Zanzibar 2020 Profesa Mbarawa atapita Zanzibar kwa zaidi ya 80%

mwana wa mtemi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
374
250
Wakuu baada ya Mwalim Seif kutangaza nia ya kuwania Urais Zanzibar, ni dhahiri shahiri Profesa Mbarawa atapita kwa kishindo kikubwa! Prof amezidi kuipaisha nyota yake katika utendaji wenye mafanikio makubwa kwa Wizara alizosimamia zenye kuhudumia Watanzania zaidi ya 58+ Million!

Kwa Zanzibar msingi alioujenga Dkt Shein hakika umepata mjenzi wa kuta zake!

Tusubiri mchakato upite salama!
 

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
27,204
2,000
Wakuu baada ya Mwalim Seif kutangaza nia ya kuwania Urais Zanzibar, nidhahiri shahiri Prof Mbarawa atapita kwa kishindo kikubwa! Prof amezidi kuipaisha nyota yake katika utendaji wenye mafanikio makubwa kwa Wizara alizosimamia zenye kuhudumia Watanzania zaidi ya 58+ Million!

Kwa Zanzibar msingi alioujenga Dr Shein hakika umepata mjenzi wa kuta zake!

Tusubiri mchakato upite salama!
Si mpeni huyo kibaraka wenu hiyo Tanganyika aiongoze kama mnamwona ni mzuri?
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,553
2,000
Maalim atashinda kwa kishindo na wizi wa kura utakua ni historia ya zamani. Siasa za kilaghai na kihuni ndizo zilizoifikisha hii nchi hapa .

Demokrasia iliheshimiwa hata viongozi watakua na Uzalendo.

CCM Zanzibar haijawahi kukubalika. Na awamu hii wazanzibari wote bila kujali vyama wanataka wachague Rais wao wenyewe na sio Rais wa mtu mmoja. Tuwaache wazanzibar wote bila ubaguzi wafurahie nchi yao wasiishi kama wakimbizi.

CCM iache uroho wakubali tu kushika umakamu wa Rais ili amani itawale Zanzibar. Mbona mnangangania Urais tu ili muteuane na kurithishana madaraka. Acheni ubinafsi wanaCCM.

Bila haki uongozi wenu hauna furaha zaidi ya kujifariji na kuishi kwa hofu na laana na chuki kuongezeka. Miaka 25 sasa kama CCM haijaweza kuweka mazingira mazuri ya kuachia madaraka kwa wapinzani utakua ni uhuni na kujilisha upepo kikinuka wakulaumiwa ni wao wenyewe mana suoni tishio lolote kwa Maalim Seif kuingia ikulu kwani Makamu wake atakua ni Mtu kutoka CCM na Jeshi lote ni hali hili na kila kitu ni hivi hivi tunachoangalia ni kuheshimu chaguo la wananchi.

Huku Tanganyika ndio bado wapinzani hawajakubalika kufikia kiwango cha kuachiwa Ikulu kutokana na wengi wao kujiuza kwa kutafuta fedha.

Hao ukiwaachia Ikulu wataiuza kwa mabeberu na kuhamia zao Ulaya kama alivyofanya Nasari kule Meru.
 

Gia kubwa

JF-Expert Member
May 28, 2020
289
500
Shamsi Nahodha ni bora zaidi , ni makosa makubwa Zenj kuendelea kuchagua watoto wa Rais na kuutukuza mfumo wa kurithishana urais kimila! yakhe koo zingine pia wana akili na uwezo wa kuongoza nchi ati!

Zenji ni Republic sio Monarch basi shime wala mapembe tuipe heshma yake sio kuongozwa ongozwa na familia flani tu ni makosa kirepublic!
 

THE BREED

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,491
2,000
Jecha anafaa kwa ule umafia alomfanyia maalim seif !hadi wazungu wakasitisha msaada!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom