Profesa Janabi’s Diet: Njia rahisi ya Kupungua na ukaona matokeo ndani ya mwezi mmoja tu

Mnakoelekea mtasema maji nayo ni sumu
kwamtu mwenye presha ya kupanda ni sumu mkuu na ndo maana mtu presha ikipanda anapewa dawa anaenda kukojoa mara kwa mara ndo anapata unafuu ha haaa mkuu kwani hujui presha ya kupanda ikoje?
 
kwa wale ambao tumewahi kuangalia postmortem kitu kinachokuw akwenye mwili wa mtu ambaye ni mnene huwa hakiangaliki ni mafuta tumbo lote, kwenye moyo, kwenye figo. kwenye utumbo mkubwa na mdogo na madaktari wengi wakati wanafanya wanaanzaelezea chanzo cha kifo pia kama alikuwa na tatizo jingine wengi huonekana wanamoyo mkubwa, figo huanza kuwa na matatizo hata kama ilikuwa haijaripotiwa kama ugonjwa, pia maini huw ana kasoro kutokana na fat liver ambayo ni chanzo cha pombe kwahiyo ni swala lakuangalia vyema na kula kwa kulinda afya zetu si mpaka tupate matatizo ndo tuanze kimbizana na madaktari na hosipitali kukikinga ni rahisi ila matibabu ni ghali sana
Ningumu kubadilika ghafla lakini unaweza kuanza kuishi in moderation, punguza nusu ya ugali na wali unaokula, ongeza mboga kwenye sahani.
 
Tuangalie na kipato, nisipokula ugali nitakula nini mixa kazi ngumu. Jamaa ana pesa ndo maana anauwezo wa kumudu hao samaki hadi kushiba
 
Siyo postmoterm tu. Hata vi-operation vidogo kama ya kidoletumbo. Watu wanene, utumbo huwa umezibwa sehemu kubwa na mafuta. Na ni kazi kukiona kidoletumbo wakati wa operesheni.
kwa wale ambao tumewahi kuangalia postmortem kitu kinachokuw akwenye mwili wa mtu ambaye ni mnene huwa hakiangaliki ni mafuta tumbo lote, kwenye moyo, kwenye figo. kwenye utumbo mkubwa na mdogo na madaktari wengi wakati wanafanya wanaanzaelezea chanzo cha kifo pia kama alikuwa na tatizo jingine wengi huonekana wanamoyo mkubwa, figo huanza kuwa na matatizo hata kama ilikuwa haijaripotiwa kama ugonjwa, pia maini huw ana kasoro kutokana na fat liver ambayo ni chanzo cha pombe kwahiyo ni swala lakuangalia vyema na kula kwa kulinda afya zetu si mpaka tupate matatizo ndo tuanze kimbizana na madaktari na hosipitali kukikinga ni rahisi ila matibabu ni ghali sana
 
Mie nakula tu mingine yatajulikana mbele ya safari, unajinyima hiki usiumwe moyo unapata saratani, unajizuia huku kujilinda na saratani unapata t.b..

Kiukweli hiz diet tunapeana stress mie nakula na kunywa vizuri tu, kasoro haya masoda soda ndio nimeacha kuyanywa.. Huo wanga naula, napiga juice za kutengeza uraiani, nakunywa maji ya kutosha, nikipata nafasi naenda beach kukimbia(kufanya mazoezi)

Mengine anajua mungu.
 
Nachowez kukubali ni kupunguza kiwango cha carbs ila sio kuacha kabisa
Atakua yuko weak kimwili uyu akipewa kazi ngumu
Shukuru Mungu anashinda ofisini na kazi za akili za upasuaji sio za kubeba vitu etc

Kila mtu atathmini kazi anazofanya maisha yake na ale kuendana nayo
Unafanya kazi ngumu lazma ule
Unakaa ofisini km kina sie huwezi kula kama mbeba mizigo
 
And breakfast and lunch ni muhimu

Dinner ndo naweza shauri watu wale very very light
Miaka yote m light on that and najikuta having the same weight 5 years hence looking young lol
 
And drink the liquor mehnn ts good for your soul every now and then
 
alichozungumza kinaukweli kwa asilimia kubwa sana ila swala ambalo hakuliweka bayana ni kwavipi mtu utaweza kukaa bilakusikia njaa muda mrefuu, ni kwamba vyakula vingi vya mafuta na protini ukila usikii njaa kwa muda mrefu mfano ukila karanga,samaki, nyama unakuwa we ni mtu wa maji tuu na njaa inakuwa mbali, pia huwa havipandishi insulin kwa kiwango kikubwa
Ni vyakula gani vinaongeza insulin?na insulin ni nini hasa na ikiongezeka inaleta madhara gani?
 
Ni vyakula gani vinaongeza insulin?na insulin ni nini hasa na ikiongezeka inaleta madhara gani?
mkuu elimu ni pana ila insulin inazalishwa na mwili pia ulaji wa mara kwa mara inasababisha mwili kuzalisha insulini ila vyakula vingi vya wanga na sukari ndivyo vinafanya mwili unamwaga insulin kwawingi mwilinin na sukar ikiwa mwilini kwawingi insulin inachelewa kushuka ambako inapelekea madhara kwenye mishipa ya damu
 
Dr sebi list
Sebi-nutritional-guide.jpeg
 
Sasa wakuu na mafuta yakupikia mazuri tupikie mafuta gani
Mafuta mazuri ni ya nazi ama olive oil, ya kawaida mazuri ni alizeti kama Sunola au Sundrop. Sema yako vere vere expensive. Kwa kweli kuishi kwa diet ni gharama. Imagine utahitaji samaki mkubwa kiasi gani ili ujiskie kushiba. Uthitaji kuku wa kienyeji kiasi gani. Kwa mtu wa kipato cha elfu 10 per day anamudu vipi hio diet. Wacha tupambane na ugali maharage tu afterall kila mtu atandanja one day!
 
Back
Top Bottom