Uchaguzi 2020 Profesa Lipumba akiwa Mkinga, Tanga: Nichagueni Oktoba 28 niwe Rais ili nisimamie maendeleo ya kiuchumi nchini

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20201010_155521_978.jpg

NICHAGUENI OKTOBA 28, NIWE RAIS ILI NISIMAMIA MAENDELEO YA KIUCHUMI NCHINI "PROF.LIPUMBA"

TANGA- MKINGA

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itajenga uchumi wa kisasa wenye ushindani wa kitaifa na kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi unaokuwa kwa kasi bila kuharibu mazingira, na ambao utakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Kukua kwa uchumi kunahitaji uongozi imara na utawala makini, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji mzuri wa
mikakati na mpango hiyo. Kujenga mazingira mazuri ya kuwekeza, kufanya biashara na ushirikiano wa kimataifa bila kuathiri uhuru wa nchi yetu.

Kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 8 – 10 kila mwaka kwa miaka kumi ijayo na kufanikisha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu mwaka 2030.
 
CUF iliwahi kuwa na nguvu sana lakini baada ya 2015 walipoteza nguvu hizo kuanzia Zanzibar na sasa bara!

Wakati mwingine ni vema kujipima. Vyama vingi haviganyi cost-benefit analysis au hata SWOT kujua kama waingie au wasiingie. Ingetosha CUF kuwekeza katika udiwani. Hawana nguvu ya kutosha hata kwa wabunge kwa sasa!
 
Back
Top Bottom