Profesa Kitila Mkumbo,Uongozi si Umahiri wa Kuongea ama Kukosoa

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Wakuu,Profesa wetu Kitila amenishangaza tena kwa kutokujua uongozi ni nini.

Profesa Kitila anasema: "Kwawaliofuatilia mjadala wa escrow bungeni watakubaliana nami kwamba wabungevijana na wale wa kizazi kipya katika siasa wameonyesha uwezo mkubwa mno wakiuongozi.


Tumeona jinsi ambavyoDavid Kafulila alivyoliibua suala la escrow na kulifafanua mara nyingi bilakuchoka hadi watu walipoanza kuelewa.

Mwanzoni alionekanaanapiga kelele tu kwa kiasi ambacho hata wabunge wenzake ndani ya upinzanihawakumpa ushirikiano wa kutosha.

Kwa muda mrefu kabisa suala la escrowlilibaki kuwa jambo binafsi la Kafulila na mbunge mwenzake Zitto Kabwe hadisiku za hivi karibuni na hasa baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya PAC bungeni".

Kitila ameeleza haya katika gazeti la leola Mwananchi.Tatizo la Kitila anafikiri uongozi ni umahiri wa kuhoji aukukosoa.Tafiti zinaonyesha kuwa watu ambao ni mahiri sana wa kuongea siwatendaji wazuri.Hata Mwalimu Nyerere aliweza kuongea vizuri vile baada yakujiandaa sana.

Na hili alilisema Mama Maria Nyerere.Kwa hiyo ni sahihi kusemakuwa Nyerere hakuwa na kipaji cha kuongea isipokuwa kwa maandalizi ya nguvu.


Ukiwafuatilia vizuri akina Zito na Kafulilautagundua kuwa hawana uwezo hata wa kuongoza kijiji.Tumeona jinsi ambavyoKafulila alipokuwa katibu mwenezi CHADEMA alivyoshindwa badala yake akawaanamudu kufanya vurugu tu.Na Zito hawezi kujivunia utendaji wake akiwa NaibuKatibu Mkuu CHADEMA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom