Profesa Lipumba alia na ucheleweshwaji Tume Huru ya Uchaguzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema ana wasiwasi kama maazimio ya Wadau wa Demokrasia yatafanyiwa kazi.

Amesema “licha ya dhamira ya Rais Samia na falsafa yake ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya, lakini suala la Tume Huru ya Uchaguzi limekuwa kitendawili".

Lipumba ameongeza kuwa ni muhimu Tume Huru ya Uchaguzi ipatikane kwa haraka ili ipate muda wa kuandaa Uchaguzi Huru na wa Haki wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

=======================

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kupata tume huru ya uchaguzi imekuwa ni kitendawili licha ya jitihada za maridhiano zianzofanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 28, 2022 jijini hapa, Profesa Lipumba amesema amejawa na wasiwasi kuona hata maazimio waliyokubalina kwenye mkutano wa wadau wa demokrasia uliofanyika jijini Dodoma Desemba, 2021 kama yatafanyiwa kazi.

"Nina wasiwasi mkubwa kwani sioni maandalizi ya kupata tume turu.

“Pamoja na dhamira ya Rais Samia (Suluhu Hassan) na falsafa yake ya 4R yaani ‘Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga upya).

Akikumbusha maazimio waliyokubaliana katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa jijini Dodoma, amesema suala la kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi lilijadiliwa.

“Tume huru isimamie chaguzi zote zikiwemo za serikali za mitaa," amesema.

Amesema ni muhimu tume huru ya uchaguzi ipatikane kwa haraka ili iwe na muda wa kuandaa uchaguzi huru na wa haki wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

MWANANCHI
 
Wazo zuri, lakini linatoka katika kinywa gani hili?

Hawa watu waliolambishwa asali wamebakia kutoa maneno ya hamasa ili sisi raia tuone kuwa tuna viongozi wa upinzani, kumbe ni masisiem mtupu yaliyojipangia mikakati na majukumu ya kuua upinzani nchini.

Huyu Lipumba na R.i.p Lyatonga Mrema waliwekwa upinzani na sisiem kwa mikakati maalumu ya kudhoofisha upinzani.

Palipokuwepo na Mrema ama palipo na Lipumba hapakosi migogoro, hata kama haipo, lazima ianzishwe kwa makusudi kukidhi lengo lao la kudhoofisha.

Mimi huyu jamaa huwa simsikilizi, maana kitokacho kinywani mwake hata kiwe na sura ya hekima namna gani, ujue hiyo ni ghilba na mkakati maalumu!
 
Back
Top Bottom