#COVID19 Profesa Lipumba apata chanjo ya Covid-19, ashauri wananchi wachangamkie fursa

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(Unicef), Cox Bazaar nchini Bangladesh.
Huu muda angeutumia kuwafundishha watu kujikwamua kiuchumi badala ya kuropoka senseless statements, kwahiyo wasio na ndugu au uwezo wa kufika huko wafe kivyao
 
Tz bd sana, kuna muda unawaza km hao mabeberu ndio wametupa elimu, technology, madawa nk, Leo hii watumalize kupitia chanjo!!? Yaani wanasiasa bd mnafuata propaganda za mwenda zake wa kujifukiza manyungu. Hata mifano hamuoni nchi zilizoendelea Europe, USA nk. Kiongoz anachoma chanjo kimya kimya we we unaambiwa chanjo so salama. Aisee hili neno #Tanzia litasikika sana kwa huu ujinga wa wanasiasa.
 
K

Lipumba pc

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo Jumatano Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(Unicef), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

"Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao.

"Hivyo na mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezeaha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, "amesema Profesa Lipumba.

Hata hivyo amesema baada ya chanjo hiyo ya awali anatakiwa arudi tena baada ya wiki sita mpaka nane kupata chanjo ya pili ili kukamilisha chanjo nzima ya kujikinga ya kujikinga na ugonjwa huo.

Pia mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia chanjo hiyo ili kuwa salama.

Wakati kwa upande wa Serikali ameishauri iangalie namna ambayo itawezesha wananchi wanaougua ugonjwa huo kupata matibabu kwa yake kwa gharama nafuu.

MWANANCHI
Kwa hiyo amechanjwa hivyo hatakufa?

Aende akawadanganye wanyamwezi wenzie
 
Back
Top Bottom