Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Habari Wote.

Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.

Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.

Imetokewa na,

Ofisi ya Mawasiliano

ngowi.jpg

Profesa Honest Ngowi enzi za uhai wake
Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani. Lori iliacha njia na kuilalia gari ya Ngowi. Alitoka kwenye ajali akiwa majeruhi, amefariki akiwa hospitali.

Pia soma > Dkt. Honest Ngowi aichambua sekta ya gesi na kukiri Serikali imejipanga

1.jpg
2.jpg

=======

Professor Honest Prosper Ngowi (PhD Economics) alikuwa mkuu wa idara ya kozi fupi, utafiti na ushauri chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya ushauri ya ANO. Katika maisha yake amekuwa mtafiti, mshauri na kuchapisha machapisho ya kitaaluma zaidi ya 60, tafiti zaidi ya 70 pia makala zaidi ya 250 kwenye magazeti.

Prof. Ngowi amebobea kwenye uchumi wa maendeleo na biashara hasa kwenye uchumi mkubwa, biashara ya kimataifa, uwekezaji wa kigeni, ujasiriamali, uchumi wa mafuta na gesi na mengineyo. Prof. Ngowi pia amefanya kazi kama msahihishaji wa nje kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha Makerere, Udsm, North West University(Afrika kusini) na vingine vingi.


 
R.I.P

Hii barabara isipotanuliwa na kuweka dual carriage way tutaisha sana kwa kweli lawama tutawapa sana madereva lakini ukweli tuuseme barabara hii ni bado ya kizamani hailingani na matumizi ya idadi ya magari iliyopo sasa.

Wanasiasa hebu tumieni hicho kiwango cha posho zenu kuokoa maisha ya watu kwa ajali ambazo huenda zingeepukika.

Hivi nchi mnazoenda kutembelea hamjifunzi tu kitu cha kufanya?

Oneni aibu kwa kuchelewa kujenga dual carriage way ya dar to morogoro tunazidiwa na nchi kama Zambia kweli?
 
Back
Top Bottom