Profesa Assad: Wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,722
Dar es Salaam, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi.

Profesa Assad amesema hayo leo Jumamosi Aprili 10, 2021 katika uzinduzi wa mfululizo wa midahalo ya umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).

“Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, hao ni wasaka fursa tu na kawaida yao hawatusaidii chochote, nchi inahitaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi,” amesema Profesa Assad.

Msomi huyo alitolea mfano kutumbuliwa kwa watendaji bila hata kufuata sheria na haki za anayetumbuliwa akisema watu walishangilia na kulikuza na sasa hao hao wanashangilia mpaka leo wakati wanapaswa kukosoa mambo yanapokwenda kinyume.

Amesema ni jambo la kawada watu kuwa hivyo kwa kuwa binadamu wengi ni wasaka fursa, wanaangalia upepo unaendaje, "wakati ule walikuwa wanashadadia mambo yakifanywa hata bila kufuta taratibu za kisheria na sasa wanashadadia hata mambo ambayo yanatofautiana na yale."

Kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Profesa Assad amesema kuna haja ya Serikali kutoa nyaraka ya mradi huo kuiweka hadharani ili wananchi wasome, waangalie faida na hasara zake na watoe maoni yao kama ni mzuri au mbaya.

“Nashindwa kusema kama mradi ni mzuri au ni mbaya maana hiyo nyaraka sijaiona lakini Serikali ikitoa taarifa, ikaitoa Ikulu tutatoa maoni nami ni mzuri katika eneo hilo la uchambuzi,” amesema Profesa Assad.

=====

My take: Tukiwa Na ma professa vichwa 10 tu kama huyu assad katika baraza la mawaziri na bungeni Basi tutatoboa...Asante Assad endelea kuwaelekeza.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Naona kama Prof. ana kinyongo na kisasi ndani yake, maneno yake yanaonesha hivyo. Kama ndivyo asamehe na kuruhusu mambo mengine yaendelee na itakuwa vema kama atajikita na kushauri uongozi uliopo.
 
Ujumbe umfikie mzee wa U-turn Ndugai

Ndugai anaongoza muhimili mkubwa sana ktk nchi yetu lakini kiukweli anapwaya sana ktk nafasi hiyo,,, Nguvu ya muhimili huo umekuwa dhaifu sana chini ya uongozi wake

Natamani hata kiongozi wa huo Mhimili angekuwa Mussa Zungu (ambae kwa mara kadhaa amekuwa Mwenyekiti wa vikao pale bungeni), huyu angalau ana kariba za Marehemu mzee Samwel Sitta
 
Unadhani kusema wanaounga mkono kila kitu ni wasaka fursa sio kushauri? Unataka ushauri upi kutoka kwa prof?
@ghost,polesana pamoja na profesa katoa tathmini hiyo ,bado mwilapwa hajaelewa na bado yuko GT JM...basi kunaumuhimu jf kufanya usajili upya wa member.....
 
Ushauri mzuri kabisa ,
Heri tuwe na msimamo wa kueleweka na regime ikiwa haiendi tunavyoamini inatakiwa tunasubiri regime yetu
 
'View attachment 1748548
IMG_20210409_214545.jpg
 
Back
Top Bottom