Elections 2010 Profesa Lipumba: Kipi kichuguu na upi mlima?

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,319
306
Profesa Lipumba - rejea mdahalo wako ITV: Kipi kichuguu na upi mlima?

Ha ha ahaaaaaa mmeanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe , mie huko sipo sio upande wangu. Ila nawashauri wapinzani nyie wote Muungane muwe kitu kimoja, umoja ni nguvu........................la sivyo CCM itawabwaga kila uchaguzi
 

Hardwood

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,020
1,024
Prof Lipumba alidhani kuwa PHD yake ingetosha kumpa ukuu bila kuioanisha na manufaa yake kwa watanzania!!!!! Alikosea sana..... Alishindwa kutueleza kwanini watu ambao sio PHD holder (lakini wenye utendaji kwa watu wao uliotukuka) kama Mwl. Nyerere ni kama MLIMA EVERIST kulinganisha na yeye, ambaye hapa yeye hata kichuguu ni kikubwa sana......
Profesa Lipumba - rejea mdahalo wako ITV: Kipi kichuguu na upi mlima?
 

Bwanga

Member
May 26, 2010
46
6
ha ha ahaaaaaa mmeanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe , mie huko sipo sio upande wangu. Ila nawashauri wapinzani nyie wote muungane muwe kitu kimoja, umoja ni nguvu........................la sivyo ccm itawabwaga kila uchaguzi


muungano upi miongoni mwa wapinzani wakati ccm na cuf washafunga ndoa?? Ni rahisa kwa ccm kuungana na cuf kuliko cuf kuungana na chadema!!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
229
Nafikiri ndoa ya CUF na CCM kule chumbani imemtesa sana Lipumba huku bara. Halafu isitoshe, kule chumbani Maalim nasikia kaminywa kisawasawa!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
229
Nasikia Mugabe ana digrii sita. Lakini ona kule alikoipeleka nchi.
 

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Ni kweli kabisa muungano wa CUF na wapinzani wengine hautakuwa na maana yoyote baada ya CCM na CUF kuingia mwafaka wa Zanzibar. Bila shaka wengi hawata unga mkono jambo hili. Lakini huu ndio ukweli
 

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,608
4,252
Ni kweli kabisa muungano wa CUF na wapinzani wengine hautakuwa na maana yoyote baada ya CCM na CUF kuingia mwafaka wa Zanzibar. Bila shaka wengi hawata unga mkono jambo hili. Lakini huu ndio ukweli

Uko sahihi kabisa. Kama CCM na CUF wameungana, tunawezaje kusema CUF wako upande wa upinzani? Itoshe kusema kuwa CCM na CUF na vyama tawala-wenza!
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
19,702
4,264
limemshuka Lipumba.
Alidai yeye ni Mlima, na Dr Slaa ni kichuguu.
Sasa wananchi ndo wamemuonyesha kuwa yeye ni kichuguu.
 

Ibnabdillahi

Member
Oct 31, 2010
39
0
Profesa kaonyesha ukakamavu wakisiasa,CUF INA VITI 24 & CHADEMA 22 NANI MLIMA?, ILA SLAA NI MCHANGA KISIASA,BORA AGOMBEE UBUNGE 2
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,607
5,565
Profesa kaonyesha ukakamavu wakisiasa,CUF INA VITI 24 & CHADEMA 22 NANI MLIMA?, ILA SLAA NI MCHANGA KISIASA,BORA AGOMBEE UBUNGE 2
Napenda kuongezea hapa kwa kifupi namjibia profesa kama ningelikuwa ni yeye:

"Ni kweli mimi nilitamka vile ITV na nimedhihirisha kwa maana nilijiandaa kwa lolote litakalotokea, Ila mwenzangu yeye alikuwa hoi taabani baada ya kucharazwa ambako hakukutarajia, mimi nilikuwa na cha kusema na nilikisema yeye hakuwa nacho aliingia mitini. mimi ninao uzoefu wa kupambana na CCM kwa hoja yeye hana ndio maana alibaki na wimbo mmoja wa UFISADI kwenye kampeni. Namheshimu Dr, Slaa, lakini ajue kupambana na CCM sio lelemama, CCM ni ngoma nzito. Ni mwizi asiekimbizwa kwa makelele, anakimbizwa kimya kimya. Ila namkumbusha Dr. Slaa nae afanyie kazi haya = Ng'ombe hanenepi siku ya Mnada, pia Mbuzi hata anenepe vipi hatolingana na Ndama wa Ng'ombe"
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom