TANZIA Profesa Augustine Massawe, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto afariki dunia

Dah! Inasikitisha sana. Mwezi uliopita nilipeleka watoto kule hospitali yake moya Bunju nafikiri. Nikasema afadhali amepata eneo kubwa na ameboresha miundo mbinu. Kumbe yeye anapanga yake na Mungu anamipango yake. So sad!
Imempata kama ya Dr wa masikio aliyekuwa na hospitali yake pale Magomeni; alikuwa na kaeneo kadogo ka kupanga akanunua nyumba akajengo ghorofa, alivyohamia tu Mungu akamchukua. RIP Prof Massawe
 
Lala salama baba. Tunakushukuru sana wa huduma Mungu aliyokuwa amekujalia

Uliitumia vyema karama Mungu aliyoiweka ndani yako

Mwendo umemaliza 💔💔💔

---
Daktari Bingwa wa Watoto Dr Augustine Massawe wa Furaha Medical amefariki Dunia leo Jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka kwa familia ni kwamba Dkt. Massawe amefariki asubuhi hii katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kwa matibabu.

Dr Dulla is gone, and massawe is gone too😭😭😭
 
Rest in peace Doctor

Mara ya mwisho mwanangu kapata jipu matata sana kichwani, kila mtu anasema hilo la kutumbua tu.

Nikafunga safari mpaka Bunju, mzee kacheki kanipa antibiotics moja tu. Siku tatu jipu kwisha kabisa.

Tupendane jamani, you never know the last time unaongea na mtu

Mlishe mwanao chakula bora usisubirie kununua antibiotics. Prof amemaliza mwendo apumzike kwa Amani.

Ametufundishia madaktari wengi sana.

Swali chokonozi wakati ule tulipokuwa tuna mtegemea Mungu kwanza na kuhimizwa hivyo na kipindi cha sasa ambapo tunahimizwa kutegemea barakoa, chanjo na akili zetu wapi misiba imekuwa mingi zaidi? Jibu mnalo nafikiri na mjisahihishe ili pengine Huruma ya Mungu na Neema yake ituokoe kama Taifa.

Mungu wa Mbinguni hadhihakiwi hata mara moja. Mtavuna mlicho panda.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom