Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kulipa ada ya kidato cha tano na sita Wanafunzi wa Kike

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
IMG_20210302_141738_857.jpg

Mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kulipa ada ya kidato cha tano na sita wanafunzi wote wa kike waliosoma katika shule za serikali na kupata Daraja la kwanza katika jimbo lake kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu 2021.

IMG_20210302_142123_334.jpg

Mbunge wa Kasulu Mjini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa Shilingi Milioni Mbili kwa ajili ya kutunusha mfuko wa kutoa motisha kwa walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya mwisho ya kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari Katika Halmashauri ya Kasulu Mji
 
Publicity. Ingawa the end justify the means na hongera kwake ila ingekuwa ni kutoa msaada angeweza kufanya kimya kimya bila kutangaza (hapo huenda kajilipa maradufu kwa kufanya kampeni)

Ukitoa sio lazima kila mtu ajue, unless otherwise unataka return ya wema wako.
 
Alipe kabisaaa🙏apewe control number alipie kwa jumla then zitasambazwa mashuleni waliko hao mabinti,we talk and do🙏
 
View attachment 1715551

Mbunge wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kulipa ada ya kidato cha tano na sita wanafunzi wote wa kike waliosoma katika shule za serikali na kupata Daraja la kwanza katika jimbo lake kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu 2021.

View attachment 1715552

Mbunge wa Kasulu Mjini na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa Shilingi Milioni Mbili kwa ajili ya kutunusha mfuko wa kutoa motisha kwa walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya mwisho ya kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari Katika Halmashauri ya Kasulu Mji
Good
 
Wasichana wangapi wanapata daraja la kwanza katika jimbo lake? Nampongeza sana, lakini angewasaidia wasichana wote wanaopata nafasi ya kuendelea kidato cha 5 na 6 hata kama wamepata daraja la pili au tatu.

Nahofia wa daraja la kwanza watakuwa wachache sana au kukosekana kabisa!
 
Mimi siamini Kama kasema hivyo. Labda arudie hiyo ahadi yake kwa kiingereza.
 
Back
Top Bottom