Kifo Cha Prof Ngowi kimeniuma kama nimempoteza kaka yangu Genius. Yani nilimpenda na kiukweli taifa tumepoteza kichwa. Jambo lakutisha sana uwenda mpaka sasa kama Taifa hatujajuwa umuhimu wa hiz think tank. Usije ukashanga Hit team ya taifa fulani imemmaliza. Why 😭 mtu mmoja aweza kuwa mchawi wa mapinduzi ya uchumi nakuliokoa taifa ktk dhiki na ukimuondoa huwez pata kichwa kama hiko tena.

Nilazima kama Taifa tujuwe tupo ktk mabadiliko makubwa ya uchumi na kama sijakosea huyu Prof was among RC that team. Kubadili fikra za vijana kutoka kuajiriwa na kujiajiri.

Prof Amelala amelala na maujanja yote yakulikomboa Taifa. Kiukweli Mungu ndie anajuwa ila nadiriki kusema Prof hajafa bali ameondoshwa na viumbe tusivyo viona je aligusa nini au alitegewa nini Mungu Mungu ndie anajuwa. Kifo Cha Prof Ngowi kinatukumbusha kumbukizi zakutisha kwenye same barabara Moja Waziri Mkuu Sokoine, Pili Mch Mtikila tatu Mzee Kombe na mwisho😭😭😭.

Tusipo fungua macho tutakuwa vipofu natusipo kuwa vipofu tutakuwa mazezeta... 😭😭😭🤐🤐🤐🤐

Hii barabara inatisha sana wajuvi tujuzen.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mkuu inataka kumaanisha vijana wa paka mrefu wamefanya yao!!!?
 
Unataka kusokomezewa. Wapo wanaohitaji hiyo huduma watakucheki
kusokomezwa mbna nasokomezwa kila siku, vipi nawee unataka tu share ukuni m1 na mie? Huenda nafaidi sana eti eeeh?

Wee ndo unatafuta soko kupitia mie, poleeeeeeh sana, tafuta basha kivyako, msieeeew.
 
kusokomezwa mbna nasokomezwa kila siku, vipi nawee unataka tu share ukuni m1 na mie? Huenda nafaidi sana eti eeeh?

Wee ndo unatafuta soko kupitia mie, poleeeeeeh sana, tafuta basha kivyako, msieeeew.
Mwanaume unasonya. Hatari
 
Habari Wote.

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.

Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.

Imetokewa na,

Ofisi ya Mawasiliano

View attachment 2166663
Profesa Honest Ngowi enzi za uhai wake
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani. Lori iliacha njia na kuilalia gari ya Ngowi. Alitoka kwenye ajali akiwa majeruhi, amefariki akiwa hospitali.

Pia soma > Dkt. Honest Ngowi aichambua sekta ya gesi na kukiri Serikali imejipanga


=======

Professor Honest Prosper Ngowi (PhD Economics) alikuwa mkuu wa idara ya kozi fupi, utafiti na ushauri chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya ushauri ya ANO. Katika maisha yake amekuwa mtafiti, mshauri na kuchapisha machapisho ya kitaaluma zaidi ya 60, tafiti zaidi ya 70 pia makala zaidi ya 250 kwenye magazeti.

Prof. Ngowi amebobea kwenye uchumi wa maendeleo na biashara hasa kwenye uchumi mkubwa, biashara ya kimataifa, uwekezaji wa kigeni, ujasiriamali, uchumi wa mafuta na gesi na mengineyo. Prof. Ngowi pia amefanya kazi kama msahihishaji wa nje kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha Makerere, Udsm, North West University(Afrika kusini) na vingine vingi.
Bonge moja ya cv yake hii hapa ila ni ya nyuma kidogo 2018
 

Attachments

  • Prof Ngowi CV...doc
    109.5 KB · Views: 13
R.I.P

Hii barabara isipotanuliwa na kuweka dual carriage way tutaisha sana kwa kweli lawama tutawapa sana madereva lakini ukweli tuuseme barabara hii ni bado ya kizamani hailingani na matumizi ya idadi ya magari iliyopo sasa.

Wanasiasa hebu tumieni hicho kiwango cha posho zenu kuokoa maisha ya watu kwa ajali ambazo huenda zingeepukika.

Hivi nchi mnazoenda kutembelea hamjifunzi tu kitu cha kufanya?

Oneni aibu kwa kuchelewa kujenga dual carriage way ya dar to morogoro tunazidiwa na nchi kama Zambia kweli?
Nimelipigia kelele sana hilo...mara nyingi mimi nimeona jinsi tunavyokoswa koswa humo njiani
 
Mmefukuza madereva wazuri kwa sababu za kipuuzi za vyeti fake mara sijui dereva naye awe form four wakati mbunge ni darasa la saba, pumbavu kabisa.

Qualification ya driver ni driving license na siyo hawa waliokosa ajira kwenye soko la ajira na kukimbilia udereva, kuendesha Passo yako ni tofauti kabisa na professional driving.

Ukiwa unasafiri jihadhari sana na hizi plate namba za STL, DFP na SU, hakuna madereva humo siku hizi ndio mitambo ya kupeleka watu kuzimu.
Loli lililobeba Contena liligonga Noah Kisha kuangukia gari aliyopanda Pro sasa hapo dereva wa SU amekosea nini?
 
Back
Top Bottom