Profesa Elifas Bisanda amemaliza kila Kitu kuhusu PT, JWTZ japo sijajua kwanini hajawataja na TISS ambako pia kuna Mapungufu kwa sasa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
"Sasa ifike muda tuambiane Ukweli nashauri kuanzia sasa Watu wanaoajiriwa katika haya Majeshi yetu ya Polisi na Jeshi la Wananchi wawe ni wale tu waliofaulu kwa Division One Shuleni au First Class Degree Vyuo Vikuu na tuachane Kuajiri Failures katika hizi Taasisi kwani hawataweza Kusaidia kufanya Tafiti za Kisasa za Kijeshi, kuwa Wabunifu Kimedani na Kushindana na Wenzao wengine ambao wameshatuacha na huenda wanatushangaa pia", amesema Profesa Elifas Bisanda ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Vyuo Vikuu vya Polisi na Jeshi na pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria.

Chanzo: Millard Ayo

Haya Wazandiki si huwa mnajifanya Kutuchukia na hata Kututishia akina Mightier na JamiiForums Great Thinkers tukisema haya? Sasa mchukieni basi na huyu Profesa Bisanda kwa huu Ukweli wake mtupu.

Japo wanaficha na Ushauri waliopewa katika Ziara zao huko nchini Rwanda, ila Wafuatiliaji wa Mambo magumu na mazito tumeambiwa kuwa hata IGP Sirro na CDF Mabeyo walipoenda (walipotembelea) Rwanda waliambiwa hivi hivi kuhusu Taasisi zao kama ambavyo Profesa Bisanda ameshauri.

Tanzania inahitaji Maprofesa Makini na very Intelligent kama huyu Elifas Bisanda na kwa haya Madini yake popote alipo (ulipo) Mightier nakuamkia Shikamoo na hakika ulistahili kuwa Profesa na umeupiga mwingi sana juu ya hili.
 
Nikikumbuka nilipoenda kwenye interview ya kujiunga na jeshi miaka kadhaa iliyopita nikaambulia kupigwa KOFI kubwa sana na mgongo kisha nikaambiwa.

“ dogo nenda chuo hapa tunataka form six wenye four hukuona tangazo??” nikapoa nikaanza kurudi home nimekuwa mnyoonge.
 
Kipindi tupo chuo kuna jamaa alikia anapata gpa ya 3.3, 3.4, 3.7 alikua anarange hapo kwenye mitihani ya mwisho, lkn tokea nieanza kusoma sijakutana na jamaa smart kama huyo alikuwa na uwezo wa kueleza hizi sijui financial policy monetary na mwenzie, alakua anafanya uchambuzi wa zile theory za economics alikuwa na uwezo wa kuongelea tukio la uchumi la hata mmika ya 1920 huko na natoa daza za kuaminika.

Huyu mtu alikua mzuri sana japo performance yake kwenye mitihani hii ya darasani ilikua sio kubwa sana. Lkn ukiangalia waliopata sijui first class hata kujieleza mtu hawezi wengi walisha zoea kumeza na kwenda kutapika kwenye exam room mtu unamuuliza unamaoni gani kwenye financial crisis iliyokea 2008 huko na nini kifanyike hawezi kujieleza. Kwa maoni yangu performance ya darasani isiwe kigezo namba moja huko tiss wajaribu ku tafuta njia nyingine
 
Nikikumbuka nilipoenda kwenye interview ya kujiunga na jeshi miaka kadhaa iliyopita nikaambulia kupigwa KOFI kubwa sana na mgongo kisha nikaambiwa
“ dogo nenda chuo hapa tunataka form six wenye four hukuona tangazo??” nikapoa nikaanza kurudi home nimekuwa mnyoonge..
😅😅😅😅😅😅😅 we unaendaje na divison 1 jeshini
 
Pamoja na kukubaliana na Prof lakini tatizo kubwa ni mindset ya vyombo vyote vya dola Tanzania, hasa vinavyohusika na uchunguzi wa makosa ya jinai

Kutesa watuhumiwa ili waseme au waandike na ku saini kile wachunguzi/wapelelezi wanachokitaka ni dalili kua hawana weledi, maarifa wala maadili ya kazi zao. Ni wahuni tu na majambazi kama majambazi wengine tu

TAKUKURU kwa mfano, wanaajaari watu wenye shahada za kwanza na kuendelea wakiwa na professions tofauti tofauti. Lakini hadi pale serikali ya awamu ya sita ya mama Samia ilipoingia madarakani na kukemea hilo, wao walikua wanaongoza kwa kupiga na kutesa watuhumiwa kisha kuacha kuwapeleka hospitali ili tu watimize haja zao binafsi za kupata conviction mahakamani ili wapandishwe vyeo!!!!

Bahati nzuri utawala wa mama Samia umeliona hilo na kulisimamisha japo watendaji wanalipinga chinichini wakitaka waachiwe mamlaka ya kuminya haki za binadamu!

Inatakiwa system overhaul na elimu juu ya haki na wajibu kwa vyombo vya ulizi na usalama, vyombo vya uchunguzi wa makosa ya jinai na vyombo vyote vya utoaji haki kwa ujumla. Vinginevyo wanachofanya ni uhalifu tena ni crime against humanity
 
Kipindi tupo chuo kuna jamaa alikia anapata gpa ya 3.3, 3.4, 3.7 alikua anarange hapo kwenye mitihani ya mwisho, lkn tokea nieanza kusoma sijakutana na jamaa smart kama huyo alikuwa na uwezo wa kueleza hizi sijui financial policy monetary na mwenzie, alakua anafanya uchambuzi wa zile theory za economics alikuwa na uwezo wa kuongelea tukio la uchumi la hata mmika ya 1920 huko na natoa daza za kuaminika. huyu mtu alikua mzuri sana japo performance yake kwenye mitihani hii ya darasani ilikua sio kubwa sana. Lkn ukiangalia waliopata sijui first class hata kujieleza mtu hawezi wengi walisha zoea kumeza na kwenda kutapika kwenye exam room mtu unamuuliza unamaoni gani kwenye financial crisis iliyokea 2008 huko na nini kifanyike hawezi kujieleza. Kwa maoni yangu performance ya darasani isiwe kigezo namba moja huko tiss wajaribu ku tafuta njia nyingine
Off point, out of Context and you must be a very Short Sighted Creature wasting your time on Earth.
 
prof mzima kuwaza divi 1 ndio ugunduzi,tunafeli kama taifa linalosikiliza wasomi.

yeye ni prof atuambie amefanya utafiti gani uliosaidia taifa baada ya kufauli vilivyo,badala ya kukweza div 1 kwanza.
 
Kipindi tupo chuo kuna jamaa alikia anapata gpa ya 3.3, 3.4, 3.7 alikua anarange hapo kwenye mitihani ya mwisho, lkn tokea nieanza kusoma sijakutana na jamaa smart kama huyo alikuwa na uwezo wa kueleza hizi sijui financial policy monetary na mwenzie, alakua anafanya uchambuzi wa zile theory za economics alikuwa na uwezo wa kuongelea tukio la uchumi la hata mmika ya 1920 huko na natoa daza za kuaminika. huyu mtu alikua mzuri sana japo performance yake kwenye mitihani hii ya darasani ilikua sio kubwa sana. Lkn ukiangalia waliopata sijui first class hata kujieleza mtu hawezi wengi walisha zoea kumeza na kwenda kutapika kwenye exam room mtu unamuuliza unamaoni gani kwenye financial crisis iliyokea 2008 huko na nini kifanyike hawezi kujieleza. Kwa maoni yangu performance ya darasani isiwe kigezo namba moja huko tiss wajaribu ku tafuta njia nyingine

kimsingi watu waliobadilisha dunia hii hawakuwa wazuri darasani kiwango cha kushtua.
 
prof mzima kuwaza divi 1 ndio ugunduzi,tunafeli kama taifa linalosikiliza wasomi.

yeye ni prof atuambie amefanya utafiti gani uliosaidia taifa baada ya kufauli vilivyo,badala ya kukweza div 1 kwanza.
Hasira zako hizi ( Povu lako hili ) inaonyesha kuwa Sindano ya Profesa Elifas Bisanda imekuingia Kisawasawa tena Mfupani kabisa. Pole....!!!
 
Futa ujinga wako TISS iko vyema na naomba usi ifananishe na hayo makolokolo ambayo yako chini ya afande SIRRO.
 
Mbona unachekesha we mtu. Hizi fikra finyu Sana sikutegemea profesa kuongea pumba mtupu. Unadhania kazi za jeshi ni kufanya utafiti peke yake shame on you
 
Back
Top Bottom