Profesa Maathai afariki dunia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Profesa Maathai afariki dunia


110926135342_wangari_maathai_926x521_others_nocredit.jpg

110926135342_wangari_maathai_926x521_others_nocredit.jpg


Kazi yake ilitambulika kimataifa na kumfanya maarufu kote ulimwenguni ambapo alijulikana pia na watu mashuhuri







Mwanaharakati wa mazingira, mtetezi wa haki za wanawake na mshindi wa tuzo ya Noble Profesa Wangari Maathai afariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 baada ya kuugua saratani.

Chanzo:
BBC Swahili - Habari - Profesa Maathai afariki dunia
 
[h=1]Prof Maathai kuzikwa kitaifa[/h]
110926083645_jp_maathai226x170_nocredit.jpg
Prof Wangari Maathai


Rais wa Kenya Mwai Kibaki ametangaza siku mbili za maombelezo kufuatia kifo cha Profesa Wangari Maathai.
Kulingana na taarifa ya rais Kibaki iliyotumwa kutoka Ikulu, hayati Profesa Maathai atafanyiwa mazishi yenye hadhi ya kitaifa.
Pia ametangaza siku mbili za kuomboleza kifo cha mwanaharakati huyo wa kutetea haki za mazingira.
Kuanzia kesho hadi Ijumaa bendera kote nchini Kenya zitapeperushwa nusu mlingoti.
Haya ndio yatakuwa mazishi ya kitaifa ya tatu kufanywa tangu Kenya ipate uhuru mwaka 1963.
Mazishi ya kwanza yalifanyika mwaka 1978 baada ya kifo cha rais mwanzilishi wa Kenya Jomo Kenyatta na mara ya pili ni baada ya kifo cha makamu wa rais Michael Kijana Wamalwa.
Tofauti na viongozi hawa Profesa Maathai hakuwa kiongozi wa serikali wakati wa kifo chake.
Awali taarifa kutoka familia ya mwanaharakati huyo ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza mwafrika kushinda tuzo ya amani ya Nobel, ilisema bado wanajadiliana kuhusu siku ya maziko na eneo gani.
Profesa Maathai alifariki Jumapili usiku baada ya kuugua saratani ya uzazi.
Viongozi wamekuwa wakituma salamu zao za rambirambi kutoka pembe zote duniani.
Chanzo: BBC Swahili - Habari - Prof Maathai kuzikwa kitaifa
 
Back
Top Bottom