Profesa Kitila Mkumbo: Waziri Ndalichako hana mamlaka ya kupanga sifa za kujiunga na chuo kikuu

nashangaa hata Mimi kila akiamka tamko...

Usiku tamko,mchana tamko,jioni tamko na asubuhi tamko.....

Aache kuchezea elimu yetu kuturudishia mifumo ya kikaburu..........

Matamko ya kielimu yanaitaji research ndipo uongee.....

Ndio maana Niko na mashaka na u professor wake......
 
Hongera Prof Kitila Mkumbo kwa kuweka uwazi juu ya mamlaka za uamuzi wa kuchagua sifa za wanafunzi wa kujiunga na chuo kikuu huyo mama sijui amepata wapi hayo mamlaka au anajua ukiwa waziri tu wa wizara fulani unajiamulia tu no
 
ninachokiona mimi serikali inapitia kipindi kigumu sana,mambo yamekwama na inaonekana wa kuyatatua hayupo/hasikilizwi,kila mahala ni kilio,kuanzia maisha magumu,makampuni kufilisika/kufungwa.Na muda wa blaa blaa kuwaaminisha watu uongo,umekwisha.

Wanachofanya sasa ku counter hayo,wanatumia mbinu kadhaa,walianza na uhakiki,zikapigwa kelele weeee ili kuwaficha watu hali mbaya iliyoko serikalini,kila mkuu wa mkoa,wilaya,akawa anaambiwa aongee hata hovyohovyo,ikaenda weeee,njia ya wasiosema kweli ni fupi,uhakiki ukakosa swaga ya kuvutia,wameuweka pembeni.

sasa hivi waliopewa jukumu la kuwatoa watu kwenye hoja ni makonda na ndalichako na makonda,lakini naona mafanikio yao ni madogo.

hawajafanikiwa kuripotiwa sana na kwa uzito na vyombo vya habari,na pia njia wanayotumia ni ya kuumiza watu,hisia,na sio ya kiutu,hivyo inawaongezea chuki.

Bora Jk alimvumbua babu wa loliondo ambaye alifanya cover ya mambo ya serikali bila kumuumiza mtu wala kumtukana
 
Hivi kwanini Profesa Mkumbo hupenda sana ' publicity ' kupitia ' matukio ' ya Wanataaluma / Wanazuoni wenzake?
Swali, ufafanuzi wa Profesa Mkumbo, na uropokaji wa Profesa Ndalichako ni nani yuko sahihi?

Kimsingi Profesa Mkumbo amehojiwa na media na akatowa ufafanuzi wa kile anachokijuwa na si kwamba amemtarget Profesa mwenzake.
 
Hivi huyu Ndalichako si aliondolewa kazini alipokuwa katibu mkuu wa wa baraza la mitihani?? Nahisi harufu ya visasi..!
 
Bado tusubiri matamko mengine....kwani hadi 2020 unafikiri atafanya nini ili kujionyesha kwa mkhururu
 
Ukiisoma kwa kina Sera ya Elimu, Proffesa Mkumbo yuko sahihi. Upo utaratibu uliotamkwa vema katika Sera. Sasa ukiona mtu anaenda tofauti na Sera ujue anataka kutengeneza matatizo. Najua wataalamu wa elimu pale Wizarani wanaelewa kabisa Waziri anaingia chaka na kwa mfumo uliopo hawawezi kumpinga waziwazi Kiranja wao.Kama amehisi matatizo katika Sera ni vyema akafuata taratibu za kutengeneza Sera mpya ya Elimu. La sivyo ataivuruga Elimu na mwishowe tutaanza kulaumiana na kutafuta mchawi.
 
kuwa profesa sio kwamba unajua kushinda watu wote tatizo la hawa viongozi wa sasa hivi ni inferiority complex kwasababu yakupewa majukumu kiupambe na kimajungu,watu wanafanyakazi sio kwa faida ya wananchi bali kuwa komoa kina fulani..!!huyu mama badala ya kudili na changamoto za elimu ikiwemo maslahi ya waalimu unakimbilia kupindua pindua mambo hivi huko CCM manifesto yao inasemaje kuhusu mpango wakuinua elimu ya Tanzania??naungana na wale wabunge wanao sema kuwa hawa wabunge wakuteuliwa wamekuwa wanaamua mambo kijingaajinga kwakuwa hawakenda majimboni kuomba kura...!!Marehemu Mungai alibadili mfumo wa elimu wataalam na wadau wa elimu wali criticize sana mpango ule na kweli ndo ulio kuja kuuwa kabisa elimu ya kujitegemea,akaja mama Sitta na cabinet yake nao ndio wakajaribu kurudisha mfumo uliokuwepo lakini ukashindwa ku compete kwakuwa haukuwa na muelekeo chanya ulikaa kisiasa zaidi. kawambwa kaja kaacha elimu ya oheahe title ya degree PHD kwa wahitimu lakini less competent candidate katika soko la ajira ndani ya Jumuiya ya Afrika mashariki,hivi huyu profesa hajifikiri au kujiuliza mkoloni na baba wataifa waliwezaje kuunda mfumo wa elimu bora ya kujitegemea?Hivi leo kweli elimu ya darasa la saba haina thamani tena wakati kwa mkoloni tu darasa la nne alikuwa bora kushinda hata mwanafunzi wa chuo kikuu wa leo,ccm Ndalichako wajue taifa haliitaji pass mark linahitaji wataalam na wabobezi rudisheni elimu ya ufundi vyuo vya ualimu,shule za msingi na sekondari,boresheni vyou vya ufundi stadi..!! kwanza kwa tathimini ya haraka watu wa blue color job ndio wengi kuliko hao white color na serikali ya viwanda hata siku moja haijengwi na white color job haya malalamiko ya ajira vijana kukosa ajira yangepungua..!!Mwisho sitasahau dhamira ya kweli ya MH.Lowassa ndomana aliweka kipaumbele cha elimu aliona mbali kushinda kundi kubwala timu ya watu 30 ndani ya ccm
 
Back
Top Bottom