Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
Naye aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alisema ameridhishwa na uamuzi wa rais kumuacha nje ya baraza hilo.
Nimeridhika kabisa na maamuzi aliyochukua Rais Kikwete, naamini maamuzi yake yamezingatia vigezo katika uteuzi sina cha kuongeza zaidi ya kuwatakia kila la heri katika utendaji wao wa kazi za kila siku, alisema Profesa Msolla.
Alisema moja ya rai anayowapa mawaziri wapya ni kuwataka watimize maratajio ya wananchi ambao wanaonekana kuwa na shauku ya maendeleo.
Nimefanya kazi yangu kwa ubunifu mkubwa, nategemea hata kama wakihitaji maoni yangu niko tayari kushirikiana nao, alisema Profesa Msolla.