#COVID19 #COVID19 NIMR: Chanjo zitakazotolewa Nchini ziko salama kwa asilimia 99.9

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Baada ya ufafanuzi mzuri wa kisayansi uliotolewa na Mkurugenzi mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya kupitia Clouds tv sitashangaa kumuona Askofu Gwajima akibadili mawazo na kutimba Ikulu kupata chanjo hapo kesho.

Prof Yunus Mgaya amesema chanjo ya Johnson & Johson inaweza kuwaathiri watu 4 tu katika kila watu 1,000,000 hivyo usalama wake ni wa uhakika.

Prof Mgaya amesema anatamani angekuwa miongoni mwa watu watano wa kwanza watakaochanjwa kesho.

----
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imesema ipo kwenye mchakato wa kutengeneza chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid- 19.

Aidha, NIMR ilisema jana kuwa chanjo zitakazotolewa nchini dhidi ya ugonjwa huo ni salama kwa asilimia 99.99 na zimethibitishwa na na jopo la wanasayansi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Yunus Mgaya alisema hayo jana wakati akijibu swali kama Tanzania ina mpango wa kutengeneza chanjo yake dhidi ya corona.

Dk Mgaya alikuwa akizungumza kwenye Kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds kinachomilikiwa na Kampuni ya Clouds Media Group.

“Ndio Tanzania tunao mpango wa kuja na chanjo yetu ya corona. Rais Samia Suluhu Hassan alishasema na Katibu Mkuu akazungumzia hilo pia na sisi NIMR tukapewa jukumu,” alisema Dk Mgaya.

Alisema kutokana na maagizo hayo, tayari NIMR iko kwenye mchakato utakaoifikisha kwenye utafiti wa chanjo yake.

“Nasema Inshallah Mungu akipenda, tunaweza tukawa na chanjo yetu Tanzania ya ugonjwa huu na magonjwa mengine,” alisema Dk Mgaya.

Alisema Covid 19 ilivyoingia na kusambaa dunia nzima wanasayansi waliona hakuna namna ya kuudhibiti ugonjwa huo kwa kuwa hauna dawa hivyo mkazo uliwekwa kwenye chanjo.

Dk Mgaya alisema na hadi jana kulikuwa na chanjo zaidi ya 200 duniani zilizokuwa kwenye majaribio, lakini zilizopitishwa na WHO zitumike chini ya mpango wa dharura ziko sita.

Alitaja chanjo hizo kuwa ni nne kutoka Marekani ambazo ni BioNTech, Pfizer, Johnson & Johnson na Moderna NIAID, Novavax ya Uingereza, AstraZeneca ya Sweden na China ziko mbili; Sinovac-CoronaVac na Sinopharm.

Aidha, alisema chanjo ya Urusi ya Sputnik V ambayo pamoja na kwamba imeshaanza kutumika kwenye nchi nyingi duniani, bado inafanyiwa tathmini na WHO huku Cuba ikitengeneza chanjo inayoitwa Abdala.

Alisema chanjo hupitishwa zitumike baada utafiti na mamlaka mbalimbali kujiridhisha ziko salama kwa matumizi.

“Mfano chanjo inatengenezwa Marekani ni lazima ipitiwe na udhibiti wa mamlaka za Marekani pia lazima WHO iidhinishe. WHO ina kamati zake za kitaalamu zinazokagua mpaka kujiridhisha kitaalamu na kubwa zaidi huangalia usalama na ufanisi,” alisema mtendaji huyo wa NIMR.

Alisema chanjo sita zilizopitishwa na WHO zimefaa, haziwezi kumdhuru mtu kwamba akinywa atakufa au kuugua na kwamba kiwango cha athari ni kidogo mno kinachofikia asilimia 0.00004.

Dk Mgaya alisema manufaa ya chanjo za corona ni pamoja na kupunguza vifo, kuzuia watu kulazwa hospitalini, kupunguza makali ya ugonjwa na maambukizi.

Habarileo
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.

Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.
 
CCM kama wana akili ya kumjeruhi kisiasa na kiheshima Askofu Gwajima, inatakiwa wawalazimishe mawaziri na wabunge wote wachomwe chanjo za Covid hadharani ili iwe hamasa kwa wananchi.

Na wa mwanzo kabisa kuchomwa chanjo awe "ASKOFU GWAJIMA" huku camera zikimchukua kwa ukaribu. Halafu vyombo vya habari apate airtime ya kutosha usiku kwenye habari kwa kuoneshwa akichoma chanjo (Clip Yake Irudiwe Hata Mara 6). Halafu Kesho yake magazeti yote yaweke picha zake ukurasa wa mbele sindano ikiingia begani.

Kwenye mitandao wamuachie hio kazi Da Mange. Sijui ataweka sura yake wapi siku ya pili watavyo mzodoa. Hajui siasa chafu huyu rashidi.
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.
Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.
Elimu haina mwisho bwashee!
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.
Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.

Ndio wasomi waliotumika kupigia mstari theory za Mwendazake kuhusu corona. Leo wamebadirika nao.
 
Back
Top Bottom