Profesa Lipumba kumbuka ulivyotusaliti upinzani wewe na Dr. Slaa

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Ninashangazwa sana Kwa MTU mzima msomi wa ngazi ya Juu Mzee wetu, Prof.Lipumba kufuta Barua yake ya kujiuzulu Na kutaka kurejea tena CUF. Prof.Lipumba Kwa mbwembwe nyingi bila kujali Watanzania wapenda mageuzi aliamua kutukimbia katika kipindi muhimu cha kuunganisha nguvu ili tushinde Uchaguzi lakini yeye Na Msaliti wa Upinzani Dr.Slaa waliamua kutusaliti Na kumpa Adui nguvu Na siri za Wapinzani.

Hakika Wapinzani hatutawasahau Wasaliti hawa katika Historia ya Upinzani Tanzania.Nawaomba Watanzania Na has a Viongozi wa CUF "Msimkubali Prof.Lipumba"Ametumwa Kuja kuiua CUF .Wakati muhimu wa Prof.Lipumba kuiongoza CUF ilikuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu , Kwa sasa CUF INA viongozi wake makini ambao wameiwezesha CUF kuongeza idadi ya Wabunge Na Madiwani kuliko kipindi Prof.Lipumba akiwa Mwenyekiti.Nasema Prof.Lipumba akikubaliwa basi Kifo cha CUF kimewadia.
 
cbe75f485219c4476ca39fdbc874e265.jpg
 
Muda utatupa majibu sahihi, CUF ndio iliomsaliti Lipumba...sababu za Lipumba kujiuzulu uenyekiti zinaeleweka.....na sababu za kutaka kurudi zitaeleweka baadae
 
viongozi wa CUF wakimrudisha tashangaa sanaa...naona anarudi ili aimalize kazi aliyolipwa na CCM ya kuuwa umoja wa upinzani aka UKAWA....
 
Aendelee kuwa mwanachama wa kawaida. Wakati tunamshawishi na kumpigia magoti asiondoke, kwa mbwembwe alitupuuza.

Tuliendelea na safari yetu na hatimaye tukavuka salama kwa mafanikio makubwa katika historia ya CUF Bara.

Tunamhitaji sana Prof Lipumba kuendelea kuwa mwanachama wa CUF ila hatumtaki kabisa kuwa kiongozi wetu.

Tunamshukuru sana kwa mazuri yote aliyotutendea. Ila hatutasahau baya moja alilotutendea pia
 
Back
Top Bottom