Profesa Maboko na Timu Yako; Kigezo Kikuu cha Kutoa Asilimia za Mikopo Kiwe Hiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Profesa Maboko na Timu Yako; Kigezo Kikuu cha Kutoa Asilimia za Mikopo Kiwe Hiki

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sabi Sanda, Feb 9, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Natumaini wote tumesikia kazi ambayo Profesa Maboko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amepewa na timu yake ya kufanya uchuguzi wa kina kuhusu mfumo mzima wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kisha kutoa mapendekezo kuhusu namna bora ya kumaliza tatizo la utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kuhakikisha kuwa bodi ya mikopo inakuwa na ufanisi uliotukuka.

  Matumaini yangu ni kuwa wataanza kwanza kwa kupata taarifa kamili kuhusu utumwaji wa fedha toka Hazina kwenda bodi ya mikopo na kuona kama kuna udhaifu wowote hapo. Kwa upande mwingine, wataangalia kwa kina na kuona kwa kiwango gani vyuo vinatimiza wajibu wao kwa wakati kuhusu suala hili la mikopo kwa wanafunzi wao.

  Mbali na ucheleweshaji wa mara kwa mara wa mikopo kwenda kwa wanafunzi, moja ya eneo ambalo wanafunzi wamekuwa wakililalamikia sana ni suala la MEANS TEST.

  Badala ya kutumia MEANS TEST ili kujua mwanafunzi husika anastahili asilimia kiasi gani, napendekeza kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi husika katika somo la Hisabati ngazi ya kidato cha nne ndiyo kiwe kigezo kikuu. Iwapo wazo hili litakubalika mapendekezo ni kuwa:-

  1. Mwanafunzi atakayepata A apate mkopo kwa asilimia 105--Asilimia tano ya ziada hapa itolewe kama Motisha.

  2. Mwanafunzi atakayepata B apewe asilimia 85. Pia hapa asilimia 5 itolewe kama motisha.

  3. Mwanafunzi atakayepata alama ya C apate mkopo kwa asilimia 65. Pia hapa asilimia 5 iwe kama motisha.

  4. Mwanafunzi atakayepata alama ya D apate asilimia 20 tu ya mkopo.

  5. Na mwisho, mwanafunzi atakayepata F apate asilimia 000 ya mkopo.
   
 2. K

  Kidagaa Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mawazo yako yanawalakini ukizingatia mfumo mzima wa elimu lakini pia mtandao wa shule za kata, je unajua kuna walimu wangapi wa hisabati tanzania? Je unafahamu kiasi cha upungufu wa vitabu? Je unajua kule vijijini hakuna vituo binafsi vya hata masomo ya ziada? Je unajua kwamba shule hata za mjini, mfano Sumbawanga mjini hakuna waalimu wa hisabati. Huoni kwamba vigezo vyako vitakuwa ni sababu mojawapo ya kuwatenga walala hoi wa nchi hii? Kikubwa ni kutafuta namna bora ambayo ni kutoa elimu kwa wote maadam nafasi ipo. Tuurudie ujamaa wetu wa kiafrika na si vinginevyo. Nawasilisha
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mh Sabi vigezo vyako sioni kama vina mantiki, hivi unafahamu kwa nn wanafunzi wa elimu ya juu wanapewa mikopo?
   
 4. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwenye issue ya mikopo kwa wanafunzi kuna masuala mengine ambayo sio Bodo ya Mikopo peke yake inaweza kufanya bila ushirikiano na vyombo vingine. Mfano ....uwezo wa wazazi/walezi wa wanafunzi sidhani kama bodi inaweza kucertify.

  Mwanafunzi mwenye uwezo mzuri wa kifedha anaweza kumuhonga afisa mtendaji aandikiwe kuwa ni yatima ili aweze kupewa 100% ya mkopo wakati si kweli. Hili si tatizo la bodi na linafall zaidi kwenye serikali kuu, serikali zetu za mitaa/TRA (mambo ya kodi - history ya tax payment) etc. Hapa maana yangu ni kuwa inahitajika system hii iwepo in place na bodi ya mikopo kutumia taarifa hizi kuverify information za wanafunzi waombaji.

  Kwa ufupi tatizo hili ni la kimfumo zaidi kuliko utendaji wa bodi ya mikopo. Ingawa na wao wanashare ya matatizo kama double/triple disbursement ya loans kwa mwanafunzi mmoja kama alivyoainisha Mwanakijiji kwenye article yake. Lakini hili nalo lilitakiwa lionekane na auditors ...either external au internal. Kwa kumalizia tatizo la yote haya ni tabia yetu ya kutotaka kuwawajibisha watu pale kosa linapofanywa.
   
 5. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mimi jamani, sina imani na tume hii. Sijui vigezo vilivyotumika kuwateua lakini nafikiri karibu wote walishiriki sana kwa kuunda Bodi ya mikopo iliyopo sasa. Hivyo hawatakuwa na jingine jipya la kutueleza. Ningependa sana kukawa na tume ambayo ni huru. Wajumbe wake wasiwe kwenye chombo chochote ambacho kilihusiana na uratibu au utoaji wa mokopo hiyo.

  Ningependa ushirikishwaji wa mashirika kama HAKI ELIMU, jumuia kama Wazazi na uwakilishi wa vijana. Haya yote hayapo au kama nimekosea nielimiswe.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Jamani Maboko hawezi kufanya lolote pamoja na kamati yake labda mngesema kuwa hio kamati iiundwe na watu walioko nje ya system ya vyuo vya elimu ya juu, sasa Maboko ni VC- sijui wa nini hapa mlimani, leo tena mnapa kazi! halafu sasa atafanya kazi za TCU au UDSM au za kamati? hakuna wengine ambao wangeweza kutumiwa? ni sawa na kesi ya Mwananyamala na kamati ikaundwa na madokta tena!!!!!
   
 7. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35


  Mkuu,

  Lengo la ushauri wako ni nini hasa? nafikiri suala la mkopo kwanza lingeangalia ufaulu wa mwanafunzi bila kujali kipato cha wazazi wake kwa maana ya kwamba mwenye Div I automatically a-qualify kupata mkopo kwa asilimia 100.

  Na kundi la pili liwe kwa wanafunzi waliopata Div II ambao watapata say asilimia 90 ya mkopo bila kujali kipato cha mwanafunzi lakini kwa mwanafunzi mwenye DiV II lakini anayetoka katika familia isiyokuwa na uwezo iwepo hiyo MEANS Test kuona kama anastahili kupata asilimia 100% ama la.

  Kwa Div III hapo wanaweza kuweka udhamini wa mkopo kwa asilimia 50 kwa wote lakini MEANS test pia itumike kuona kama mwanafunzi mwenye daraja hili anastahili kupata asilimia 100

  Lakini msisitizo ni kwa wanafunzi waliofaulu vizuri kupata asilimia 100 bila kujali uwezo wa wazazi wao hii inakuwa incentive kwa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.
   
 8. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  umeanza vizuri ila umemalizia vibaya sana.
   
 9. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kidagaa, changamoto uliyoitoa ni nzuri. Nia yangu hasa ya kutumia kigezo cha ufaulu wa Hisabati ni kuhakikisha kuwa hayo uliyoyasema kama vikwazo kwa wanafunzi wetu katika ngazi za elimu, yanapatiwa ufumbuzi haraka. Hatuna njia lazima tufanye kazi. Kuwa mlalahoi haimaanishi kuwa huwezi kufaulu vizuri somo la Hisabati. Je unajua kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wanafunzi wamefeli somo la Hisabati ngazi ya kidato cha nne mwaka 2010?. Serikali kuu lazima ikubali kubana matumizi kadri inavyowezekana na kuhakikisha kuwa bageti ya maendeleo kwa shule zetu za msingi mpaka chuo kikuu kila mwaka haipungui shilingi trilioni moja kwa mwaka. Hizi fedha zipo na zinapatikana bila tatizo lolote. Naamini Waziri wa fedha na timu yake wanajua ukweli na undani wa hiki ninachokisema. Uzuri wa kigezo hiki cha ufaulu katika somo la Hisabati kitaondoa kabisa utata uliopo kwa sasa wa kutumia MEANS TEST. Kwa upande mwingine ukiniuliza mimi ningependelea sana kila mwanafunzi apate mkopo kwa asilimia 100 kama itawezekana na kuwe na sharti kuwa hakufeli somo la Hisabati katika mtihani wake wa kidato cha nne.
   
 10. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba ufafanue kama hutajali.
   
 11. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana kimsingi na mawazo yako. Lengo langu kuu ni kuhakikisha yafuatayo:-

  1. Serikali inaboresha elimu yetu kwa ngazi zote kwa kiwango cha hali ya juu sana. Fedha zipo.
  2. Tatizo la Wanafunzi wengi kupita kiasi kufeli Hisabati linafikia mwisho.
  3. Idadi ya wanafunzi wanaochukua mchepuo wa sayansi inaongezeka kwa kasi.
  4. Tunapata walimu wa kutosha na wenye ujuzi wa kutosha kufundisha Hisabati kwa weledi unaotakiwa kuanzia ngazi ya Chekechea mpaka chuo kikuu.

  Hivi unafahamu kuwa kwa sasa zaidi ya asilimia 52 ya wanafunzi wanaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza huwa wamefeli somo la Hisabati katika ngazi yao ya shule za msingi?
   
 12. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Bila wanafunzi wetu kuwa na weledi wa hali ya juu katika Hisabati kuanzia ngazi ya shule za awali mpaka chuo kikuu, wataendelea kufanya vibaya sana kila mwaka na tusitegemee Muujiza kutokea-----HISABATI KWANZA.
   
 13. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na bila Kampeni ya Kitaifa na ya Kudumu ya HISABATI kamwe hatutatoka hapa tulipo. HakiElimu tunaomba muanzishe Kampeni hii ya Kitaifa ILI TAIFA LETU LIOKOKE.. Vinginevyo taifa halitatoka GIZANI KAMWE.
   
 14. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Tuwahimize sana watoto wetu wasome sana Hisabati ili waje kuwa Mabingwa katika fani mbalimbali.
   
 15. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ila Ni Muhimu Sana Huyo Mwanafunzi akawa amefaulu HISABATI NGAZI YA KIDATO CHA NNE NA SITA.
   
 16. A

  Analytical Senior Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani hizin ni criteria mbaya sana kuliko ukizingatia mfumo wa shule zetu Tanzania, ambapo mara nyingi wanaopata alama nzuri ni wale waliosoma shule nzuri na si za kata. Kwa maana hiyo watakaoweza kupata 100% ni wale wale wenye nazo. Mimi napendekeza watoe mkopo kwa kila mtu aliye na admission under TCU cutoff point. Kwa maana hiyo hakutakuwa na haja ya bodi labda tu kidawati kidogo kule wizara ya elimu. kwa hiyo fedha ambazo zingetumika kuendesha bodi ya mikopo zingetumika kuwa kukopesha wanafunzi.
   
 17. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana nawe Analytical iwapo tu mkopo utakuwa kwa asilimia mia moja na mwanafunzi lazima awe amefaulu somo la HISABATI katika ngazi ya kidato cha nne na sita. Lazima F za HISABATI zifikie MWISHO.
   
Loading...