Pumzika kwa amani Prof MassaweLala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia
Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako
Mwendo umemaliza 💔💔💔
---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.
Kwani ugonjwa gani ambao hauui?Surua,kifua kikuu,ndui,pepopunda,kifaduru na kadhalika zote zina chanjo na zinaua.Kinachotakiwa kufanyika ni binadamu kutumia akili yake optimally.Kwamba na hao wa Ulaya na maeneo mengine wanaoendelea kufa hawana akili?
Unaweza kutoa jawabu la wenye akili wanachofanya waepuke kifo? Hali ni mbaya CDC na FDA wako kwenye mijadala mizito kuhusu Booster kwa waliokwishachanjwa dozi zote, hebu tupe mbadala mkuu.
NdiyoHivi ndio yule mwenye pale Morocco au maana namsikiaga tu ila simjuagi
Ulikuwa unaishi nchi IPI? Mbona enzi za Magu watu wamekufa sana mpaka barabaran unaokota watuMlishe mwanao chakula bora usisubirie kununua antibiotics. Prof amemaliza mwendo apumzike kwa Amani.
Ametufundishia madaktari wengi sana.
Swali chokonozi wakati ule tulipokuwa tuna mtegemea Mungu kwanza na kuhimizwa hivyo na kipindi cha sasa ambapo tunahimizwa kutegemea barakoa, chanjo na akili zetu wapi misiba imekuwa mingi zaidi? Jibu mnalo nafikiri na mjisahihishe ili pengine huruma ya Mungu na Neema yake ituokoe kama Taifa.
Mungu wa Mbinguni hadhihakiwi hata mara moja. Mtavuna mlicho panda.
Ulikuwa unaishi nchi IPI? Mbona enzi za Magu watu wamekufa sana mpaka barabaran unaokota watu
Very sad. Mungu afariji Familia yake.Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia
Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako
Mwendo umemaliza 💔💔💔
---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.
Duh.! Ni kama mzaha hivi...R.I.P Daktari2005 nilipata huduma toka kwa huyu mzee pale morocco. Binti yangu aliyezaliwa tu akiwa na siku kama 6. Alikuwa akilia sana muda wote. Akipewa nyonyo ananyonya baada ya muda kidogo analia tena.
Nikampeleka pale. Sitakaa nidharau taaluma ya mtu. Hata akiwa mkuluma.
Mzee masawe akamwambia wife akamue maziwa ajazi kikombe kilikuwa pale. Kukamua kumbe mama maziwa hana na mtoto analia sababu hashibi. Nikaanza kuingia super market kununua mazuwa ya kopo. Kwa sasa ni mkubwa na yupo form two pale St marie Eugen.
Pumzika kwa amani mzee wangu Masawe.
Kwani ugonjwa gani ambao hauui?Surua,kifua kikuu,ndui,pepopunda,kifaduru na kadhalika zote zina chanjo na zinaua.Kinachotakiwa kufanyika ni binadamu kutumia akili yake optimally.
Sasa hivi Corona ina chanjo na bado inaua lakini binadamu angekaa kimya bila kufanya lolote ingeua zaidi.Kinachotakiwa kufanyika ni kuongeza jitihada zaidi na wala siyo kubeza jitihada zinazoendelea.
Imani bila matendo imekufa.Binadamu wakikaa tu chini bila ya kufanya lolote na kusema kuwa Mungu ni mkubwa sana wataisha wote.Cha msingi ni kuendelea kutumia akili tulizo nazo.Hata mbuyu ulianza kama mchicha,usitegemee Corona ikamalizwa yote ndani ya siku moja.Kila kitu huhitaji muda.
Wazazi wa kule kwetu kwa Mtogole hawamjui huyo.Alikuwa Daktari Mbobovu aliyesaidia watoto wengi, mitaa yote ya Dar nani mwenye mtoto asiyemjua? Apumzike kwa amani.
Au marehemu?Unamaanisha wajinga ni kina nani!?
Waliofiwa au aliowahudumia?
Pole sanaRIEP baba Furaha...Umetibu watoto wetu ambao nao wameshakuwa ma dr. Sasa...Sleep well baba yetu
Mi sipo kinyume na taaluma ya mtu lakini approach ya Magufuli ya kututaka tusiipe airtime corona bali tumwangalie Mungu ni sawa na ile ya approach ya Musa jangwani kwamba atengenenze nyoka wa shaba ili wale watakaoinangalia nyoka ile watapona. Watakaokazana kutazama chini ili wasiumwe na nyoka watapukutika.Mlimwita 'mjinga/nchi inaongozwa na washamba' kwa maamuzi ya kuhimiza kumtegemea Mungu kwanza na mengineyo. Ngoja tuwaone wajanja wa kutegemea akili zao na si Mungu watakapo tufikisha kama Taifa.
Unaweza kuthibitisha kuwa wameuawa na chanjo ya Corona na wala siyo kwa kitu kingine chochote kile?Hatujawahi kusikia watu walio uliwa na kuambukizwa na chajo hizo nyingine kwa jinsi ya na chanjo hii ya corona.
Tumeanza kusikia hii ya corona ikituulia wapendwa wetu kwa namna ya kuogofya acha wakiobanwa na matumbo ya kuhara na kukosa nguvu mwilini, kifo kiliwadip/beep baada ya kuchanjwa..
Ndio maelekezo yake pia.... lakini shida ikitokea hamna namna unakwenda kufuata msaada.Mlishe mwanao chakula bora usisubirie kununua antibiotics. Prof amemaliza mwendo apumzike kwa Amani.