo cha wiki nzima kimeoza kwenye friji kwa hiyo kama nahitaji supu asubuhi nikatafute nitakapo jua, kweli hiyo ni sawa?
 
Kwa kweli baada ya Prof Muhongo kuondoka, huduma ya upatikanaji wa umeme ilizorota, naamini sasa Tanesco watabadilika, na kurudi kwa Prof Muhongo mambo yataboreka.

Vv
 
Mpwa haya maigizo tumeyachoka sasa. Hivi wanatuonaje hawa jamaa? Mie nimerudi home naambiwa kitoweo cha wiki nzima kimeoza kwenye friji kwa hiyo kama nahitaji supu asubuhi nikatafute nitakapo jua, kweli hiyo ni sawa?
Wanatufanya hatuna kumbukumbu kama watoto wanavyodanganywa ntakununulia pipi!
 
Mhongo ni "tingatinga2". Tunakuaminia. Vunja Tanesco kwa kuunda makampuni mawili tofauti. Uzalishaji na usambazaji. Imarisha mifumo ya usambazaji umeme vijijini.Shusha bei ya umeme.Hakikisha umeme haukatiki hovyo.

Sera ya uwekezaji si IPO?
Karibisha wawekezaji ktk sekta hiyo kwa kuwapa masharti nafuu kuwe na ushindani.
Nini tatizooo.
Mbona mawasiliano mmeuwa TTCL au Tanesco hamna share?
 
Safi sana, tunahitaji kazi ifanyike siyo ngonjera kila siku
 
Back
Top Bottom