ndayilagije
JF-Expert Member
- Nov 7, 2016
- 7,492
- 8,295
Katika hili ninajiuliza mambo kadhaProfesa Juma Kapuya aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi,amefunguka kuhusu ndoa yake aliyofunga Jumapili ya Februari 12 na mwanamke anayejulikana kwa jina la Mwajuma Mwiniko.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Kapuya amesema anawashangaa watu wanaomsema kuoa mwanamke aliyemzidi umri kwani wanataka aoe mwanamke anayefanana na bibi yake?
Kapuya amesema umri hauhusiani na mapenzi, hivyo watu wakubali matokeo kwani hajamtorosha shule huyo mwanamke,wala hajavunja sheria, mila, desturi pamoja na dini.
"Unajua mimi nawashangaa sana watu wanaoshangaa mimi kuoa mwanamke niliyemzidi umri,hivi umri unahusiana nini na mapenzi? Na ukiangalia huyu mwanamke mimi sijamtorosha shule, wala sijavunja mila, desturi pamoja na dini, au watu walitaka nioe mwanamke anayefanana na bibi yangu? Nawaambia wakubali matokeo tu waache kusema sema," alisema Kapuya.
Aidha, Kapuya aliongeza kusema, "Yeye sio wa kwanza kuoa mwanamke wa umri huo mdogo chamsingi ni kukubaliana tu, na siwezi tena kuoa mwanamke mwingine kwani mke huyu ni somo tosha, sababu mke wangu wa kwanza anaishi Dar nampenda sana ,huyu ni wa pili sasa natafuta nini tena kuoa? Hapa subirini tu mtoto kutoka kwa huyu mwanamke mnayesema ana umri mdogo,"alisema Kapuya.
Hata hivyo Kapuya amesema kwa mara ya kwanza amekutana na Mwajuma Kaliua, alipokuwa anaenda kufanyia vikao na Kaliua na Urambo sio mbali.
-Mwananchi
Dah! Demu wa jamaa kaolewa na huyu mzee....anyway, "MwanaFA unaoa lini?" Bado niponipo kwanza.Profesa Juma Kapuya aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi,amefunguka kuhusu ndoa yake aliyofunga Jumapili ya Februari 12 na mwanamke anayejulikana kwa jina la Mwajuma Mwiniko.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Kapuya amesema anawashangaa watu wanaomsema kuoa mwanamke aliyemzidi umri kwani wanataka aoe mwanamke anayefanana na bibi yake?
Kapuya amesema umri hauhusiani na mapenzi, hivyo watu wakubali matokeo kwani hajamtorosha shule huyo mwanamke,wala hajavunja sheria, mila, desturi pamoja na dini.
"Unajua mimi nawashangaa sana watu wanaoshangaa mimi kuoa mwanamke niliyemzidi umri,hivi umri unahusiana nini na mapenzi? Na ukiangalia huyu mwanamke mimi sijamtorosha shule, wala sijavunja mila, desturi pamoja na dini, au watu walitaka nioe mwanamke anayefanana na bibi yangu? Nawaambia wakubali matokeo tu waache kusema sema," alisema Kapuya.
Aidha, Kapuya aliongeza kusema, "Yeye sio wa kwanza kuoa mwanamke wa umri huo mdogo chamsingi ni kukubaliana tu, na siwezi tena kuoa mwanamke mwingine kwani mke huyu ni somo tosha, sababu mke wangu wa kwanza anaishi Dar nampenda sana ,huyu ni wa pili sasa natafuta nini tena kuoa? Hapa subirini tu mtoto kutoka kwa huyu mwanamke mnayesema ana umri mdogo,"alisema Kapuya.
Hata hivyo Kapuya amesema kwa mara ya kwanza amekutana na Mwajuma Kaliua, alipokuwa anaenda kufanyia vikao na Kaliua na Urambo sio mbali.
-Mwananchi
Wapo watu wanamsema katika mitandao wanajadili Picha na kusambaza
kiufupi huyu profesa yuko sahihi kabisa maana waoaji vijana wameadimika lakini basi ingekuwa vyema akaoa kimyakimya
Miaka ile iliyopita wakati nakua nilikuwa nikiambiwa mtu kasoma hadi kufikia ngazi ya profesa au dokta namchukulia ni mtu wa hadhi ya juu mno! Siku hizi naona kawaida sana
enzi hizo akija kaliua na ndege ya jeshi ilikua ni full matangazo kwa abilia wanakuja dar tua kaliua,angalau niliionjamlitaka nipande punda?!?
Vigezo vpo, sema vinatofautiana, mf pesa , elimu, ufupi, urefu , dini , nguvu , Sura, tabia , etc, ni ngumu kujua kigezo cha mtuHii ya Pro.nimeipenda sana inatuonyesha ni jinsi gani kuna tatizo la waoaji kwenye jamii hivyo mabinti wanalazimika kuolewa na MTU yoyote bila kuweka vigezo zaidi ya kigezo cha kuwa mwanamume.