Profesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Mkuu wa Chuo mwenye ekimu kiwango cha Professa ataweza kuikwamua Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere Kigamboni ili kiwe Chuo cha mfano Afrika Mashariki na Kati.Wahusika wangezingatia hilo kwani Chuo hicho kina Hostoria ya kuwatoa viongozi wa nchi. Chuo hicho bado hakina Mkuu wa Chuo kutokana na aliyekuwepo kumaliza muda wake. WanaJF mnaoifahamu Chuo hicho mna maoni gani juu ya hili kwa mamlaka husika?
 
Jina la chuo halijatendewa haki, wapatikane academic staff wenye ranks za juu
 
Jina la chuo halijatendewa haki, wapatikane academic staff wenye ranks za juu

Ni kweli jina halijatulia, Mkuu wa Chuo akiwa Professa hataogopa kuwaajiri Ma Dr. wengi na wenye shahada za uzamili.
 
hivi chuo ili kiwe chuo lazima kiwe na professa au......maana sijakuelewa!!!!!!!!!!
Professa ni Elimu ya juu kabisa katika taasisi ya Elimu kama Chuo/Chuo Kikuuu, hivyo kiongozi wake ni vema awe na elimu hiyo ili aweze kuonyesha njia kutokana na uwezo wake.Wewe maoni yako ni nini kama umeelewa?
 
Udom kuna maprofesa katika safu yote ya juu lakini ni janag la kitaifa
 
Udom kuna maprofesa katika safu yote ya juu lakini ni janag la kitaifa
Tatizo la Udom si Uprofessa ila tatizo ni udini, ubaguzi na upendeleo.Angalia pana Udom mwanafunzi anaweza kufelishwa kwa kuwa ni ndugu wa fulani au mfuasi wa chama fulani.Udom mfanyakazi anapatikana kindugu/kidini na mshahara mkubwa ni hivyohivyo, hivyo vyote havina uhusiano na Uprofessa wa Mkuu wa Chuo ila ubinafsi tu.Kwa ujumla tunategemea kuwa katika Vyuo wale wanaoongoza wawe na elimu ya juu ambayo ni uprofessa kwani vyuo vinahusika na utafiti, ufundishaji na ushauri.
 
ni kweli kiongozi lazima aonyeshe njia sio tu kwa kuwa na mipango mizuri au kuwa mtu wa mikakati lakini pia katika suala la ELIMU akiwa wa kiwango cha Full Professor itakuwa inatia changamoto nzuri lakini elimu yake tu haitoshi inatakiwa kuwe na Bodi mahiri na Menejimenti iliyojaa kiu ya maendeleo!mikakati isiyotegemea pesa za serikali tu pia walimu wa kujitosheleza walio na hamasa ya kutoa mchango wao katika jamii kupitia machapisho n.k
Serikali pia inatakiwa kukisaidia kifedha chuo hicho licha ya ka wimbo ka kasungura kadogo. Serikali wanaweza kuwadhamini katika mifuko ya jamii na taasisi nyingine ili ziwekeze mitaji yao katik chuo ili chuo kipanuka na kuwa na uwezo zaidi katika miundo mbinu mbalimbali
 
Mkuu wa Chuo mwenye ekimu kiwango cha Professa ataweza kuikwamua Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere Kigamboni ili kiwe Chuo cha mfano Afrika Mashariki na Kati.Wahusika wangezingatia hilo kwani Chuo hicho kina Hostoria ya kuwatoa viongozi wa nchi. Chuo hicho bado hakina Mkuu wa Chuo kutokana na aliyekuwepo kumaliza muda wake. WanaJF mnaoifahamu Chuo hicho mna maoni gani juu ya hili kwa mamlaka husika?

Hapana, Chuo hicho kina hstoria ya kuwatoa makada wa CCM
 
Makada waliokabidhiwa chuo wamekididimiza. Chukulia kwamba kuna uhaba wa mabweni, vitabu, madarasa miundo mbinu mibovu lakini watawala wanaona priority ni kujenga ukuta wa mabilioni ya fedha. Hapa unategemea nini? Chuo kinahitaji management ya wanataaluma si wanasiasa.
 
Kwa sasa ni muda muafaka kwa serikali kutangaza nafasi ya Mkuu wa Chuo hicho maana aliyepo anaondoka mwisho wa 2013. Ni vizuri sifa ya Mkuu wa Chuo iwe ni Profesa na msaidizi awe na PhD ili kuifufua Chuo hicho ambacho sasa kimeandamwa na kashfa za ufisadi wa mali za chuo na ufisadi wa elimu.
Mkuu wa Chuo mwenye ekimu kiwango cha Professa ataweza kuikwamua Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere Kigamboni ili kiwe Chuo cha mfano Afrika Mashariki na Kati.Wahusika wangezingatia hilo kwani Chuo hicho kina Hostoria ya kuwatoa viongozi wa nchi. Chuo hicho bado hakina Mkuu wa Chuo kutokana na aliyekuwepo kumaliza muda wake. WanaJF mnaoifahamu Chuo hicho mna maoni gani juu ya hili kwa mamlaka husika?
 
Mkuu wa Chuo mwenye ekimu kiwango cha Professa ataweza kuikwamua Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere Kigamboni ili kiwe Chuo cha mfano Afrika Mashariki na Kati.Wahusika wangezingatia hilo kwani Chuo hicho kina Hostoria ya kuwatoa viongozi wa nchi. Chuo hicho bado hakina Mkuu wa Chuo kutokana na aliyekuwepo kumaliza muda wake. WanaJF mnaoifahamu Chuo hicho mna maoni gani juu ya hili kwa mamlaka husika?
Hili ndilo suluhisho kwa kuikwamua Chuo hicho.
 
Hayo yapo vyuo vingi mf. Ilitokea cbe wakamkataa dr mmoja hivi, Mipango au irdp ndo balaa. Siasa inaongoza elimu ya juu. Jk sijui halioni hili. Vyuo vya juu visimiwr na profesa au dr mwenye calibre sio kipeana tu. Nacte nao vilaza tu, wametoa mwongozo lakini haufwati, yanabaki majungu ya vyeo. Jk lione hili utaua vyuo kupeleka viongozi weak na wasio na elimu. Ni.angalau huyo.ana phd kuliko sehem.nyingi wapo wenye kadigri ksmoja tu, wakati huyu anasimamia utafiti, publication etc. so atabaki simamia supporting staff. Elimu ya juu sio halmashauri kwa madiwan, hku ni kwa think tanks na,sio sink tanz
 
Sikufahamu kuwa uprofesa ni elimu ya juu kabisa. Nidhani ni rank ya juu ya kikazi katika vyuo vikuu. Hivi ni chuo gani kinatoa uprofesa nataka nimshauri mdogo wangu akasome kwakuwa alimaliza Phd siku nyingi na akadhani hakuna level ya elimu iliyobaki ya kusomea. What I know there is a lot of good doctors who have published enough to qualify to hold any higher post in their area of speciality.
 
Professa ni Elimu ya juu kabisa katika taasisi ya Elimu kama Chuo/Chuo Kikuuu, hivyo kiongozi wake ni vema awe na elimu hiyo ili aweze kuonyesha njia kutokana na uwezo wake.Wewe maoni yako ni nini kama umeelewa?

Si kweli!!!

Elimu ya juu kabisa ni "PhD". Mtu kuwa "professor" ni lazima uwe mkufunzi!! Ni wadhifa/cheo/ngazi ambayo mtu anapandishwa kutokana na uzoefu wa kufundisha.
 
Back
Top Bottom