Profesa Ibrahim Juma: Muhtasari wa Hukumu kuanza kutolewa kwa Kiswahili mwezi Februari

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama ya Tanzania itaanza kutoa muhtasari wa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuanzia Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuanza kuendesha shughuli zote za Mahakama kwa lugha hiyo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika Februari Mosi, mwaka huu.

Maadhimisho hayo yatafanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama Kuu Tanzania.

Profesa Juma amesema, uendeshaji wa shughuli za Mahakama kwa lugha ya Kiswahili ni suala muhimu, lakini linahitaji umakini kulitekeleza.

"Mwishoni mwa mwaka jana, Mheshimiwa Waziri wa Sheria alitutembelea, tulizungumza kwa kina kuhusu uendeshwaji wa shughuli zote za Mahakana kwa lugha ya Kiswahili, lakini ni suala linalohitaji umakini mkubwa.

Hili suala ni muhimu sana na tayari katika Mahakama ya mwanzo shughuli zote zinafanyika katika lugha ya Kiswahili," amesema.

Profesa Juma amesema kwa sasa ni sahihi kusema Kiswahili kinatumika kwa asilimia 70 katika shughuli za kimahakama kwa sababu Mahakama hizo za mwanzo ndizo zinazosikiliza asilimia 70 ya mashauri yote.

Amesema, katika Mahakama nyingine ni kumbukumbu tu za kimahakama ndizo zinaandikwa Kiingereza, lakini shughuli nyingine zinafanyika kwa Kiswahili isipokuwa pale inapolazimu kutumia lugha ya Kiingereza.

Chanzo: Habari Leo

=======

Hongera kwa Jaji Mkuu kwa kuhakikisha Hukumu zote sasa zinaandikwa kwa kiswahili, maana itatusaidia sana watanzania kuelewa kilicho andikwa, hakika hii ni hatua kubwa na ya muhimu ktk upatikanaji wa haki kwa wananchi.

matumizi ya lugha ya kiswahili ni fahari na tunu kwa watanzania, nimekuwa nikiona mataifa mbali mbali kama vile: Urusi, China, uturuki, uarabuni n.k zikitumia lugha zao na zimefanikiwa sana ktk nyanja ya sheria, naamini pia Tanzania kwa mabadiliko haya ya matumizi ya kiswahili yatainua sana sekta ya sheria.

naaamini tasisi za kiswahili zilizo bobea tunazo, tunayo TUKI, BAKITA n.k kuna wabobezi wa kiswahili ambao wanaweza kabisa kutafsiri sheria zetu kwa lugha ya kiswahili.

Tudumishe utamaduni wetu, Lugha ndio kielelezo kikuu, wala hakuna dhambi yoyote kutumia lugha ya kiswahili, sisi sote ni watanzania/ waswahili hakuna haja ya kulazimisha kutumia kifaransa au kichina ktk shughuli zetu.

Lugha zingine kama; Kifaransa, Kingereza, Kichina, Kiarabu n.k zitumike kama lugha za mawasiliano tu lakini sio kendeshea shughuli zetu.
 
Urusi China Uarabuni Uturuki siyo wenzetu kihistoria wala kimaendeleo. Wenzetu ni Kenya, Uganda Zambia Zimbabwe au Nigeria ns South Afrika na wote wanatumia kiingereza mahakamani na shuleni. Maendeleo ya China na Urusi hayatokani na kutumia lugha zao yanatokana na historia zao mataifa yao yalikuwepo miaka zaidi ya 2000. Sisi hata miaka 100 kama taifa hatuna tunahitaji kutumia lugha za kigeni kuiba elimu za wenzetu. Afterall kiswahili siyo lugha ya babu zetu ni pidgin ya kiarabu. waswahili ni machotara wa kiarabu na kiafrika waliozalisha lugha hiyo nayo ni ya kigeni tu imported language.!!
 
kwa hiyo unataka kusema sisi watanzania asili yetu ni Uingereza na kiingereza ndio lugha mama?!!! au unamaanisha nini?

kenya na uganda wenyewe wanakitegemea kiswahili pamoja na mataifa mengine, Jumiya ya Afrika Mashariki amabyo kwa sasa nchi wanachama ni zaidi ya nchi 8 ambazo ni; kenya, uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, nchi zote hizo zimepitisha lugha ya kiswahili ndio lugha rasmi. sasa wewe kwa nini unakibeza na kukidharau kiswahili.

inakadiriwa kuwa kati ya 15% mpaka 20% ya watanzania ndio wanajua lugha ya kiingereza zaidi ya 85% wanajua lugha ya kiswahili kwa ufasaha.

sasa ni maajabu ya dunia kuwaandikia wananchi wako sheria zinazo wahusu wao kwa lugha ya kigeni!!! huo ni utumwa wa kifikra!! tubadilike.kiingereza kitabaki kuwa kama lugha muhimu ya mawasiliano lkn sio lugha ya kuendesha shughuli za wananchi wetu wa kitanzania. kumbuka siku zote hapa ni TANZANIA sio UINGEREZA.

ni kichekesho kwa wewe mtanzania mswahili kujifanya eti unakijua kiingereza vizuri zaidi kuliko kiswahili!!!!
enzi utamaduni wako na udumishe hiyo ndio silaha ya kulinda uhuru wa nchi yetu.
 
Hoja ni kwamba kiswahili kinajitosheleza
Na waswahili wanajua kiswahili
zaidi ya 95% ya watanzania wanazungumza kiswahili fasaha.
tuna taasisi zenye wataalamu walio bobea ktk lugha ya kiswahili, tuna TUKI, BAKITA n.k hao ndio kazi yao kutunga, kuendeleza na kuibua misamiati ya kiswahili,
kumbuka kuwa lugha inatabia ya kukuwa kulingana na matumizi....kadiri tunavyo itumia ndivyo misamiati mipya inajitokeza....
 
Mahakama ya Tanzania itaanza kutoa muhtasari wa hukumu kwa lugha ya Kiswahili kuanzia Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuanza kuendesha shughuli zote za Mahakama kwa lugha hiyo.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika Februari Mosi, mwaka huu.

Maadhimisho hayo yatafanyika sambamba na Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama Kuu Tanzania.

Profesa Juma amesema, uendeshaji wa shughuli za Mahakama kwa lugha ya Kiswahili ni suala muhimu, lakini linahitaji umakini kulitekeleza.

"Mwishoni mwa mwaka jana, Mheshimiwa Waziri wa Sheria alitutembelea, tulizungumza kwa kina kuhusu uendeshwaji wa shughuli zote za Mahakana kwa lugha ya Kiswahili, lakini ni suala linalohitaji umakini mkubwa.

Hili suala ni muhimu sana na tayari katika Mahakama ya mwanzo shughuli zote zinafanyika katika lugha ya Kiswahili," amesema.

Profesa Juma amesema kwa sasa ni sahihi kusema Kiswahili kinatumika kwa asilimia 70 katika shughuli za kimahakama kwa sababu Mahakama hizo za mwanzo ndizo zinazosikiliza asilimia 70 ya mashauri yote.

Amesema, katika Mahakama nyingine ni kumbukumbu tu za kimahakama ndizo zinaandikwa Kiingereza, lakini shughuli nyingine zinafanyika kwa Kiswahili isipokuwa pale inapolazimu kutumia lugha ya Kiingereza.

Chanzo: Habari Leo

=======

View attachment 1680977
The compromised judiciary!~
Compromised and controlled judiciary. Kufuata maagizo ya wanasiasa haraka haraka Mwigulu Nchemba kamuagiza Chief Justice! Nyerere hakuliona hili miaka 25 ya utawala wake na alikuwa mzalendo kweli kwel kuliko hawa wa sasa. Aliliona na alisema KIINGEREZA NI KISWAHILI CHA DUNIA NA SISI TUNAISHI DUNIANI HATUWEZI KUJITENGA NA DUNIA. Wanasiasa badala ya kuinua elimu wanakimbilia hukumu ziandikwe kiswahili mwishowe watasema ziandikwe kimasai na kisukuma na kinyakyusa.
 
These are the characteristics of a compromised judiciary.
 
Compromised and controlled judiciary. Kufuata maagizo ya wanasiasa haraka haraka Mwigulu Nchemba kamuagiza Chief Justice! Nyerere hakuliona hili miaka 25 ya utawala wake na alikuwa mzalendo kweli kwel kuliko hawa wa sasa. Aliliona na alisema KIINGEREZA NI KISWAHILI CHA DUNIA NA SISI TUNAISHI DUNIANI HATUWEZI KUJITENGA NA DUNIA. Wanasiasa badala ya kuinua elimu wanakimbilia hukumu ziandikwe kiswahili mwishowe watasema ziandikwe kimasai na kisukuma na kinyakyusa.
swali rahisi la kujiuliza ni Lugha ya Taifa ni ipi?
1. Kiingereza au

2. Kiswahili?
Bunge letu linaendeshwa kwa lugha ya kiswahili na nyaraka zake zote zinaandikwa kwa lugha ya taifa sasa iweje ionekane taabu kwa vyombo vingine kutumia lugha ya kiswahili?!

nauliza swali matumizi ya kiingereza ni kwa maslahi ya nani haswa?

1. Mtanzania au?

Lugha ya kiingereza itabakia kama lugha muhimu ya mawasiliano lkn sio lugha ya shughuli za kiserikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
si bure!
utakuwa na ubia na mabeberu
Huwa ninyi watu ni kichekesho. Umekazana asilimia 95 nchini wanajua Kiswahili fasaha. Umeyatoa wapi hayo? Wewe mwenyewe bila kukimbizwa unaandika kukuwa badala ya kukua! Lugha rahisi ya Kiingereza imewashinda. Siku hizi Watanzania wanajifunza Kichina. Msikimbilie Kiswahili kwa sababu Kiingereza kimewashinda. Kiswahili kikiwashinda mtaenda wapi? Mnakikimbia Kiswahili cha dunia? Kaeni tafuta sababu inayoleta ushinde kwa Kiingereza.
Mwingereza wa kawaida naye akiisoma hukumu haambulii kitu. Sheria ina istilahi yake. Na pia kuna Kiingereza cha sheria! Wanakijua watu wa sheria tu.
 
Wewe ndio mbabaishaji hasa. Tofautisha kati ya official na national language. Na jaji mkuu naye asije akapatikana na la kumpata katika suala kama hili. Isiwe alimsikiliza aso haya aliyesimama na kudai vifo vya korona visitajwe. Upumbavu uliompa uwaziri. Kusoma uchumi sio kuwa mchumi. Mchumi gani asojua umuhimu wa takwimu? Kufanya Kiswahili kuwa official kinyemela. Anzia kidato cha kwanza Kiswahili officially! Wimbo uliochakaa bila kuimbwa.
 
Huwa ninyi watu ni kichekesho. Umekazana asilimia 95 nchini wanajua Kiswahili fasaha. Umeyatoa wapi hayo? Wewe mwenyewe bila kukimbizwa unaandika kukuwa badala ya kukua! Lugha rahisi ya Kiingereza imewashinda. Siku hizi Watanzania wanajifunza Kichina. Msikimbilie Kiswahili kwa sababu Kiingereza kimewashinda. Kiswahili kikiwashinda mtaenda wapi? Mnakikimbia Kiswahili cha dunia? Kaeni tafuta sababu inayoleta ushinde kwa Kiingereza.
Mwingereza wa kawaida naye akiisoma hukumu haambulii kitu. Sheria ina istilahi yake. Na pia kuna Kiingereza cha sheria! Wanakijua watu wa sheria tu.
umemaliza kazi, umempa kibano.
 
Hongera kwa Jaji Mkuu kwa kuhakikisha Hukumu zote sasa zinaandikwa kwa kiswahili, maana itatusaidia sana watanzania kuelewa kilicho andikwa, hakika hii ni hatua kubwa na ya muhimu ktk upatikanaji wa haki kwa wananchi.

matumizi ya lugha ya kiswahili ni fahari na tunu kwa watanzania, nimekuwa nikiona mataifa mbali mbali kama vile: Urusi, China, uturuki, uarabuni n.k zikitumia lugha zao na zimefanikiwa sana ktk nyanja ya sheria, naamini pia Tanzania kwa mabadiliko haya ya matumizi ya kiswahili yatainua sana sekta ya sheria.

naaamini tasisi za kiswahili zilizo bobea tunazo, tunayo TUKI, BAKITA n.k kuna wabobezi wa kiswahili ambao wanaweza kabisa kutafsiri sheria zetu kwa lugha ya kiswahili.

Tudumishe utamaduni wetu, Lugha ndio kielelezo kikuu, wala hakuna dhambi yoyote kutumia lugha ya kiswahili, sisi sote ni watanzania/ waswahili hakuna haja ya kulazimisha kutumia kifaransa au kichina ktk shughuli zetu.

Lugha zingine kama; Kifaransa, Kingereza, Kichina, Kiarabu n.k zitumike kama lugha za mawasiliano tu lakini sio kendeshea shughuli zetu.
Safi hii ni habari mbaya kwa wale wanasheria wanaojitegemea maana walikuwa same time wanawazunguka wateja wao kwa kigezo cha lugha maana akoshajua mfeja lugha hajui wanatumia fursa
 
Back
Top Bottom